Thursday, April 26, 2018

Uzinduzi wa malori wa kustajaabisha zaidi katika kanda

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CFAO Motors, Marius Prinsloo (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Dar Es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa Malori mapya ya kisasa ya Mercedes Benz aina ya Actros na Arocs. Wengine kwenye picha kutoka kulia ni Maneja Mauzo wa MB Trucks Africa, Hansjorg Richter, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Huduma kwa Wateja Mercedes Benz Trucks Africa, Torsten Bauerheim na mwisho kushoto ni Meneja Chapa wa Mercedes Benz Tanzania, Jerome Sentimea. 
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Huduma kwa Wateja Mercedes Benz Trucks Africa, Torsten Bauerheim (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Dar Es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa Malori mapya ya kisasa ya Mercedes Benz aina ya Actros na Arocs. Wengine kwenye picha kutoka kushoto ni Meneja Chapa wa Mercedes Benz Tanzania, Jerome Sentimea, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CFAO Motors, Marius Prinsloo na Maneja Mauzo wa MB Trucks Africa, Hansjorg Richter
Meneja Chapa wa Mercedes Benz Tanzania, Jerome Sentimea (wa kwanza kushoto ) akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Dar Es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa Malori mapya ya kisasa ya Mercedes Benz aina ya Actros na Arocs. Wengine kutoka kulia ni Maneja Mauzo wa MB Trucks Africa, Hansjorg Richter, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CFAO Motors, Marius Prinsloo na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Huduma kwa Wateja Mercedes Benz Trucks Africa, Torsten Bauerheim


·  Mercedes-Benz inapeleka mbele historia ya malori yenye nguvu nchini TANZANIA

·       Malori yote mapya aina ya Actros na Arocs yamezinguliwa
Tarehe 8/02/2019 Jijini Dar es salaam. Actros mpya kabisa: Ni malori ya kuaminika na yenye ufanisi kwaajili ya masafa marefu na usamabazaji yamezinduliwa leo katika mji mkuu wa Tanzania.

Akiongea katika hafla hiyo ya kupendeza, Mkurugenzi wa Mauzo na Huduma kwa Wateja wa Malori ya Mercedes Benz Afrika Bwana Mr Torsten Bauerheim akisema, 'Malori yote mapya ya Actros na Acros yanakuja na injini yenye ufanisi yenye silinda 6 katika mstari, vyumba vya dereva vya kisaa vinavyoruhusu hewa kupita na Mercedes PowerShift 3 ya kisasa, injini ya kujiendesha yenyewe zikiwa na miundo mbalimbali tofauti kutegemeana na mazingira ya kanda husika.  Aliongeza kuwa, Malori yote mapya ya Actros ni ya kuaminika na ya uhakika kwaajili ya ujenzi na matumizi katika barabara za vumbi na zote zimepitia majaribio makali ya ubora ya zaidi ya kilomitea milioni 60 kabla ya kufanya uzinduzi wa soko.

Mkurugenzi Mtendaji wa wasambazaji walioithibishwa wa Mercedes-Benz, CFAO Motors Tanzania Ltd, Bwana Marius Prinsloo amesema kwamba 'Maloti mapya ya Actros na Arocs yanatoa kiwango cha ziada cha uimara, ufanisi katika matoleo ya malori ya Mercedes-Benz Yakiwa yametengenezwa katika kiwanda cha malori kikubwa kuliko vyote duniani nchini Ujerumani, Malori haya yanakuja katika aina mbalimbali mahususi kwaajili ya soko letu la Tanzania - yakiwa yamebuniwa na kutengenezwa kuhimili mazingira magumu ya uendeshaji.

Yamejaribiwa kwa kina duniani kote, katika barabara za aina zote na katika mazingira magumu zaidi, magari haya ni mifumo bora zaidi kwaajili ya kazi ngumu. Majaribio yalijumuisha jumla ya zaidi ya kilometa milioni 6 za mbio za ustahimilivu zilizofanywa na kituo cha majaribio ya malori ya Mercedes-Benznchini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu.
Aliongeza kuwa 'Chumba kipya cha pekee cha dereva kinajivunia kiwango cha juu cha vifaa na mazingira mazuri ya ndani, wakati uendeshaji ni rahisi na wakustarehesha . Aina zote mbili za malori ya Actros na Arocs zinavutia kwa teknolojia ya kisasa zaidi na mfumo wa kuaminika wa uendeshaji kutokea chanzo kimoja.  Injini zenye ustahimilivu, zenye nguvu na zenye ufanisi zinapatikana katika aina za utoaji moshi wa Euro III, IV na V, ikiwa inatoa aina mbalimbali za nguvu ya msukumo kuanzia 240 kW (326 hp) mpaka 460 kW (625 hp). Ikiwa imeunganishwa na toleo la hivi karibuni la Mercedes PowerShift 3, gia boksi ya kujiendesha yenyewe, malori ya Actros na Arocs yanafikia kiwango cha juu cha ufanisi wa mafuta, ikiwa inachangia kuongeza faida za uendeshaji

Actros mpya zimetengenezwa kwaajili ya usafirishaji wa masafa marefu pamoja na usambazaji wa mizigo mizito. Zinapatikana na mpaka aina 22 tofauti za chumba cha dereva na zinakuja katika matoleo ya chuma au ya kushikiliwa na upepo. Kwaajili ya mazingira magumu ya uendeshaji, Actros zinapatikana katika injini zenye nguvu za 15.61 na kasi ya 16 na gia boksi ya kujiendesha yenyewe ya Mercedes PowerShift 3

'Arocs mpya ya kustaajabisha iko kwaajili yako pale utakapo kuwa unahitaji ustadi wa kipekee - iwe katika shughuli za ujenzi mbali na barabara za lami. Malori ya Arocs yenye ustahimilivu mkubwa yanaweza kufanya kazi katika mazingira magumu zaidi ya barabara za vumbi mbali na bara bara za lami. Arocs zinapatikana kama Chassis-, Mixer-, Tipper- na aina mbalimbali za uendeshaji - kuanzia miundo ya 4x2 mpaka 8x8 na uzito (GCW) wa mpaka kufika tani 250.

Kwa kudokeza, Actros na Arocs yanaweka viwango vipya pale inapokuja kuhusu suala la usalama na mifumo ya usaidizi, inayomsaidia dereva na kuokoa maisha. Bwana Torsten Bauerheim alihitimisha.


Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote Mjini Iringa


 Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2018 mkoani Iringa kwa jina la usanii PPT akitoa burudani kwenye jukwaa la Tigo Fiesta
Msanii wa Bongo Fleva Chege akiwa kwenye jukwaa la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote usiku wa kuamkia Jumatatu tamasha lililofanyika  kwenye uwanja wa Samora Mjini Iringa

Mkuu wa Wilaya ya Iringa , Richard Kasesela akilishwa keki na msanii Chege ambaye usiku wa Tigo Fiesta mjini Iringa ilikuwa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa

Mkuu wa Wilaya ya Iringa , Richard Kasesela (mbele kulia) akicheza pamoja na wasanii waliotoa burudani kwenye Tamasha Kubwa la Tigo Fietsa 2018 Vibe Kama Lote  uwanja wa Samora Mjini Iringa Usiku wa kuamkia jumatatu

Nyota wa Iokote Maua Sama akitoa burudani kwenye Jukwaa la Tigo Fiesta Iringa.



Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote 2018 limeendelea usiku wa kuamkia jumatatu kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa. Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa kampuni ya simu za mkononi Tigo kudhamini tamasha hilo.
Akizungumza mbele ya umati wa mashabiki waliohudhuria tamasha hilo Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini, Richard Kasesela amepongeza kampuni ya Tigo kwa kuwaletea burudani na fursa mbalimbali kwa wakazi wa Iringa. "  Hii ni fursa ya pekee kwa wakazi wa mji huu ambayo kampuni ya Tigo imetuletea kwa mara nyingine ndani ya mkoa huu" Ukiondoa Burudani, pia wafanyabiashara wamenufaika sana ndani ya wiki nzima alisema Kasesela.
Pia mkuu huyo wa wilaya aliweza kupata nafasi ya kumkabidhi zawadi ya Keki kwa msanii Chege Chigunda kwa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake.
Kwa upande wa Burudani wasanii wa kundi la Weusi ndio waliofunika kwenye tamasha hilo ilipopelekea mashabiki kuomba wasitoke kwenye jukwaa na kundi la Weusi walifanya hivyo hadi mwisho wa shoo kwa kuimba nyimbo zao nyingi za kuvutia zikiwemo, Madaraka,Swagire, NiCome na nyingine nyingi.
Mdhamini mkuu wa msimu huu, kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki kufurahia promosheni zake tatu murwa katika msimu hii wa vibes. ‘Data Kam Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+.

Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa Sumbawanga, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 5,000 pekee badala ya TSH 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim, Wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya  http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.

TIGO YAZINDUA PROMOSHENI YA ‘JIGIFTISHE’ AMBAPO SHILINGI MILIONI 600 ZITATOLEWA KWA WATEJA NA KUWAFANYA MAMILIONEA MSIMU HUU WA SIKUKUU

Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed (kushoto), Meneja Uhusiano wa Tigo Woinde Shisael (kati) pamoja na Balozi wa promosheni ya Tigo Jigiftishe, Lucas Mkenda almaarufu Joti (kulia) wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Jigiftishe itakayowapa wateja wote watakaotumia huduma za Tigo katika msimu wa sikukuu fursa ya kushindania jumla ya shilingi 600 milioni. 
Mkuu wa Masoko wa Tigo, Tarik Boudiaf (kushoto), Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed (wa pili kushoto), Balozi waTigo Lucas Mkenda almaarufu Joti (katikati), Meneja Mawasiliano Woinde Shisael (wa pili kulia) pamoa na Mkuu wa Bidhaa za Tigo Pesa, James Sumari (kulia) wakizindua promosheni ya Jigiftishe itakayowapa wateja wa Tigo fursa ya kushinda hadi TSH 50 milioni katika msimu huu wa sikukuu.

Wateja watakaoongeza salio au kuweka Pesa Kwenye Tigo Pesa au Kutumia huduma yoyote ya Tigo watapata nafasi ya kushinda zawadi nono za hadi TSH milioni 50!  
Dar es Salaam, 15 Novemba 2018; Tigo Tanzania - kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, itawezesha wateja wake kuwa mamilionea baada ya kuzindua promosheni kubwa zaidi itakayogawa kiasi cha TSH milioni 600 katika msimu huu wa sikukuu.

Promosheni hiyo ya kipekee ya ‘JIGIFTISHE’ kutoka Tigo katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka Mpya itawafanya zaidi ya wateja 450 kuwa mamilionea ndani ya siku 45, kutokana na kutumia huduma za Tigo pekee. Ni rahisi na hakuna kujiunga kwenye promosheni hii.

‘Wateja wa Tigo watakaoweka pesa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa, kuongeza salio au kununua simu janja kwenye maduka yote ya Tigo au kutumia huduma zozote za Tigo katika kipindi hiki cha sikukuu watapata fursa ya kujishindia TSH milioni 1 kila siku au TSH milioni 10 kila wiki. Pia kutakuwa na zawadi kubwa za TSH milioni 15, TSH milioni 25 au TSH milioni 50 zitakazotolewa mwishoni mwa promosheni hii ya JIGIFTISHE!’ Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Akibainisha vigezo vya ushiriki katika promosheni hiyo ya JIGIFTISHE, James Sumari, Mkuu wa Bidhaa za Huduma za Tigo Pesa wa Tigo alisema kuwa ili kupata fursa ya kushinda, wateja wa Tigo wanahitaji kununua kifurushi chochote kwa njia yoyote (ikiwemo kupitia *147*00#, *148*00# au kuongeza muda wa maongezi kwa njia ya kielektroniki, kadi au kupitia Tigo Pesa) au kufanya miamala ya Tigo Pesa kupitia *150*01# katika msimu huu wa sikukuu.

‘‘Ni rahisi sana! Hakuna kufanya kitu chochote maalum ili uweze kushinda. Unachohitaji kufanya ni kuendelea kutumia huduma au kununua bidhaa za Tigo ili upate nafasi ya kuwa milionea!” Woinde alisisitiza.

Kila muamala utakaofanyika utampa mteja nafasi moja ya kushiriki katika droo, na wateja wanaweza kutazama nafasi zao za kushinda kwa kupiga *149*22#. Kadri unavyofanya miamala zaidi ndivyo unavyojiongezea nafasi za kushinda.

Promosheni hii ya JIGIFTISHE itakayojaza mifuko ya wateja na manoti na kubadilisha maisha yao  inathibitisha kuwa Tigo ndio mtandao unaotoa huduma bora zaidi za kidigitali kwa wateja wake na kuwawezesha kufurahia msimu huu wa sikukuuu huku wakimaliza au kuanza mwaka mpya kwa mtindo tofauti.

‘Hii ndio njia yetu ya kuwashukuru wateja wetu wote kwa kuendelea kutumia huduma zetu bora, zenye kasi ya juu na rahisi. Tunachukua fursa hii kuongeza tabasamu katika nyuso za wateja wetu,’ Woinde alisema.
Tayari wateja wa Tigo wanafurahia unafuu na urahisi wa kutumia huduma bunifu za Tigo kama vile kufanya miamala ya Tigo Pesa (kutuma na kupokea pesa ikiwemo kutoka mitandao mingine na benki), kulipia huduma mbali mbali kama vile LUKU, kufanya manunuzi kutoka kwa wafanyabiashara tofauti, kukamilisha malipo ya Kiserikali na pia kufurahia huduma bora za maisha ya kidigitali kwenye mtandao mkubwa zaidi wa 4G nchini. 

Tuesday, April 24, 2018

Zantel yazindua Ofa babu kubwa ya mfungo wa Ramadhan

Meneja Uhusiano wa Zantel Rukia Mtingwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ofa maalum ya mfungo wa Ramadhani jijini Dar es salaam, Ofa hiyo mpya itawapa wateja uhuru zaidi wa kuwasiliana pamoja na kuwapa taarifa muhimu kipindi cha mfungo kama nukuu za Quran pamoja na jumbe za kuwakumbusha muda wa swala kufuturu na mwisho wa kula daku.

Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel April 23, 2020 imezindua ofa maalumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa wateja wake ili kuwawezesha kufanya mawasiliano kwa gharama nafuu pamoja na kupata taarifa mbalimbali zenye kujenga imani zao katika mwezi huu mtukufu.

Ofa hiyo inawapa wateja uhuru wa kuwasiliana zaidi pamoja na kupata taarifa muhimu kama vile nukuu mbalimbali za Koran takatifu pamoja na jumbe za kuwakumbusha muda wa swala na ujumbe wa sauti utakaoingia kwenye simu zao
kama simu nyakati za iftar na nyakati za daku.

Akizindua ofa hiyo mjini Zanzibar, Mkuu wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa alisema ofa hiyo itawasaidia waumini wa dini ya kiislamu kuimarisha zaidi mahusiano baina ya ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki cha mfungo.

“Zantel inapenda kuwatakia waislamu wote mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunatambua mwezi huu ni muda muafaka wa kujenga mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki hivyo ofa hii itahakikisha kwamba wateja
wetu wanawasiliana bila mipaka na pia kuwapa taarifa zitakazosaidia kujiimarisha kiimani ili kufanikisha funga zao,” alisema Mussa.

Naye, Meneja bidhaa na huduma wa Zantel, Aneth Muga alisema ofa hiyo itawazawadia wateja watakaojiunga na vifurushi vilivyoboreshwa zaidi vya siku,wiki na mwezi ambapo mbali na muda wa maongezi watajipatia nukuu za Koran takatifu pamoja na jumbe za kuwakumbusha muda wa swala tano.

“Tumeboresha zaidi vifurushi vyetu ili kuwapa wateja sababu zaidi za kuwasiliana msimu huu.Kwa wateja watakaojiunga kifurushi cha siku kwa Shilingi 1,000/- watajipatia dakika 150, SMS 100 pamoja na nukuu moja ya Koran, jumbe tano za kukumbusha muda wa swala,” alisema Muga.

Vilevile, kwa kifurushi cha wiki cha Shilingi 2,000 mteja atapata dakika 250, SMS 200 huku kifurushi cha mwezi cha Shilingi 10,000/- atapata dakika 1,250, SMS 500 pamoja na nukuu mbalimbali za maandiko ya Koran takataifu, jumbe za
kuwakumbusha muda wa kufuturu pamoja za kukumbusha muda wa swala. 

Ili kujiunga na ofa hii mteja wa Zantel apige *149*15# na kuchagua namba 1 ambayo ni Ramadhani ofa na atajiunga na kifurushi anachohitaji.

Kuhusu Zantel
Zantel ni Kampuni inyaoongoza kwa utoaji wa huduma za mawasiliano Visiwani Zanzibar kwa miaka mingi hivi sasa ikiongoza kwa ubora miundombinu ya mawasiliano, huduma pamoja na bidhaa.

Huduma ya kifedha ya Ezypesa ni ya kwanza nchini Tanzania kutoa huduma za kibenki za kawaida pamoja na za kiislamu kwa ushirikiano na benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Aidha, Zantel ni kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za intaneti nchini Tanzania kupitia uwekezaji kwenye teknolojia ya fibre optic cable ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki na duniani
umeiwezesha Kampuni hiyo kuleta mapinduzi ya haraka ya kidigitali hapa nchini.

Aidha,Miundombinu hiyo imeiwezesha Zantel kutoa huduma za kimataifa za sauti na data kwa jumla kwa kampuni nyingine na nchi jirani hivyo kuchagiza ukuaji wa teknolojia ya digitali

Kwa Mawasiliano zaidi kuhusu Zantel tembelea tovuti; www.zantel.co.tz
Rukia Mtingwa – Manager Brand and Communication 
Mobile: +255 774 55 9999





Sunday, April 22, 2018

QNET IMEWAPONGEZA CAF NA KLABU ZA MPIRA WA MIGUU ZA AFRIKA KWA MAFANIKIO YAO KATIKA MASHINDANO YA MPIRA YA CAF MWAKA 2018

                                                                                              
Kampuni inayoongoza ya mauzo ya moja kwa  moja QNET, na mbia katika ligi ya mabingwa ya CAF, Kombe la Shirikisho la CAF na kombe la Super Cup imewapongeza Shirikisho la Soka Afrika, CAF na vilabu vyote vinavyoshiriki katika mashindano yote ya klabu ya CAF mwaka 2019.

QNEt imekaribisha ushirikiano wake na CAF, katika mwaka 2018 na inaelezea fahari yake katika mpira wa miguu wa Afrika.

Ushirikiano kati ya kampuni ya QNET na CAF ni sehemu ya juhudi za QNET za kukuza michezo Afrika na dunia kote.
Kwa kweli, kama ilivyo katika michezo, QNET inaongozwa na ari ya kufanya kazi kwa pamoja kama timu pamoja na shauku wakati inapofanya biashara zake kila siku.

Ushirikiano huu ni fursa nyingine kwa QNET kuwa karibu na wawakilishi wake wa kujitegemea (IRs), walaji na wateja ambako QNET inaendesha shughuli zake tangu zaidi ya muongo mmoja iliopita.

Meneja Mkuu wa QNET wa Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara, Biram Fall amesema kwamba, “Mwaka uliopita ulikuwa ni mwaka mzuri kwa mpira wa miguu barani Afrika. Katika QNET tunaona fahari sana kujihusisha na CAF na ukuaji wa mchezo wa mpira wa miguu barani. Falsafa ya biashara yetu inashikilia mwenendo wa mpira wa miguu, ambao kimsingi ni ufanyaji wa kazi katika timu, ushirikiano, shauku na kufanyakazi kwa bidii. Tunawawezesha wajasiriamali katika bara zima la Afrika na tumejikita katika kusaidia wengi zaidi waweze kufanikiwa. Vilevile ni heshima kwetu kudhamini mashindano haya maarufu na yanayoheshimiwa sana, na tusingeweza kupata mshirika bora zaidi kuliko Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kuweza kufanikisha lengo hili. Mwaka 2019 unaonekana kutia matumaini zaidi na QNET itakuwa katika upande wa CAF kwaajili ya kuhakikisha utendaji bora zaidi”.

Katika mwaka 2019, QNET itakuwepo zaidi viwanjani ikiwa na uhamasishaji, matukio zaidi kwaajili ya kuhamasisha mashabiki kuongeza nguvu kazi ya mauzo ya QNET na wawakilishi wa kujitegemea (IRs).

QNET inaendelea kuongeza uwepo wake katika bara zima la Afrika, ikiwa inatoa fursa za ujasiriamali kwa watu na kusaidia watu kubadili historia zao vyema zaidi. Ukiachilia mbali ushirikiano wa kimichezo, QNET pia ni kampuni ambayo inajihusisha na majukumu ya kijamii, kutoa kwaajili ya maendeleo endelevu ya jamii katika kanda zote ambako inaendesha shughuli zake. Katika mwezi Novemba, kampuni ya QNET ilitunikiwa tuzo ya mwaka ya e-commerce CSD Company na Kituo cha Uwajibikaji kwa Jamii cha Afrika Magharibi (Centre for Corporate Social Responsibility West Africa)
   

WATAKA SHERIA YA WATIA MIMBA WANAFUNZI IONGEZWE MENO

Na: Amina Hezron,  Morogoro

Wito umetolewa kwa serikali kuhakikisha wanawadhibiti na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika wamebaka au kuwapa mimba wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari nchini.

Baadhi ya wadau wa Elimu Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mkutano huo.
 Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau wa elimu wilaya ya mvomero mkoani Morogoro wakati wa mkutano ulioandaliwa na mtandao wa elimu Tanzania TEN /MET ili kupeana mrejesho wa namna ya kukabiliana na changamoto za mimba za utotoni kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari.


Katika mkutano huo wa wadau  wamebaini ushiriki wa karibu wa wazazi na watoto wao haupo kwa kiasi kikubwa jambo linaloelekea kuendelea kuwepo kwa changamoto hiyo.


Kwa upande wake afisa elimu wa wilaya hiyo Bi. Maajabu Nkamyemka amesema kwa wilaya ya mvomero takwimu zinaonesha hadi April 6 mwaka huu takribani mimba 90 zimebainika kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambapo miongoni mwa hizo mimba 13 ni kutoka shule za msingi.

Aidha Bi. Nkamyemka amesema kuwa ni jukumu la wazazi na walimu kwa kushirikiana na wanafunzi kuhakikisha wanawafichua wale wote ambao ni wahusika bila kuwafumbia macho ili sekta husika kupambana nao ili kutokomeza janga hilo.

"kwa kuwa binti akipewa ujauzito huwa tunahangaika tu na aliyempa ujauzito, na yule mwenye ujauzito tunamuacha sasa bhas sasa kwa kuwa wazazi hawataki kuleta ushirikiano tutamfungulia kesi mwanafunzi mwenye mimba pamoja na wazazi ili wazaz wawachunge watoto wao ipasavyo "Alisema Nkamyemka.
Wadau hao wa elimu wakiwa ndani ya mkutano huo 
Naye mratibu elimu wa kata za mhonda na Kweuma bwn, Heriamini Mariki amesema kuwa kumekuwa na changamoto ya mimba hasa kwa wanafunzi, wa sekondari jambo ambalo kwa kiasi kikubwa wazazi ndiyo chanzo cha tatizo hilo huku akitaja sababu zinazochangia kuwa ni pamoja na uelewa finyu wa wazazi na wakati mwingine umaskini kwa baadhi ya kaya nyingi wilayani humo.

 “Sisi kama wadau wajibu wetu mkubwa ni kuwapatia elimu wazazi juu ya athari za kutokaa karibu na watoto wao na kuwa wawazi juu ya madhara ya kufanya ngono wakiwa na umri mdogo" alisema Mariki

Naye diwani wa kata ya mhonda Bw. Abdallah Hassani Khalifa ametoa rai kwa Serikali kujenga hosteli kwa shule za kata ili kuondokana na tatizo la mimba za utotoni linaloikumba nchi nzima kwa kiasi kikubwa, huku akiwataka wazazi na walimu wanawapa  watoto wanafunzi ushirikiano wa kutosha na ulinzi kwani ndiyo haki pekee wanaotakiwa kuzipata ili kufanya vyema katika masomo yao.


Saturday, April 21, 2018

#IdrisnaUber: Kampuni ya Uber imesaini mkataba na Msanii Idris Sultan kuwa Balozi wake nchini Tanzania mwaka 2018










Dar es Salaam, Tarehe 20 Aprili 2018.... Kampuni ya Uber imemtangaza msanii Idris Sultan kuwa balozi wake mpya nchini Tanzania mwaka 2018. Idris anakuwa msanii wa kwanza nchini Tanzania kuwa balozi wa Uber, programu ya usafiri yenye umaarufu mkubwa, nchini Tanzania.
Msanii huyu wa uchekeshaji, muigizaji wa tamthlia, na mtangazaji wa vipindi vya redio ametangazwa rasmi katika hafla ya kukata na shoka iliyokwenda kwa jina la #IdrisnaUber iliyohudhuriwa na wageni wachache na wanahabari wa humu inchini. Shughuli hiyo imefanyika katika mgahawa wa kifahari wa Akemi jijini Dar es Salaam.
Tangu mwanzoni mwa zoezi hili, tulifanya juhudi kubwa kuhakikisha kwamba tunampata balozi mwenye ufuasi mkubwa na atakayeiletea Uber ufanisi nchini Tanzania,amenukuliwa Bi.Elizabeth Njeri, Meneja wa Masoko wa Uber Kanda ya Afrika Mashariki. Idris Sultan ni mcheshi na ni msanii ambaye hafanyi mambo yake kwa mazoea, pia anaheshimika katika tasnia ya uchekeshaji,tamthlia, na utangazaji wa vipindi vya redio. Tuna imani kwamba Idris atailetea Uber tija kubwa kwa sababu ni mzalendo kweli kweli - yeye ni kielelezo cha Utanzania na anawasiliana na mashabiki wake kupitia mitandao ya jamii kila wakati. Hizi ndizo sifa tunazosistiza tunapotaka kuwa na mkataba na mabalozi wa kampuni yetu kwa sababu zinasaidia sana katika kuonesha kwamba tunajali maslahi ya wasafiri na madereva wanaotumia mfumo wetu nchini Tanzania.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Bw Alfred Msemo; Meneja Msimamizi wa Uber nchini Tanzania, alisema; “Kampuni ya Uber inajituma kutumia uwezo wake kupitia oparesheni zake kimataifa ili kuwa karibu na wateja wake humu nchini. Mchango wa Idris Sultan katika muziki wa Tanzania unaendana na dhamira yetu ya kujenga kampuni ya kimataifa inayogusa maisha ya madereva na wasafiri wanaotumia mfumo wetu hapa nchini. Tutaendelea kuwahudumia wasafiri wetu sambamba na kutoa fursa za ajira kwa madereva wanaotumia mfumo wetu.
Idris alifurahi sana alipotangazwa kuwa Balozi wa Uber nchini Tanzania; “Nimefurahi sana na ni heshima kubwa kwangu kupata fursa hii adimu ya kushirikiana na Uber,kwa sababu mimi nishabiki mkubwa wa mapinduzi yaliyoletwa katika sekta ya usafiri kupitia kwa mfumo wake kote duniani. Nimefurahi kuona jinsi Uber imepata umaarufu jijini Dar es Salaam, binafsi mara nyingi mimi hutumia usafiri wa uberX nikiwa na marafiki zangu kwenye mitoko yetu ya jioni na sasa wamaleta huduma nyingine ya bajaji; uberPOA ambayo nina hamu sana kuitumia - utaniona hivi karibuni. Uber inaendelea kubadilisha maisha ya maelfu ya madereva jijini Dar es Salaam sambamba na kuwapa wasafiri uhuru wa kuchagua usafiri wanaotaka. Nimefurahi sana kuwa sehemu ya kampuni ambayo inajituma kuleta mabadiliko chanya katika maisha yetu.
Baadaye kwenye hafla hiyo, Idris alipanda jukwaani na kuwatumbuiza mashabiki, wanahabari,na wafanyakazi wa Uber kwa kionjo cha kazi yake ya uchekeshaji. Msanii huyo na mshindi wa zamani wa shindano la Big Brother Africa alivunja mbavu za umati huo kwa vichekesho vyake.  
Tangazo hili linakuja siku chache tangu Uber ilipo tangaza kushirikiana na Tigo kwenye mpango
ambao wateja wa Tigo wanapata bando za bure wanapotumia programu ya Uber. Ushirikiano
huu wa kipekee nchini Tanzania umekuwa na manufaa makubwa kwa wasafiri na madereva
wanaotumia Uber na umechochea wasafiri na madereva zaidi kujiandikisha kutumia programu
ya Uber nchini Tanzania.

Thursday, April 19, 2018

Uber na Tigo zashirikina kama njia ya kuwafikia wateja wao vizuri

Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari akipeana mikono na Meneja Mkuu wa Uber Afrika Mashariki, Loic Amado mara baada ya kuingia makubaliano ya kipekee yatayowafaidisha watumiaji wa Tigo wakaotumia huduma za usafiri za  Uber kwa kutumia Uber App bure. Kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Uber Tanzania, Alfred Msemo na kushoto ni Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha wa Tigo, Hussein Sayed kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam.
uber
Ufanisi katika jambo lolote lenye tija na manufaa ni kitu muhimu sana na sasa huduma ya usafiri wa kukodi unaotolewa na Uber imefungua ukurasa mpya kwa kuamua kufanya kazi na Tigo Tanzania.
Usafiri wa kukodi, Uber umekuwa na umaarufu wake kwa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam na hivyo kuwa na mvuto kwa wengi hasa wale ambao hawapendi kupata shida ya kugombania usafiri au kufika sehemu ambayo mtu anakwenda bila nguo yake kuchafuka kwa vumbi/majasho.
Unaweza ukajiuliza nini ambacho kimewaleta Uber na Tigo katika meza moja na kuamua kufanya kazi kwa pamoja? Jibu ni rahisi sana, teknolojia lakini utauliza tena kivipi? Uber anamiliki programu tumishi na ili uweze kuita huduma ya usafiri wa Uber basi itakubidi uwe na kifurushi cha intaneti (MBs).

Watumiaji wote wa app ya Uber na wanaotumia laini ya Tigo hawatatozwa kiasi chochote cha kifurushi cha intaneti wanapokuwa wanatumia programu tumishi ya Uber.



Uber na Tigo
Uber ni moja ya huduma ya usafiri ambapo iwapo safari ya kwenda mahali imeanza na dereva hakuwasha kiyoyozi una haki ya kulalamika kwanini dereva hajawasha “Kileta upepo” ndani ya gari.


Uwezo wa kutumia app ya Uber bila kifurushi chako cha intaneti kutumika ni kwa wote, dereva pamoja na abiria anayetumia laini ya TIgo.

MAkubaliano baina ya Uber na Tigo Tanzania yanaangaziwa kama hatua mojawapo ya watu kuzidi kutumia programu tumishi ya Uber ili kuweza kupata huduma hiyo bila makato ya MBs (bure).

Ofa nyingine kutoka Tigo na Uber zipo mbioni kuja. Ulishawahi kutumia huduma ya usafiri wa Uber kabla na baada ya ofa hii kuwepo? Unazungumziaje makubaliano ya Tigo Tanzania na Uber?

FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY YABADILI NEMBO YAKE, NA HUU NDIO MUONEKANO WA NEMBO YAO MPYA

Baada ya zaidi ya muongo mmoja na nusu kufikia Azaki nchi nzima, Sasa Foundation for Civil Society (FCS) inajikita katika kuongeza ufanisi na juhudi za kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau wote katika kuleta maendeleo.

Baada ya uzinduzi huu ndio muonekano wa Nembo mpya ya Foundation for Civil Society (FCS).

Hayo yameelezwa mapema jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Bw. Francis Kiwanga wakati wa uzinduzi nembo mpya ya shirika hilo ambayo itaendana na mabadiliko na mfumo wake wa utendaji.

Alisema kuwa hii itahusisha kushirikiana na taasisi zote za Serikali, Bunge, Sekta binafsi, Asasi za kiraia (AZAKI) ili kufikia Maendeleo Endelevu ya Dunia pamoja na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa kuboresha maisha ya watanzania ifikapo 2025.

Aidha aliongeza kuwa kwa sasa FCS itatoa ruzuku kwa wastani wa Asasi 150 kwa pande zote mbili za muungano yaani Tanzania Bara na Visiwani kila mwaka, ambapo hapo awali ilikuwa ikitoa kwa Azaki zaidi ya 5500 zilizokuwa zikihudumia wananchi wa mikoa yote hapa nchini.

Alisisitiza kuwa kiasi cha ruzuku kitaongezeka na kwa sasa taasisi hiyo itatoa ruzuku zenye thamani ya billion 11. kwa mwaka na muda wa mkataba pia utakuwa mrefu hadi kufikia miaka miwili ili kupata matokeo mazuri kwa miradi itakayofadhiliwa na FCS.

Akieleza sababu ya kufanya hivyo alisema kuwa wamejikita katika eneo la utawala bora na maendeleo hivyo siyo rahisi kuboresha maeneo hayo kwa mkataba wa mwaka mmoja au miezi sita tu, Hivyo wameona kuna haja ya kuongeza mkataba na kiwango cha ruzuku katika kufanikisha hili.

Na mwisho kabisa alipenda watu wafahamu kuwa FCS ipo kwa ajili ya watanzania hivyo waondoe mila potofu ya kuwa ni chombo ambacho hakina ubia na serikali na kwa sasa watafanya mambo mengi mazuri kwa kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa Tanzania.


            Mazungumzo ya azaki yanaendelea kupitia hastag hizi.

                                        #AZAKITanzania  / #CivilSocietyTanzania 


Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis kiwanga akitoa maana ya kitu kimoja baaba ya kimoja katika nembo ya kwanza ya shirika hilo kabla ya kuzinduliwa kwa nembo mpya.


Zoezi la uzinduzi wa nembo mpya ya Foundation for Civil                                        Society likifanyika.

Baadhi ya washiriki kutoka AZAKI mbalimbali hapa nchini wakifuatilia matukio yanayoendelea katika Tafrija hiyo ya Uzinduzi wa nembo mpya ya FCS.

Baada ya Uzinduzi wa nembo mpya ya FCS kulifuatiwa na tukio lingine la uzinduzi wa tovuti mpya (Website) mpya ya shirika hilo kama inavyoonekana pichani.

Washiriki wa semina wakiendelea kusherehekea tafrija.

Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa shirika la Foundation For Civil Society. 

Wafanyakazi wa Foundation for Civil Society wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Tafrija hiyo, Ambao pia ni wana AZAKI wanaofanyanao kazi kupitia miladi mbalimbali wanayoiendesha.