Wednesday, June 29, 2022

IGP SIRRO ASKARI POLISI 156 WAMEFUKUZWA MAFUNZO

Leo Juni 29, 2022. Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema takribani askari Polisi wanafunzi 156 wamefukuzwa mafunzo ya kijeshi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo za utovu wa nidhamu na kufanya mambo ambayo hayakubaliki ndani ya shule ya Polisi.

-IGP Sirro amesema hayo wakati alipofanya ziara kwenye uwanja wa medani za kivita wilaya ya Siha, West Kilimanjaro katika Shule ya Polisi Tanzania, ambapo pia amewaelekeza wanafunzi hao wa kozi ya awali ya askari Polisi kufuata sheria, kanuni na taratibu za shule hiyo ikiwa pamoja na kudumisha nidhamu ndani ya Jeshi la Polisi.

Demetrius Njimbwi

Afisa Habari wa Jeshi la Polisi

 

Shirika la Posta Tanzania limesaini Mkataba wa kusafirisha Sampuli za Kibailojia na kampuni ya TUTUME.

Na. Vicent Macha Dsm

Shirika la posta nchini pamoja na Kampuni ya kusafirisha mizigo ya TUTUME wamepongezwa kwa ubunifu wa kushirikiana kuhakikisha watanzania hawakosi huduma muhimu za afya.

Pongezi hizo zimatolewa na Waziri wa Habari, Mawasialiano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Moses Nauye alipoalikwa kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa usafirishaji wa sampuli za kibaiolojia baina ya shirika hilo pamoja na kampuni hiyo.

Aidha amesema kuwa kama lilivyo lengo la serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan la kusogeza huduma mbalimbali karibu na wananchi hivyo mikataba hiyo itasaidia sana kupanua huduma hizo hasa katika upende wa Afya.

Ameongeza kuwa licha ya kuwa mkataba huo unalenga sekta lakini angalieni pia katika maeneo mengine ambayo mnaweza kushirikiana na mkiangalia wote mnafanya kazi ya aina moja hivyo mkiongeza mashirikiano katika vitu vingi mtaweza kuwasaidia watanzania kwa sehemu kubwa sana.

Amemalizia kwa kuwataka TUTUME, Shirika la Posta pamoja na wote wanaotoa huduma za kusafirisha bidhaa kuweza kuutumia vizuri mfumo wa anuwani za makazi ili kurahisisha ufanyaji wao wa kazi, na pia amewaomba Wizara ya Afya ikiwezekana kuwafuata watu majumbani kuchukua sampuli na kutuma kwa mashirika haya na baadae kuwarudishia pia majibu kupitia wasafirishaji hao hao.

kwa upande wake Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrice Mbodo amesema kuwa mkataba huo waliyosaini na Kampuni ya TUTUME ni wa kiuwakala wa kusambaza Sampuli mbalimbali za Mahabara

Ameongeza kuwa majukumu ya TUTUME, itakuwa ni kuchukua Sampuli kutoka katika ngazi ya kwanza ya Mahabara na kupeleka ngazi ya pili ya Mahabara na wao Shirika la Posta kazi yao itakuwa ni kutoa ngazi ya pili na kupeleka katika Mahabara za uchunguzi na baadae muhusika kupelekewa majibu yake.

Ameendelea kusisitiza kuwa Shirika la Posta limekuwa likitoa huduma za kusafirisha mizigo kwa njia mbili yaani njia ya haraka pamoja na kawaida, Na kuongeza kuwa mpaka sasa shirika hilo limetoa ajira ya uwakala kwa vijana wa boda boda zaidi ya 450.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Tutume, Misana Manyama amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi zinapohitaji kushirikiana na idara za Serikali ili kuweza kuleta maendeleo katika nchi yetu. 

Ameongeza kwa kusema kuwa waoa kama TUTUME, wataifanya kazi hiyo kwa uadilifu na weledi mkubwa sana, na kutii masharti yale yote yaliyopo kwenye mkataba huo na kwamba wao wanauzoefu wa kutosha katika kazi hiyo kwani walikwisha ifanya hapo nyuma na wanaendelea kuifanya na kuongeza kuwa mpaka sasa wanavijana wa boda boda zaidi ya 1450 nchi nzima.

HABARI PICHA.
Waziri wa Habari, Mawasialiano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Moses Nauye katika zoezi la kusaini mkataba kati ya shirika la Posta na Kampuni ya TUTUME.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonaz akitoa neno katika zoezi la uwekaji saini mkataba wa kusafirisha Sampuli za kibaiolojia.
Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrice Mbodo akiongea katika zoezi la kusaini mkataba kati ya shirika la Posta na Kampuni ya TUTUME.
Mkurugenzi wa Kampuni ya TUTUME, Misana Manyama akiongea namna watakavyoshirikiana na Shirika la Posta nchini kuweza kusafirisha sampuli za kibaiolojia.
Zoezi la utiaji wa saini likiendelea kati ya Shirika la Posta nchini na Kampuni ya TUTUME, zoezi lililofanyika mapema jana Mkoani Dar es salaam.






Saturday, June 25, 2022

Mpendekezo ya ACT - Wazalendo Kuhusiana na Ajali ya Treni iliyotokea Mkoani Tabora.

Juzi, Jumatano 21, 2022 tulitoa taarifa ya awali kupitia akaunti za mitanao ya kijamii ya Msemaji wa sekta ya Habari na Uchukuzi wa ACT Wazalendo Ndg. Ally Saleh kwa kutoa pole kwa wananchi waliopata ajali ya Treni iliyotokea siku hiyo katika eneo la Malolo Mkoani Tabora. 

Ajali hiyo ilihusisha treni iliyokuwa ikifanya safari kati ya Kigoma na Dar es Salaam na chanzo chake kikielezwa ni kuwa hitilafu za miundombinu ya reli kutokana na uchakavu. Treni iliyopata ajali iliondoka stesheni ya Kigoma saa mbili usiku Jumanne Juni 21, 2022 kuelekea Dar es Salaam ikiwa na behewa nane zilizobeba abiria 930.

ACT Wazalendo pamoja na mambo mengine kwenye suala hili tumeona Takwimu za waathirika wa ajali hii zimekuwa na mkanganyiko mkubwa kati ya taarifa kutoka Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Shirika la Reli, Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Wahudumu wa Hospitali ya Kitete. Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuwa ajali hiyo imesababisha vifo vya watu wanne (4) na majeruhi wapatao 205. 

Aidha, chanzo cha ajali hii haikijawekwa wazi na kutolewa maelezo ya kutosha na mapendekezo ya namna ya kukomesha tena kutokea kwa ajali kwa wakati mwingine. Tunafahamu umuhimu na mchango wa Usafiri wa reli nchini hususani kwenye Mikoa ambayo reli hii inahudumia kama vile Morogoro, Dodoma, Singida, Shinyinga, Mwanza na Kigoma kwa upande wa reli ya kati. 

Shirika la Reli, linasimamia Miundombinu ya Reli na uendeshaji mzima wa usafirishaji wa mizigo na watu kupitia usafiri huu, hivyo ilitarajiwa kuona shirika linashtushwa na kuguswa zaidi kutokea kwa ajali ambayo imeleta athari kubwa kwa wananchi kwa kutoa maelezo ya kutosha na hatua Madhubuti zitakazo rejesha Imani ya wananchi kuhusu usafiri huu.

Kinyume chake, Shirika la reli halijaipa uzito na kutoa hatua madhubuti za kushughulikia waathirika, kutoa taarifa za aendeleo yao, uchunguzi wa chanzo halisi cha ajali na kuimarisha kwa Miundombinu na nyenzo za usafiri wa reli. Kama tulivyotangulia kusema awali; taarifa yetu ya mwanzo ilikusudia kutoa pole, hivyo kutokana na taarifa ya sasa, 

ACT Wazalendo tunatoa mapendekezo yafuatayo ili kushughulikia waathirika na kuimarisha uendeshaji wa huduma ya reli nchini: 

i. Serikali isiwe inaficha takwimu halisi zinapotokea ajali kama hizi ili kuondoa mkanganyiko na kujulisha umma ukubwa wa ajali. 

ii. Serikali ilisimamie Shirika la Reli kuhakikisha kuongezeka kwa ubora wa huduma na usalama wa usafiri huo usioweza kukwepeka na wananchi wengi. 

iii. Abiria wote waliojeruhiwa wapatiwe matibabu bure kadri ambayo watayahitaji ili wapone kabisa na warudi katika kazi na maisha yao ya kawaida.

 iv. Serikali iandae utaratibu wa kutoa fidia kwa majeruhi watakao pata ulemavu wa kudumu na fidia kwa familia kwa wale waliopoteza maisha kutokana na ajali hii. 

v. Uchunguzi wa tukio hilo ufanywe kwa haraka na uweledi ili taarifa sahihi itolewe kwa umma. 

Imetolewa na; Ndugu Ally Saleh 

asaleh@actwazalendo.or.tz 

Msemaji wa Sekta ya Habari, Teknolojia ya Habari na Uchukuzi ACT Wazalendo

Friday, June 24, 2022

Mapendekezo Manne ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwenye Suala la Katiba Mpya.

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Wakili Anna Henga akitoa ufafanuzi wa jambo mapema leo mkoani Dar es salaam.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetangaza mapendekezo manne kufatia kauli ya chama cha Mapinduzi mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri kuu ya chama hicho  kuwa imeridhia kuanza kwa mchakato wa katiba mpya.

Akizungumza jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Wakili Anna Henga amesema kauli ya chama hicho kikongwe kuridhia kuanza kwa mchakato huo ni ya kupongezwa.

Alisema LHRC inapendekeza Serikali kuanza kwa kupeleke mswada wa katiba, mswada wa sheria, pamoja na rasimu ya pili ya Katiba pendekezwa (katiba ya Warioba) kisha ianze majadiliano na wananchi kupitia mikutano hata vyombo vya habari.

“Ikumbukwe kuwa 31 Disemba 2010 aliyekuwa Rais wa Awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza kuanza rasmi kwa mchakato wa Katiba katika kongamano la LHRC ambalo lilibeba kauli mbiu ya KATIBA MPYA NI WAJIBU” Alibainisha Wakili Henga.

Kwa upande wake Afisa programu wa LHRC bwana  Maduhu William aliongezea kuwa mchakato wa Katiba ni jumuishi hivyo kuna watu wa makundi mbalimbali basi uwe shirikishi kwa watu wote.

“Katiba ni zaidi ya Dola, ili mchakato uwe hai lazima uwe rafiki ushirikishe makundi yote wakiwemo walemavu, wazee, vijana, wanafunzi kwa kufanya hivyo mchakato utakuwa rafiki kwa makundi yote ” Alisema Bw. Maduhu 

Mh. Gondwe Afurahishwa na Tamasha la watoto wenye Mahitaji Maalumu lililoandaliwa na Kijiji cha Makumbusho.

Na. Vicent Macha Dsm.

Afisa elimu wa Wilaya ya Kinondoni amepewa siku saba za kuhakikisha Katika shule zote za msingi na sekondari zilizopo katika wilaya ya hiyo kuwepo na walimu walezi.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Godwine Gondwe akiangalia baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa na watoto wenye Mahitaji Maalum mapema leo Mkoani Dar es salaam.

Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa wilaya ya Kindondoni Mh. Godwine Gondwe katika Tamasha la Watoto wenye Mahitaji Maalum lililoandaliwa na Kijiji cha Makumbusho ya Taifa Mapema leo mkoani Dar es salaam.

Aidha Mh. Gondwe amesema kuwa ni muhimu sana kuwepo kwa walimu hao mashuleni kwani itasasaidia kuwagundua na kuwapa msaada wa karibu Watoto hao, kwa sababu wanafunzi wanatumia muda mwingi shuleni kuliko majumbani.

Ameendelea kukipongeza Kijiji cha makumbusho kwa kwa kuweza kuandaa tamasha hilo lililojumusha shule mbalimbali za Watoto wenye mahitaji maalum Pamoja na shule za kawaida ili kuwafanya Watoto wachangamane na waweze kucheza na kufurahi kwa Pamoja.

Ameongeza kuwa Watoto wenye ulemavu wanatakiwa,kutambuliwa, kuthaminiwa na kupatiwa haki zao za msingi ikiwemo elimu ili kuwafanya waweze kuishi katika maisha bora ,huku akikemea jamii kuacha  vitendo vya unyanyapaa kwa Watoto hao.

Katika Tamasha hilo lililobeba kauli mbiu isemayo "Haki Sawa Kwa Wote" limeweza kuwakutanisha wanafunzi kutoka shule za Msingi ikiwemo Mugabe, Uhuru Mchanganyiko, Mikocheni, Makumbusho na Shule ya msingi Jeshi la Wakovu.

Baadhi ya Watoto wenye Ulemavu wakicheza na kuburudika katika Tamasha la Watoto wenye Mahitaji Maalum lililoandaliwa na Kijiji cha Makubusho Mkoani Dar es salaam. 

Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Kijiji Cha Makumbusho Bi.Wilhelmina Joseph amesema kwamba Makumbusho ya Taifa itaendelea kuthamini makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo Watoto wenye mahitaji mbalimbali ili kuwafanya wapate haki zao za msingi.

"Tumeandaa tamasha hili ili kuthamini haki za Watoto hawa ,hivyo sisi Kama Makumbusho ya Taifa tumeandaa tamasha hili la Watoto wenye mahitaji Maalumu na tukaweka kauli mbiu ya Haki Sawa kwa Wote" ili kuifanya jamii itambue kuwa hata watu wenye ulemavu wana haki sawa na wengine hivyo wasiwafiche majumbani" amesema Bi Wilhelmina.

Wednesday, June 22, 2022

MAKAMU WA RAIS OTHMAN AZINDUA TAMASHA LA ZIFF2022

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), itatengeneza na kusimamia Sera ya Filamu itakayohakikisha kukua kwa utamaduni na kusaidia kuweka mazingira bora ya uwekezaji utakoimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na mataifa mengine.

Mheshimiwa Othman ameyasema hayo Usiku wa Juni 19, mwaka huu wakati wa Sherehe za Ufunguzi wa Tamasha la 25 la Filamu kwa Nchi za Jahazi (ZIFF) zinazoendelea kwa siku 9 katika viunga vya Ngome-Kongwe, Forodhani, Mjini Unguja.

Mhe.Othman amesema kuwa hiyo ni kutokana na uhalisia kwamba mwendelezo wa harakati za Tamasha la Filamu na Maonyesho ya shughuli mbali mbali za Utamaduni wa Asili wa Mzanzibari na Nchi za Jahazi, zinaitambulisha Zanzibar duniani na kwamba ni miongoni ma fursa muhimu za kuikuza Nchi kiuchumi.

Ambapo amesema matukio ya kitamaduni, kama vile Tamasha la ZIFF linaloendelea sasa nchini hapa, huwezesha ubadilishanaji wa moja kwa moja wa mawazo, mila, silka na maongezi kati ya jamii za watu tofauti, hasa kwa kuzingatia uzuri na upekee wa Visiwa vya Zanzibar tangu asili uliotokana na historia ndefu katika ulimwengu wa ustaarabu.

Mhe.Othman amebainisha kuwa Binaadamu daima hujisikia vyema anapoweza kutambulisha ustaarabu wake na wengine wakasifia na kuweza kujifunza kutoka kwake, ambapo hiyo ni katika siri za Tamasha la Utamauni wa Nchi za Jahazi.

"Katika kujifunza tunapata kubadilishana mawazo, ujuzi, ufahamu na elimu, vitu ambavyo ni muhimu kwa maendeleo ya binadamu na ni sehemu muhimu sana ya kuenzi na kutukuza utu wetu katika njia ya mshikamano na hivyo kuwa kielelezo cha haki, amani na ustawi wa kimataifa", amesisitiza Mheshimiwa Othman.

Aidha amesema kuwa filamu zinazungumza lugha moja; ni muhimu na zina maana sawa  kwa ulimwengu na watu wote, bila kujali asili zao za kitaifa, kitamaduni au kijamii ambapo pia ni njia moja maarufu ya sanaa za kisasa, zinazovunjavunja vizuizi baina ya watu, mataifa na tamaduni, huku zikisisitiza maadili, hisia na utashi ambao mwanadamu daima anapenda kuudhihirisha kupitia kubadilishana mawazo.

Katika nasaha zake Mheshimiwa Othman ametoa wito kwa wageni ambao ni kutoka ndani na nje ya Afrika, wakiwemo washiriki kutoka Oman,Falme za Kiarabu, na Umoja wa Ulaya, kutenga muda na kutembelea vivutio vya Zanzibar kwa ujumla, na kujionea urithi na utajiri wa utamaduni wa visiwa hivi,huku akisisitiza kwa kusema, "haya ni maendeleo ya kipekee ya Tanzania ya leo na ndipo tunapoona umuhimu wa kuwa na Tamasha la Kimataifa".

Aidha, akabainisha:
"Kupitia mahusiano haya wakaambukizana utamaduni na urithi wa dunia; ndiyo maana ni furaha kubwa kuona kwamba kwa kupitia Tamasha hili tunaendeleza nguzo hiyo moja muhimu ya utu na urithi wa binadamu", ameongeza Mheshimiwa Othman.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Bi Tabia Maulid Mwita amesema kuwa daima amekuwa akifahamisha tija ya ziada iliyopo katika ufanikishaji wa Tamasha la Filamu la ZIFF hapa visiwani, ikiwemo upeo mpya wa ubunifu baina ya watengeneza- filamu wa Tanzania, na kwamba ikitokea shaka yoyote dhidi ya mila na silka za asili, ni vyema watu wasisite kuibuka na kushauri ili kunusuru utamaduni uliojaa ustaarabu wa Kizanzibari. 

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Bw. Hassan Mitawi amesema kuwa filamu ni chombo muhimu cha kuelezea maisha na utamaduni wa watu na jamii yeyote inayohitaji maendeleo katika nyanja zote za maisha zikiwemo za uchumi. 

Akieleza mafanikio ya ZIFF kwa Kpindi cha Miaka 25 tangu kuasisiwa kwake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tamasha hilo hapa Visiwani, Profesa Martin Mhando amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, tasnia ya filamu ya Tanzania na Afrika kwa ujumla imestawi, ambapo filamu bora zaidi za Kiafrika na hata za Kitanzania zinaonekana katika orodha ya Tuzo za Kimataifa. 

Nae Mkurugenzi Mkuu a Tamasha hilo, Prof. Martin Mhando alibainisha kuwa, Watengeneza filamu wa Kitanzania kupitia Tamasha hilo, watapata fursa adhimu ya kutazama filamu kutoka nchi mbalimbali zilizochaguliwa vyema, zenye mandhari na mitindo mbalimbali, ili kujifunza zaidi. 

Aidha, alisema kuwa, Mwaka huu takribani filamu 3450 kutoka Nchi 33 ziliingia katika mchujo na hatimaye 101 zilipata kupita na kuoneshwa kupitia Tamasha hilo. 

Watu Mashuhuri na Viongozi mbali mbali wa Serikali na Asasi za Kiraia wamejumuika katika tukio hilo.

RC MAKALLA: WAKANDARASI WA TAKA, MAWAKALA NA WATUMISHI 19 JIJI LA DSM WATAKIWA KUREJESHA FEDHA BILIONI 10

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla.

Atoa siku 7 kupata maelezo ya kina kwa wote waliotajwa na taarifa ya ukaguzi maalum kuanzia juni 2020/ juni 2021

Fedha zote zirejeshwe ndani ya siku 60 kinyume chake Wote waliotajwa watakabidhiwa TAKUKURU.

Madiwani wamshukuru mkuu wa mkoa kwa maelekezo, wahaidi kuchukua hatua stahiki kwa wote wakiohusika

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa muda wa siku 60 kwa Wakandarasi wa taka, Wakala wa ukusanyaji mapato na Watumishi 19 wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam waliohusika kuchota zaidi ya Shilingi Bilioni 10 za Mapato kuhakikisha wanazirejesha fedha hizo na endapo watakaidi kutekeleza agizo Hilo watafikishwa Mahakamani.

RC Makalla maelekezo hayo wakati wa Kiako Cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ambapo pia ametoa muda wa siku Saba kwa Mkurugenzi wa Jiji, Mkaguzi wa ndani, msimamizi wa mfumo wa mapato na Mhasibu kutoa maelezo ya kimaandishi kueleza ni kwanini wameshindwa kudhibiti ubadhirifu wa fedha hizo.

Hatua hiyo imekuja Baada ya Ukaguzi maalumu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali CAG mwaka 2020/2021  kuonyesha kiasi Cha Shilingi Bilioni 10 zilikusanywa lakini hazionekani kwenye mfumo ambapo Wakala wamehusika na upotevu wa Bilioni 4.5 na Watumishi 19 wa Halmashauri kuhusika na upotevu wa Bilioni 5.4 na mpaka Sasa hakuna aliechukuliwa hatua licha ya CAG kuelekeza fedha hizo kurejeshwa.
Aidha RC Makalla ameagiza Baada ya wahusika hao kuhojiwa, Baraza la Madiwani liketi na kupitia upya kasoro zote zilizoonekana na kutoka na maazimio ya kuzitatua.

Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Mabaraza ya Madiwani  Halmashauri zote za Mkoa huo kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kujiridhisha kwa kina Kila taarifa wanazopitisha kwenye vikao Kama ni sahihi.

Hata hivyo RC Makalla pia ameelekeza Halmashauri hiyo kufanyia kazi hoja 18 zilizobaki Kati ya hoja 49 zizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali CAG na kuhakikisha hoja hizo zinafungwa na zisijirudie.

Monday, June 20, 2022

ACT Wazalendo yataka ukaguzi maalum, kufuatia hasara ya Bilion 208 TADB.

Tarehe 16 Juni 2022, ACT Wazalendo tulifanya uchambuzi wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23. Katika uchambuzi wetu miongoni mwa mambo tuliyoyabainisha ni kutaka uwajibikaji kutokana na hasara iliyopatikana kwenye Sakata la korosho mwaka 2018. 

Hoja yetu ilitokana na Taarifa ya Uchumi wa Taifa 2021 iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Nchemba, iliyosema kuwa Serikali imelibeba deni hili la TADB lenye thamani ya shilingi bilioni 208 ambazo zilikopwa kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB), kwa kuligeuza kuwa mtaji wa TADB (coversion). 

Jumamosi tarehe 18, Juni 2022 Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kupitia mitandao ya kijamii na tovuti yake, ilikanusha kuwa hakuna hasara yoyote iliyopata kutokana na sakata la korosho kwa kuwa fedha zilizokopwa zilikuwa na lengo la kukuza mtaji wa benki hiyo na siyo kununua korosho. 

ACT Wazalendo bado tunataka uwajibikaji katika suala hili na tunamshauri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) afanye ukaguzi maalum wa ushiriki wa TADB katika kununua Korosho mwaka 2018/19 na matumizi ya mkopo huu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). 

Imetolewa na: Ndugu Juma Kombo

jkombo@actwazalendo.or.tz 

Naibu wa Sekta ya Fedha na Uchumi - ACT Wazalendo 

20.06. 022.

Sunday, June 19, 2022

Efm kuzindua kipindi kipya kiitwacho "Jioni ya Leo"

Vipindi vingi vya redio vinavyoanza majira ya jioni kuanzia saa 10 havifanyi vizuri kama inavyotakiwa na hii nimeiona katika utafiti wangu na kuamua kuja na kipindi kitakachokonga nyoyo za mashabiki wetu hapa nchini Tanzania.

Hayo yameelezwa mapema jana mkoani Dar es salaam na Mkuu wa vipindi kutoka kituo cha Efm Redio Bw. Dickson Ponera wakati wa uzinduzi wa kipindi kipya kiitwacho "Jioni ya Leo" kitakachorushwa na Redio hiyo.

Aidha ameongeza kuwa kipindi hicho kitakuja kuleta mapinduzi makubwa sana kwani kitakuwa kimesheheni mambo mengi mazuri na kuunganisha watangazaji kutoka katika vipindi tofauti vya Efm, akiwemo Dina Marious aliyetoka katika kipindi cha uhondo, Osca Osca sports HQ, Mpoki na Roman Shirika kutoka kipindi cha ubaoni.

Ameendelea kusema kusema kuwa Kipindi hichi cha "Jioni ya Leo" kitakuwa siki za katikati ya wiki na kitaanza saa 10 mpaka saa 1 kamili usiku na kuchukua nafasi ya kipindi cha Ubaoni ambaho ndio kilikuwa kikianza na kumalizika muda huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Efm Bw. Dennis Busolwa (Sebo) akiongea na waandishi wa habari katika Tafrija fupi ya kutambulisha kipindi kipya cha "Jioni ya leo" kilichozinduliwa makao Makuu ya Media hiyo Mkoani Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Vipindi Efm Dickson Ponera (Dizzo ONE) akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na kituo cha Radio cha Efm mapema jana mkoani Dar es salaam.
Mtangazaji wa Muda mrefu Dina Marios Akiongea na waandishi wa habari katika hafra fupi ya kutambulisha kipindi kipya cha "Jioni ya leo" kilichozinduliwa jana makao makuu ya Efm Redio Mbezi Beach mkoani Dar es salaam.
Tafrija ikiendelea.
Baadhi ya Viongozi na Watangazaji wa Efm wakishangaa bango la kipindi kipya cha "Jioni ya leo" baada ya uzinduzi mapema jana Mkoani Dar es salaam.




Saturday, June 18, 2022

Tamko la Global Peace Foundation kwenye siku ya Mtoto wa Afrika.

Mkurugenzi mkaazi, wa Global peace Foundation Tanzania Bi. Martha Nghambi.

Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Juni 16

Global Peace Foundation Tanzania (GPF), ni asasi ya Kiraia inayofanya kazi ya kuelimisha jamii na kujenga uwezo kwa makundi mbalimbali ya kijamii juu ya umuhimu wa kulinda Amani nchi Tanzania, ikiwa imejikita zaidi katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania  hasa ile iliyopakana na nchi jirani. Pamoja na hayo, Taasisi inafanya kazi katika eneo la kujenga uwezo kuhusu haki na usawa wa Kijinsia katika nyanja zote.
Kila mwaka tarehe 16 Juni Tanzania inaungana na Nchi zingine za Afrika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.

Chimbuko la Maadhimisho haya ni Azimio lililopitishwa na uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) mwaka 1990 kwa lengo la kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini waliouawa tarehe 16 Juni, 1976 kutokana na ubaguzi wa rangi.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Maendeleo Endelevu 2030: Imarisha Ulinzi na Fursa Sawa kwa Watoto” Kauli mbiu hii inawataka wazazi, walezi, Serikali na wadau wengine kuzingatia wajibu wetu katika kuimarisha mifumo ya ulinzi na maendeleo ya Mtoto ili aweze kudhibiti changamoto ya ongezeko la vitendo vya ukatili nchini pamoja na kutoa haki sawa kwa watoto wote bila ubaguzi wa aina yoyote.

Sisi Global Peace Foundation, mwaka huu tunaikumbusha jamii kuhakikisha inawalinda watoto dhidi ya vitendo vya Ukatili wa Kijinsia na unyanyasaji ambao unaweza kupelekea kuathirika kisaikolojia na kujiingiza kwenye migogoro ya kifamilia au makundi hatarishi.
Kukosekana kwa ulinzi na usalama kwa watoto wadogo katika ngazi ya familia, kunawaweka katika mazingira hatarishi ya kujiingiza kwenye makundi yanayochochea vurugu na chuki na kuongezeka kwa watoto wa mitaani. 

Tunaisisitiza jamii ya watanzania wote, kushirikiana na Mamlaka za serikali za Mitaa katika kuweka mikakati ya kuwalinda watoto wote, kusaidia kuwaondoa watoto walioko katika mazingira hatarishi na kuwaweka mahali salama ili kuwa na vijana wa baadaye watakao kuwa wazazi bora na wenye hulka ya kulinda na kuijenga Amani ya taifa letu. 
GPF tunasisitiza, kuwekwa kwa mikakati dhabiti ya kisera, ikiwa ni pamoja na kuimarisha Kamati za Ulinzi wa mama na mtoto ngazi ya Kijiji, Mitaa na Kata ili kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia. 

Aidha Tunaendelea kuishauri serikali kuharakisha maandalizi ya Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na watoto wa Pili (NPA-VAWC II) ili kuboresha zaidi Mikakati ya kukabiliana na changamoto  za Ukatili kwa watoto. Watoto wasipofanyiwa ukatili wa Kijinsia tutakuwa na jamii yenye Amani na inayojali Amani. 

Imetolewa na 

Martha Nghambi
Mkurugenzi Mkaazi
Tanzania
June 15,2020

Haya hapa Mapungufu yaliyopo katika Bajeti kuu ya 2022/2023 uchambuzi uliyofanywa na LHRC.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)  Wakili Anna Henga.

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeainisha mapungufu matatu katika Bajeti ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 iliyowasilishwa hivi karibuni bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba.

Mapungufu hayo yameainishwa leo Juni 17, 2022 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Wakili Anna Henga wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uchambuzi wa makadirio ya mapendekezo ya Bajeti hiyo kwa mtazamo wa haki za binadamu.

Ametaja mapungufu hayo kuwa yanagusa maeneo ya matumaini ya Watanzania kuhusu Bima ya Afya kwa wote, Jinsia na Bajeti ya Taifa ya mwaka 2022/2023 na Ada mpya za ving'amuzi.

Akitolea ufafanuzi kuhusu matumaini ya Watanzania kuhusu Bima ya Afya kwa wote, Wakili Henga amesema kwamba baada ya kilio cha muda mrefu cha Watanzania wa kipato cha chini kukosa huduma za Afya kutokana kutokuwa kwenye mfumo wa Bima,

Kwamba mjadala umeibuka katika miaka ya hivi karibuni juu ya umuhimu wa Bima ya Afya kwa watu wote.

“Mara kadhaa watenaji wa Serikali na Viongozi wamesikika wakieleza juu ya umuhimu wa mpango wa Bima ya Afya kwa wote. LHRC imeshangazwa na ukimya wa Bajeti ya mwaka 2022/2023 kuhusu suala ya Bima ya Afya kwa wote,” amesema Wakili Henga.

Hivyo, LHRC inapendekeza kwa Serikali na Bunge kuzingatia hitaji la kutenga Bajeti kwa ajili ya Bima ya Afya kwa wote.

Kuhusu Jinsia na Bajeti ya Taifa ya mwaka 2022/2023, Wakili Henga amesema kwa watetezi wa haki za binadamu na usawa kijinsia, bajeti ya mwaka 2022/2023 imekuwa na mapungufu kadhaa ya kijinsia.

“Kwa mfano, ingawa Waziri wa Fedha na Mipango amesifu Wanawake kwa kiwango kizuri cha urejeshaji wa mikopo, imekuwa mshangao kuwa bajeti inapendekeza kushushwa kwa asilimia ya mikopo ya Wanawake kupitia Halmashauri kutoka asilimia 4 hadi 2,” amesema Wakili Henga na kuongeza kwamba,

“LHRC inapendekeza kwa Serikali na Bunge kurudisha kiwango cha awali,”.

Pia, amesema baadhi ya bidhaa zitumiwazo na Wanawake ikiwemo nywele za bandia zimeongezwa ushuru wa forodha kutoka asilimia 25 mpaka 35 kwa madai ya kuendana na makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwamba mbaya zaidi kwenye taulo za za watotozi (Baby diapers) ambazo ni msaada mkubwa katika malezi ya watoto zinazoagizwa toka nje zimepandishiwa ushuru wa forodha kutoka asilimia 25 hadi 35.

“LHRC inaona kuwa hii sio haki kwa watoto na Wanawake ikizingatiwa kuwa uzalishaji wa ndani ya nchi haukidhi mahitaji kamili na kwamba ubora wake bado ni changamoto. Kijinsia, kupanda kwa ushuru wa forodha kwa taulo za watoto kunahatarisha Afya ya ngozi ya mtoto,” ameongeza Wakili Henga.

Kwa upande wa ada mpya za ving’amuzi, Wakili Henga ameeleza kwamba Wakati Watanzania wakitafakari kuhusu tozo kadhaa ambazo tayari zimepandishwa na mfumo wa kodi nchini, bajeti ya mwaka 2022/2023 inapendekeza kuanzishwa ada mpya ya matumizi ya ving’amuzi ambayo itakuwa ni Kati ya shilingi 1,000 hadi 3,000 kulingana na kiwango cha matumizi.

Wakili Henga amesema, maoni ya LHRC ni kwamba ada hii mpya ni mzigo wa ziada kwa watumiaji wa huduma ya ving’amuzi kwamba Haki hiyo inaweza kukwamisha juhudi za Serikali kuongeza kiwango cha upashanaji habari nchini kinyume na ibara ya 18 ya katiba.

Hivyo LHRC imependekeza kuiondoa kodi hiyo kwa kuwa itaongeza gharama za vufurushi na kuongeza mzigo kwa wananchi na kupelekea kuminya haki ya kupata taarifa.

Friday, June 3, 2022

"Jeshi la Polisi Latakiwa kuzingatia utawala wa sheria" Tume ya haki za Binadamu.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini imelitaka Jeshi la Polisi Nchini kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za jeshi ilo ili kuepuka vitendo vya uvunjifu wa haki za Binadamu.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu, Mathew Mwaimu wakati akitoa taarifa ya Tathmini kuhusu mwenendo na utendakazi wa Jeshi ilo nchini kwaanzia mwaka 2020 hadi 2022.

Mwaimu amesema tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora ilifanya uchunguzi kumi ikiwemo kutembelea vituo vya polisi katika baadhi ya mikoa nchini na kubaini kupigwa na kuteswa kwa watuhumiwa wakati Ukamataji au wakati wa upelelezi,kuwepo tuhuma za Rushwa dhidi ya baadhi ya Askari.

Pia Jaji Mwaimu amesema tume hiyo imebaini baadhi ya Askari polisi kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu vitendo wanavyolalamikiwa na wananchi pamoja na watuhumiwa kuwekwa mahabusu za polisi muda mrefu bila dhamana.

Aidha,Jaji Mwaimu amelitaka jeshi la polisi kuzingatia sheria ya Jeshi la polisi na huduma saidizi sura ya 322,sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai sura 20 na kanuni za jeshi la polisi za mwaka 2013 ambazo zimeainisha kazi za jeshi ilo