Showing posts with label AFYA. Show all posts
Showing posts with label AFYA. Show all posts

Thursday, March 15, 2018

"TAFITI ZINAONYESHA WANAUME WENGI WANA MATATIZO YA NGUVU ZA KIUME" NAIBU WAZIRI WA AFYA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo, jamii, jinsia na Watoto, Dk Faustine Ndugulile amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Afya akishirikiana na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), kufanya utafiti wa afya ya uzazi kwa wanaume ili kubaini sababu za tatizo hilo na kujua ongezeko la upungufu wa nguvu za kiume ni kubwa kiasi gani nchini.
Picha inayohusiana

Ndugulile amefikia uamuzi huo kwani mara zote Serikali imekuwa ikitilia mkazo afya ya uzazi kwa mwanamke na kusahau upande wa pili.

Amesema kwa upande wa Tanzania mpaka sasa hakuna tafiti zozote zilizofanyika juu ya tatizo hilo kwa wanaume, hivyo ni wakati wake sasa kulifanyia uchunguzi wa kina na kubaini suluhusho lake.

Aidha kwa tafiti zilizofanywa kisayansi duniani zimebaininsha kuwa wanaume wengi wana matatizo ya nguvu za kiume sababu kubwa ikiwa ni mtindo wa maisha, kwani wengi wao hupendelea kula vyakula ambavyo si bora vyenye mafuta na sukari kwa wingi ambavyo kwa kiasi kikubwa huchangia magonjwa yasiyoambukizwa na ukosefu wa nguvu za kiume.

Pia tafiti hizo zimeonesha kwamba matumizi ya vilevi ikiwemo pombe na sigara, kutofanya mazoezi mara kwa mara, unene kupita kiasi, msongo wa mawazo, matumizi ya dawa kwa muda mrefu, magonjwa sugu kama kisukari na presha kwa kiasi kikubwa huchangia tatizo hilo.

Katika harakati za kupambana na tatizo hilo Serikali juzi imepitisha baadhi ya dawa za tiba asili kutibu tatizo hilo ambazo zimethibitishwa na Mkemia Mkuu na kuruhusiwa kutumika kukabiliana na tatizo hilo dawa hiyo ni Ujana, huku dawa nyingine ambazo zimesajiliwa na zinafaa kutumiwa ni Sildenafil na Tadalafil.

Dawa hizo zimechunguzwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na kuthibitishwa kuwa hazina sumu wala madhara kwa watumiaji na zinapatikana katika maduka mbalimbali ya dawa

Monday, February 5, 2018

HUBERT KAIRUKI KUJENGA KITUO KUSAIDIA WENYE MATATIZO YA UJAUZITO

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Professa Charles Mgone akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano iliohusu maadhimisho ya Kumbukizi ya muasisi na Mmiliki wa Shirika la Elimu Kairuki (KHEN), Chuo Kikuu cha Kumbukumbuku ya Hubert Kairuki (HKMU), Hospitali ya Kairuki (KH) na Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN). 

Mkutano huo umefanyika Dar es Salaam leo Februari 4, 2018. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo HKMU (Taaluma), Prof. Ntabaye Moshi na Mkurugenzi wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Assey Mchomvu. 


Na Cathbert Kajuna- Kajunason/MMG.

Katika kuadhimisha miaka 19 ya kumbukizi ya Marehemu Profesa Hubert Kairuki, Shirika la afya na elimu la Kairuki limejipanga kujenga kituo cha kusaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida. 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Professa Charles Mgone amesema kuwa maadhimisho hayo yaliyoanza tokea Februari 1-6, 2018 jambo kubwa wamejipanga kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kusaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida huko Bunju jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Ali Hapi.

 "Kumekuwa na matatizo hasa ya ukosefu wa vituo vya kuwasaidia watu wenye matatizo ya uzazi jambo linalotupa msukumo wa kuanza ujenzi huu, kwa sasa tupo katika hatua za mwisho tupate kibali tuanza ujenzi maana sisi tumeshajipanga na tumeshazalisha wataalamu wa kutosha," alisema Prof. Mgone. 

Professa Mgone amesema kukamilika kwa kituo hicho kitakuwa msaada mkubwa maana mpaka sasa hospitali ya Hubert Kairuki imekuwa chachu katika utoaji wa huduma ya afya ambapo kwa siku wanapokea zaidi ya wagonjwa 700. 

Aliongeza kuwa mbali na ujenzi wa kituo hicho wanatarajia kuanzisha kliniki ya mama, baba na mtoto huko Bunju ili kuendeleza kuokoa vifo vya akinamama na watoto hasa waliombali na huduma. 

Jambo lingine ambalo wanalifanya katika maadhimisho hayo ni kutoa huduma za afya bure kwa kipindi cha kuanzia Februari 1-6, 2018  kwenye Hospitali ya Kairuki, pia wanajitolea damu kwa hiari ili kuokoa vifo vitokanavyo na ukosefu wa damu. 

Vile vile wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki watashiriki katika shindano la kujipima ujuzi juu ya mambo mbalimbali katika taaluma ya afya, maswali ya ufahamu kuhusu Tanzania, maisha ya mhasisi Marehemu Prof. Kairuki, Jiografia na jamii kiujumla. 

Mwisho wa kilele cha maadhimisho hayo kutafanyika mhadhara wa kitaaluma utakaoendeshwa na Professa Malise Kaisi juu ya mada 'Maono ya Prof. Hubert Kairuki yanayodumu': Umuhimu wake katika utoaji wa huduma za afya barani Afrika. 

Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN) limasimamia Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Hospitali ya Kairuki (KH) na Shule ya Uuguzi Kairuki (KSN) ambapo muasisi wake ni marehemu Hubert Clement Mwombeki Kairuki aliyezaliwa Juni 24, 1940 Bukoba mkoani Kagera. Mnamo Machi 17, 1987 muasisi huyo alianzisha hospitali ya TAG Mikocheni na mwaka 1992 aliibadilisha jina na kuitwa Mission Mikocheni hospitali ambayo kwa sasa inaitwa Kairuki Hospitali. 

Mwaka 1997, Prof. Kairuki alianzisha Mikocheni International University na baadae miaka 2 kupita alifariki dunia Februari 6, 1999 na chuo kikabadilishwa kuwa Hubert Kairuki Memorial Univesity. 

Wakati hospitali inaanzishwa ilikuwa walikuwa na uwezo wa kupokea wagonjwa wa nje 200 na wagonjwa wa ndani 30 kwa siku na kwasasa hospitali inauwezo wa kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje 700 kwa siku na wagonjwa 150 wa ndani ambapo wakati muasisi anafariki chuo kilikuwa na wanafunzi 30 katika fani ya udaktari na uuguzi kwasasa chuo kinatakribani wanafunzi 1509.

Saturday, January 20, 2018

UGONJWA MPYA WAIBAINIKA KENYA, WATANZANIA WAJIANDAE SOMA HAPA KUJUA

Tokeo la picha la UMMY MWALIMUSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa homa ya Chikuganya ambao umeripotiwa na vyombo vya habari kutokea jijini Mombasa nchini Kenya.

Taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu imesema kuwa mpaka sasa Shirika la Afya Duniani (WHO) bado haijatoa taarifa rasmi lakini wao wanaotoa taadhari kuzingatia muingiliano mkubwa wa watu baina ya nchini hizi mbili Kenya na Tanzania. 

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya wanasema kuwa ugonjwa wa Chikunganya unasababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa mbu wa aina ya Aedes na kusema ugonjwa huu si mgeni nchini Tanzania kwani ulishawahi kutokea. 

Friday, December 29, 2017

ARUSHA WAIOMBA KAMPUNI YA ABACUS PHARMA (A) LTD KUWAPELEKEA BIDHAA ZA SUGAR FREE

Muonekano wa jiji la Arusha katika picha

Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wa jijini Arusha wameiomba Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD kuwapelekea bidhaa za Sugar Free ambazo zinasaidia kupunguza  matumizi makubwa ya sukari.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyekuwepo mkoani humo kusherehekea Sikukuu ya Krisimasi walisema bidhaa hizo ni mkombozi kwao.

"Binafsi napenda kusema bidhaa hizi za Sugar Free kwa hapa Arusha zitapata soko kubwa kutokana na watu wengi kuathiriwa na ugonjwa wa kisukari" alisema Mzee Mollel mkazi wa Njiro.

Mollel alisema watu wengi jijini humo wananchi kwa masharti ya ulaji na unywaji wa vitu visivyo na sukari jambo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa karibu familia nyingi.

Alisema wakazi wa jiji hilo wamezipokea kwa mikono miwili bidhaa hizo ambapo wameiomba kampuni hizo kufungua tawi mjini humo ili bidhaa hizo ziweze kupatika wakati wote.

"Tunaomba bidhaa hizi ziuzwe na maofisa mauzo wa kampuni hiyo wasiwape wenye maduka itakuwa changamoto kupata maelezo ya kina ya matumizi yake na tunahofu wakiachiwa wafanyabiashara wengine wanaweza kutupandishia bei" alisema mkazi mwingine wa jiji hilo aliyejitambulisha kwa jina la Laizer.

Laizer alisema humo kumekuwa na unywaji na ulaji wa vyakula vyenye sukari lakini kuingia kwa bidhaa hizo zitasaidia sana wananchi hasa baada ya kupata maelekezo ya utumiaji wake.

Akizungumza bidhaa hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu alisema bidhaa hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi makubwa ya sukari katika vyakula. 

Alisema bidhaa hizo zimetengenezwa mahususi ili kukabiliana na ongezeko la sukari mwilini na hivi sasa zinapatikana kwa bei ya chini katika soko la nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi na kuwa bei hizo zipo kuanzia shilingi,4200, 4,500, 5,700, 8,850 na za bei ya juu ni shilingi 13,000 na kuwa zinategemea bidhaa husika.

"Bidhaa hizi zipo za aina mbili za sugar free gold  ambazo hutumika katika chai, uji, na vinywaji baridi tu  na sugar free natura hutumika katika baking, kupikia vyakula vinavyohitaji sukari katika upishi na pia hutumika katika chai, uji na vinywaji baridi na matumizi yake ni rahisi sana," alisema Babu.

Alisema kwa Tanzania bidhaa hizo zimeanza kuchukua soko kubwa baada ya wananchi kuona umuhimu wake na hivyo wanategemea muitikio utaendelea kuwa mkubwa.

Aliongeza kuwa, lengo kubwa la kampuni hiyo kusambaza bidhaa hizo ni kusaidia jamii kuelewa matumizi ya bidhaa hizo ambazo hazina sukari ingawa zina ladha ya sukari kama ile ya kawaida  na kwamba bidhaa hizo zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa hizo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga alisema ugonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa kwani Tanzania ni nchi ya tano Barani Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi.

Alisema hali hiyo inatokana na watu wengi hasa vijijini kutojijua mapema kama wameathiriwa na ugonjwa huo ambapo baadhi yao huanza kugundua baada ya kupata upofu, kukatwa miguu na kadhalika. 

Aliongeza kuwa, matibabu ya mgonjwa mmoja wa kisukari yanafikia asilimia 25 ya pato la familia fedha ambazo ni nyingi jambo linalowafanya wauguzaji kukata tamaa ya kumtibu mgonjwa na kuamua fedha hizo kuzielekeza katika matumizi mengine.

Dk.Chiwanga alitoa mwito kwa kusema ni vizuri kuzuia kupata kisukari kuliko kutibu.

Akizungumzia bidhaa za sugar free alisema hazitibu ugonjwa wa kisukari isipo kuwa zinamsaidia mgonjwa au mtu mwenye kisukari anapokula vyakula vingine visivyo na sukari kupata radha ile ile.

Alisema mtu mwenye ugonjwa wa kisukari hatakiwi kabisa kuvuta sigara ingawa vitu vingine kama vinywaji na pombe anatakiwa kutumia kwa uangalifu.

Sunday, December 3, 2017

ZIJUE DALILI NA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HATARI WA MATENDE

Ugonjwa wa matende ni aina ya ugonjwa unaosababisha ngozi na tishu zilizo chini ya ngozi ya mwanadamu kuwa nene(thickening of skin and underlying tissue).
Image result for ugonjwa wa matende
Ugonjwa huu huathiri miguu, mikono, figo, korodani na kusababisha
korodani kuvimba na kuwa kubwa sana.

Inakisiwa watu milioni 120 duniani wana maambukizi ya ugonjwa huu ambapo kati yao milioni 40 wamepata madhara makubwa kutokana na ugonjwa huu.

Kati ya hawa walioathirika theluthi moja huapatikana katika bara la Afrika, theluthi moja nyingine hupatikana India na kiwango kilichobakia hupatikana katika visiwa vya Pacific, Marekani na Asia ya kusini.

Ugonjwa wa matende husababishwa na vimelea aina ya minyoo (parasitic worm) vinajulikana kama Wuchereria bancrofti, Brugia malayi, B. timori ambavyo huenezwa na mbu jike aina ya culex quinquefasciatus mosquitoes na jamii fulani ya mbu dume(Anopheles species) wakati minyoo aina ya Brugia roundworms huenezwa mbu wanaojulikana kama Mansonia mosquitoes.

Mbu hawa hueneza ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa
mwengine.
Aina nyingine ya ugonjwa wa matende inayojulikana kama nonparasitic
elephantiasis au podoconiosis ambayo haisababishwi na vimelea vyovyote
hupatikana katika nchi za Afrika Mashariki (Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi) Sudan, Egypt na Ethiopia.

Asilimia 6 ya maambukizi ya aina hii ya podoconiosis hupatikana nchini Ethiopia.

 
Nini hutokea baada ya maambukizi?Kwa kawaida mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu huwa na mabuu (larvae)
kwenye mfumo wa damu mwilini mwake wanaojulikana kama microfilariae.

Mabuu haya husafiri kutoka kwenye mfumo wa damu hadi kwenye mfumo mwingine unaojulikana kama mfumo wa limfu (lymphatic system) na kukua kuwa minyoo kamili (adult worms) ambayo huziba mfumo huu wa limfu ambao unategemewa sana katika kuweka uwiano sawa wa maji (fluid balance) kati ya mfumo wa damu na tishu ndani ya mwili na husaidia kuupa mwili kinga dhidhi ya magonjwa mbalimbali.

Minyoo hii huishi kwa miaka minne hadi sita na katika uhai wake huzaa mamilioni ya mabuu (microfilariae) mengine wakati ikiwa kwenye mfumo wa damu.

 
Mbu huenezaje ugonjwa huu?
Mtu ambaye ameambukizwa ugonjwa huu huwa na mabuu kwenye mfumo wake wa damu na anapongatwa na mbu ambawo wanauwezo wa kuchukua mabuu haya ambayo huendelea kukua na kufikia hatua
ya kuambukiza mtu mwingine ndani ya mwili wa mbu.

Kwa kawaida, ukuaji huu wa mabuu ndani ya mwili wa mbu huchukua wiki moja hadi tatu na baada ya kukua na kufikia hatua ya kuambukiza mtu
mwingine, mabuu haya husogea mpaka kwenye sehemu ya mdomo wa mbu ambayo ndio huwa humng'ata mtu wakati mbu anapofyonza damu kutoka kwa mtu.

Mbu mweye mabuu kwenye mdomo wake anapomngata mtu ili kufyonza damu, ndipo mabuu haya yanapoingia kwenye mwili wa mtu na hivyo kusababisha maambukizi ya ugonjwa huu.

 
Dalili za ugonjwa huu ni zipi?
• Dalili kubwa ya ugonjwa huu ni kuvimba sehemu ya chini ya mwili yaani kwenye miguu na vidole.

Pia mtu anaweza kuvimba sehemu ya mikono au mkono wote
pamoja na vidole vya mkononi. Wengine
huvimba kwenye korodani (wanaume).

• Kuhisi uzito na kukamaa kwa mikono au miguu kutokana na uvimbe             uliopo.

• Kutoweza kutumia kiungo husika kilichovimba.

• Maumivu au kutohisi vizuri kwenye mikono au miguu.

• Kupata maambukizi ya mara kwa mara kwenye sehemu iliyovimba.

• Ngozi kuwa nene na ngumu kwenye mikono au miguu.
 
 Dalili nyingine ni pamoja na;
- Homa
- Maumivu ya kichwa
- Maumivu kwenye jointi na mifupa
- Kutapika

- Vidonda kwenye mikono au miguu
- Mistari ya rangi nyekundu inayoonekana kwenye mikono au miguu (red       streaks)

 
Vipimo vya uchunguzi
• Blood examination under microscope - Kipimo cha kuangalia damu            kwenye hadubini ili kuangalia kama kuna mabuu ya ugonjwa huu  wa        matende.

Kwa wale ambao wana ugonjwa huu kwa muda mrefu, mabuu hayaonekani kwenye damu kwani tayari yatakuwa yameshaingia kwenye mfumo wa limfu. Hivyo, kutoonekana kwa mabuu kwenye damu kwa kutumia hadubini si kigezo cha kusema kwamba mgonjwa hana ugonjwa
huu wa matende.

• Vipimo vyengine vinavyoweza kutumika ni pamoja na CT Scan, MRI, Doppler Ultrasound, Radionuclide Imaging ili kuweza kutofautisha ugonjwa huu na magonjwa mengine yanayosababisha kuvimba kwa miguu au mikono kama saratani za aina mbalimbali, kuganda kwa damu kwenye mishipa ya damu(blood clot) na kadhalika.

• Kwa wale wenye kuvimba korodani, ni muhimu kwa daktari kuchukua kipimo kwa kukwangua sehemu husika kisha kuchanganya na potassium hydroxide na kutazama kwenye hadubini kama kuna dalili (Meddler bodies, sclerotic bodies) za ugonjwa wa fangasi unaojulikana kama chromobalstomycosis (unaosababishwa na fangasi aina ya Fonsecaea pedrosoi, Phialophora verrucosa, Cladosporium carrionii, au Fonsecaea compacta). 

Pia ukungu huu huweza kuoteshwa maabara ili kuangalia kama kuna fangasi aina yoyote ile niliyotaja hapo juu watakaota.

 
Tiba ya ugonjwa wa matende ni nini?
Tiba ya ugonjwa wa matende hutegemea na sehemu husika. Kwa wagonjwa walio katika jangwa la sahara, tiba ni dawa aina ya albendazole pamoja na ivermectin. 

Kwa wagonjwa waliopo sehemu nyingine duniani tiba huusisha matumizi ya albendazole pamoja nadiethylcarbamazine.

Kusafisha sehemu iliyoathiriwa na ugonjwa wa matende mara kwa mara
husaidia kupunguza dalili na viashiria vya ugonjwa huu. 

Kwa wale waliovimba korodani kutokana na ugonjwa wa matende,
 
tiba yake ni upasuaji.
Wakati mwingine, kama mgonjwa atakuwa amevimba sana korodani, basi
baada ya kufanyiwa upasuaji wa kawaida, atahitaji kufanyiwa upasuaji kurekebishwa ngozi yake (plastic surgery)
.
Katika utafiti uliofanywa na chuo cha Liverpool school of tropical medicine
mwaka 2005, umeonyesha dawa ya antibiotiki hususan doxycyline inaweza
kutumika kutibu ugonjwa huu wa matende kutokana na minyoo (adult
worms) kuwa na bakteria aina ya wolbachia wanaoishi ndani ya minyoo hii,
hivyo dawa hii hutibu kwa kuua bakteria hawa na kusababisha minyoo hii kufa, na kuondosha kabisa microfilariae kwenye damu ya mgonjwa na hivyo mgonjwa kupona.

Dawa hii hutumika kwa muda wa wiki 8. Hata hivyo, kama mgonjwa
atakuwa na mabuu ndani ya mfumo wake wa limfu, basi itakuwa vigumu kwake kupona.

Utafiti zaidi unahitajika ili kuwa na uhakika zaidi juu ya dawa hii kutibu
ugonjwa huu.

 
Kinga ya ugonjwa wa matende ni nini?
• Shirika la afya duniani (WHO) limeanzisha jitihada za kutokomeza               ugonjwa huu wa matende ifikapo mwaka 2020.

• Matumizi ya dawa aina ya albendazole kwa wale walio katika hatari             kupata ugonjwa wa matende unaosababishwa na vimelea.

• Kuvaa viatu wakati wa kutembea nje ilikujikinga kupata maambukizi ya       aina yapodoconiosis.

• Kuosha miguu na mikono kwa kutumia maji na sabuni

• Kuosha miguu kila siku kwa kutumia antiseptic (bleach).

Tuesday, November 28, 2017

MKURUGENZI MKUU MSD AFANYA ZIARA HOSPITALI JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na viongozi mbalimbali wa Hospitali ya Sinza alipofanya  ziara ya kikazi katika Hospitali hiyo na  Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo, ili kubaini changamoto zilizopo za  upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na kuzipatia ufumbuzi wa pamoja. Kutoka kulia ni Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola.
 Maofisa wa Hospitali ya Sinza wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (hayupo pichani)
 Mkutano ukiendelea.
  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola, akizungumza katika mkutano huo.
 Laboratory Manager wa Hospitali ya Sinza, Emmanuel Kiponda, akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule, akizungumza kwenye mkutano huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Hospitali ya Sinza baada ya kufanya nao mazungumzo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, akiwa katika picha ya pamoja na maofisa mbalimbali wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.


Na Dotto Mwaibale

MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu amewatembelea wateja wa MSD wanaohudumiwa na Kanda ya MSD Dar e's Salaam ukiwa ni pamoja na Hospitali ya Mwananyamala na Sinza kubaini changamoto zilizopo katika upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ili kuzipatia ufumbuzi.

Katika ziara hiyo iliyofanyika jumanne jijini Dar es Salaam Bwanakunu amewataka wateja hao kufanya Maoteo ya mahitaji yao sahihi na kuyawasilisha Msd kwa wakati kwa mujibu wa sheria yaani tarehe 30 Januari kila mwaka,hasa dawa na vifaa tiba vinavyonunuliwa kwa Manunuzi maalumu.

Bwanakunu alihimiza watoa huduma katika hospitali hizo kutambua jukumu walilonalo katika usimamizi wa matumizi ya dawa na vifaa tiba kwa wananchi.

Akizungumza akiwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Bwanakunu alisema anazitambua changamoto zilizopo za usambaji wa dawa na vifaa tiba na wamedata msaada wa magari kutoka Global Fund ambayo yataboresha usambazaji kutoka mara nne kwa mwaka hadi mara sita kwa mwaka.

Kuhusu vifaa vya Manunuzi maalumu Bwanakunu amesema hospitali zikiwa zinaomba kwa wakati mmoja ingerahisisha kuagiza vifaa hivyo mapema,badala ya kila hospitali kuleta kwa wakati wake.

"Vifaa hivi tunaagiza nje ya nchi na mchakato wake unachukua muda mrefu na changamoto kubwa " alisema Bwanakunu.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola alisema hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali hiyo kwa sasa ni asilimia  80 .

"Changamoto iliyopo ni uhaba wa vitendanishi vya maabara na vifaa vya macho na meno ambavyo tunapata chini ya kiwango hivyo havikidhi mahitaji tuliyonayo," alisema.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Daniel Mkungu alisisitiza haja ya ushirikiano baina ya Hospitali hizo na MSD ili kuboresha huduma za afya hapa nchini.

Ziara hiyo ya mkurugenzi huyo itaendelea tena kesho katika baadhi ya hospitali zilizopo jijini Dar es Salaam.


Sunday, November 26, 2017

JPM ATOA NENO LA SHUKRANI KWA SERIKALI YA CHINA KWA KULETA MELI KUBWA ILIYOTOA MATIBABU BURE KWA WATANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameishukuru serikali ya watu wa China kwa msaada wao walioutoa kwa wananchi wa Tanzania wa kuwapatia matibabu bure, akisema jambo hilo ni upedo usio elezeka.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo alipoenda kutembelea meli yenye madaktari bingwa kutoka China ambayo imetia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam, na kutoa huduma za vipimo na matibabu kwa wakazi wa Dar es salaam bila gharama yoyote.

"Tunapenda kusema shukrani kwa dhati kwa serikali ya China kuamua kuituma meli na madaktari kuja Tanzania, tunafurahi kwa huduma zao, wameokoa maisha ya watanzania zaidi ya elfu 6,400, huu ni upendo wa pekee unaogusa, ndio maana leo nimeshindwa kuvumilia nimeona bora nije nishukuru, nimeguswa mno na ndugu zetu wachina, yapo mataifa mengine matajiri, yenye mali nyingi lakini hayajaguswa", amesema Rais Magufuli.

Sambamba na hayo Rais Magufuli amewakabidhi madaktari hao barua maalum kwenda kwa raisi wa nchi yao Xi Jinping pamoja na kinyago kama zawadi kwake, kumshukuru kwa mchango wake na ukarimu wake kwa watanzania masikini.

Pia Rasi Magufuli amewatakia safari njema madaktari hao na kuwaomba kurudi tena wakati mwengine, na kuwataka kukaa kwa muda mrefu zaidi ili waweze kutoa huduma kwa watanzania wengi hata watakaotoka mikoan

Thursday, November 23, 2017

VYAKULA VITANO MUHIMU KWA UKUAJI WA AKILI YA MTOTO


Na Jumia Food Tanzania

Miongoni mwa changamoto zinazowakumba wazazi wengi wa kitanzania ni kushindwa kufahamu na kupangilia vyakula sahihi kwa ukuaji wa afya za watoto wao. Afya ya akili ya mtoto ni kitu muhimu na cha kuzingatia kwani humfanya mtoto aweze kufanya shughuli tofauti kwa ukamilifu ikiwemo uwezo wake wa kujifunza shuleni pamoja na kushiriki michezo mbalimbali na wenzake.
Baadhi ya wazazi kwa kutokufahamu huwapatia watoto wao vyakula ambavyo huwa haviwasaidii watoto kwenye hatua ya ukuaji. Inawezekana watoto huwa hawapendelei vyakula hivyo muhimu kwa afya zao, lakini inashauriwa kuanza taratibu na hatimaye wanazoea. Jumia Food imekukusanyia aina tano za vyakula ambavyo ukianza kumpatia mtoto wako utashangazwa na ukuaji wa afya ya akili yake.

Mayai. Virutubisho vinavyopatikana kwenye mayai ni muhimu kwenye utengezaji wa seli zinazotunza kumbukumbu kwenye ubongo. Kadiri tunavyokuwa na seli nyingi ndivyo tunakuwa na uwezo mkubwa wa kuhifadhi kumbukumbu. Hivyo ni vizuri kuzingatia kujumuisha aina hii ya chakula unapomtayarishia mtoto wako chakula, kwa mfano asubuhi kabla mtoto hajakwenda shuleni.  

Maziwa. Maziwa yasiyo na mafuta yanajulikana kuwa chanzo kikubwa cha protini, Vitamini D na fosforasi. Lakini pia kalsiamu inayopatikana ndani yake inasaidia namna miili yetu inavyodhiti nishati. Kalsiamu pia ina mchango mkubwa kwa uzalishaji wa insulini kwenye miili yetu. Mbali na kunywa maziwa kama yalivyo unaweza kunogesha kwa kuongeza chokoleti. Wataalamu wanasema kwamba kuna kiasi kidogo cha ‘kafeini’ kwenye maziwa ya chokoleti, na yanakuwa karibu na kiasi sawa cha sukari iliyopo kwenye juisi za matunda.  

Matunda. Ukuaji wa afya ya akili ya mtoto huhitaji matunda kwani humsaidia kwenye mchakato mzima wa kujifunza. Lakini pia matunda husaidia katika mchakato mzima wa kulainisha choo hivyo kusaidia kwa kiasi kikubwa watoto wengi wanaokumbwa na changamoto hiyo. Ukiachana na maji na mazoezi, matunda ni mbinu bora ya kuwafanya watoto kuwa na afya bora na hivyo akili kuwa tayari kwa kujifunza. Ili kutomtia mtoto uvivu katika kula matunda, unaweza kumuandalia kwa kuyakata kwa mtindo wa vipande vidogovidogo.   
Maji. Jambo ambalo wazazi wengi hawalifahamu ni ambavyo watoto wao hunywa kiasi kidogo sana cha maji kutwa nzima. Wataalamu wengi wamekuwa wakionya namna maji ambavyo huwa yanapuuzwa kama chakula muhimu kwenye mwili wa binadamu, si kwa watoto tu bali hata watu wazima. Watoto muda mwingi huwa wanakuwa kwenye pilikapilika zao bila ya kuwa na maji ya kutosha mwilini. Kutokunywa maji au kutumia kwa kiasi kidogo huwafanya watoto kuhisi njaa isiyo ya lazima. Hakikisha kuwa unajumuisha maji kwenye kila mlo unaomuandalia mtoto wako.
Nyama. Ukosefu wa madini ya chuma ni miongoni mwa tatizo sugu linalotokana na upungufu wa lishe, na huongoza kwa magonjwa yanayotokana na upungufu wa lishe duniani. Na kutokufanya vizuri kwa watoto shuleni huweza kuwa dalili mojawapo. Kiasi cha nyama unachokitumia kwenye mlo kila siku kina faida kubwa ambayo huwezi kuifikiria. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, hata kiasi kidogo unachokula kwa kimeonyesha utofauti mkubwa kwenye uwezo wa mwili kufyonza madini ya chuma kutoka vyanzo mbalimbali.

Inafahamika kwamba wazazi wengi huwapatia watoto wao vyakula ambavyo ni muhimu kwenye ukuaji wao. Kama mzazi au mlezi jaribu aina mbalimbali ya vyakula mbali na vilivyoorodheshwa humu, fuata ushauri wa wataalamu mbalimbali wa afya au kusoma zaidi majarida tofauti ya afya na lishe.  

Wednesday, November 15, 2017

Maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani 2017, Wananchi wapewa Tahadhari

Na Binagi Media Group

Novemba 14 kila mwaka Tanzania huungana na mataifa mbalimbali kuadhimisha Siku ya Kisukari Duniani ambapo pamoja na mambo mengine, lengo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa kisukari ili kutambua namna ya kujiepusha na ugonjwa huo.

Katika kuadhimisha maadhimisho hayo mwaka huu yaliyofanyika jana, Chama cha Watoa Huduma za Afya Tanzania APHTA kwa kushirikiana na hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure, kilitoa fursa kwa wananchi kupima afya zao bure kwa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari.

Maadhimisho hayo kwa mkoa wa Mwanza yalifanyika kwenye uwanja wa Nyamagana ambapo mgeni rasmi ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Leonard Subi anawahimiza wananchi kuzingatia ulaji sahihi wa vyakula pamoja na kufanya mazoezi ili kujiepusha na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo kisukari.

Hata hivyo wananchi wanahimizwa kupima afya zao mara kwa mara ili kuepuka madhara wanayoweza kukumbana nayo kutokana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari, ikizingatiwa kwamba watanzania tisa kati ya 100 wenye umri wa miaka 25 na kuendelea wana ugonjwa wa kisukari ambapo kati ya hao tisa, ni wagonjwa wawili tu wenye kutambua kwamba wanaugua ugonjwa huo. https://youtu.be/IZTn8q3Cjrk  <iframe width="560" height="315" src="https://www.youtube.com/embed/IZTn8q3Cjrk" frameborder="0" gesture="media" allowfullscreen></iframe>

Mgeni Rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Leonard Subi (kushoto) akifanya uchunguzi wa afya yake kwenye maadhimisho hayo ya Siku ya Kisukari Duniani 2017 yaliyofanyika kwa mkoa wa Mwanza katika uwanja wa Nyamagana jana.

Mtaalamu wa afya akionyesha namba maalumu zinazotumika kufanyia utambuzi wa uono.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonard Subi akipokea maelezo kutoka banda la Abacus Pharma ambao ni wauzaji wa bidhaa za Sugar Free zisizo na athari ya kumsababishia mtumiaji ugonjwa wa kisukari.

Mwakilishi wa kampuni ya Abacus Pharma, Jeremiah Bwana akitoa maelekezo kwa wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo.

Monday, October 23, 2017

HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA SARATANI PAMOJA NA MATIBABU YA AWALI KUTOLEWA BURE KATIKA HOSPITALI ZA SERIKALI

Waganga wa vituo vyote vya Serikali hapa nchini wametakiwa kuhakikisha huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti zinatolewa bila malipo yeyote sambamba na matibabu ya awali.
Huduma za Uchunguzi wa Saratani kutolewa bila malipo
Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali kuamua kuboresha huduma hizo kwa kununua mashine 100 za tiba mgando,mashine 9 za upasuaji mdogo ambazo zitatumika kwa ajili ya matibabu ya awali ya saratani kwa wanawake pamoja na mitungi 173 ya gesi ya carbon dioxide zitakazowezesha mashine hizo kufanya kazi.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,wazee na Watoto Ummy Mwalim amebainisha hayo jijini Dar es salaam ambapo amevitaka vituo vya umma nchini kuhakikisha vinatenga siku maalum katika kila mwezi ili kuweza kuwahamasisha wanawake waweze kujitokeza kupata huduma hizo.

"natoa rai kwa wananchi hasa wanawake wenzangu kuhudhuria vituoni ili kuweza kupata huduma za uchunguzi mapema"alisema Ummy.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa katika kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje,Serikali ya awamu ya tano imeamua kuboresha huduma za afya hususani upande wa saratani ili kuweza kuhakikisha wagonjwa hao wanatibiwa hapa nchini.

Ifahamike kuwa takribani wagonjwa wapya elfu 50 kila mwaka wanagundulika kuwa na saratani ,na idadi hii inakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2020.

Tuesday, October 17, 2017

VYAKULA UNAVYOTAKIWA KUEPUKA KULA KAMA UNATAKA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI


Na Jumia Travel Tanzania

Leo siku ya Oktoba 16 dunia inaadhimisha Siku ya Chakula Duniani ambapo Shirika la Chakula Duniani (FAO) kila mwaka huadhimisha kwa shughuli na kauli mbiu mbalimbali. Kwa mwaka huu kauli mbiu ni ‘Badili Hali ya Uhamiaji ya Baadaye: Wekeza Katika Usalama wa Chakula na Maendeleo ya Vijijini.’ Kwa mujibu wa FAO, dunia inapitia mabadiliko kadha wa kadha kila kukicha. Watu wengi wamelazimika kuhama makazi yao kutokana na sababu tofauti kama vile kuongezeka kwa migogoro na kutokuwepo usalama wa kisiasa. Lakini njaa, umasikini, na kuongezeka kwa matukio ya hali ya hewa yanayochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa ni sababu zingine za muhimu zinazochangia katika kupelekea watu kuhama.    

Miongoni mwa changamoto kubwa inayowakumba watu siku za hivi karibuni ni katika upatikanaji wa chakula, matumizi yake na namna ya kudhibiti ili kutoleta athari katika mwili. Kwa kuwa leo ni maadhimisho ya ‘Siku ya Chakula Duniani,’ Jumia Travel ingependa kukushirikisha aina za vyakula vya kupunguza au kuacha kula kabisa kama unataka kupunguza uzito wa mwili wako.

Friday, October 13, 2017

MRADI WA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA AWALI YA SARATANI YA MLANGO WA SHINGO YA KIZAZI UMEFUNGWA RASMI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Leo ikiwa ni tarehe 13 mwezi octoba ni Siku ya kufunga mradi wa miaka mitano uliolenga kupunguza athali za saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake wa kitanzania.
Mkurugenzi Mkazi wa Maria Stopes Bw. Anil Tambay akitoa hotuba fupi katika siku ya kufungwa kwa mradi wa uchunguzi na matibabu ya awali ya saratani ya mlango wa shingo ya kizazi, hafra iliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.

Mradi huu uliojikita kwenye uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na utoaji wa matibabu ya awali, ulitekelezwa kwa kiasi kikubwa na Marie Stopes Tanzania, PSI/Tanzania na UMATI.


Katika kipindi cha miaka mitano cha utekelezaji wa mradi, vilianzishwa vituo 79 katika mikoa 22 nchini Tanzania na watoa huduma za afya 210 wakapatiwa mafunzo ya utoaji wa huduma hiyo.

Kwa uwezeshaji uliofanywa na Taasi ya Bill and Melinda Gates, mradi uliweza kuwafikia takribani wanawake 187,267 waliopata huduma ya uchunguzi na wanawake 7,602 wakipatiwa matibabu.
Mawakilishi wa Mkurugenzi wa Afya ya mama na mtoto kutoka wizara ya afya Bi. Safina Yuma akiwasilisha taarifa na hatua zilizochukuliwa na serikali katika kupunguza tatizo hilo la saratani ya mlango wa shingo ya kizazi, katika hafla fupi iliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam

Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha afya ya uzazi kilichopo chini ya wizara ya afya amesema; “Saratani ya mlango wa kizazi ni tatizo kubwa Tanzania. Kwa ushahidi uliopo, saratani ya mlango wa kizazi inaongoza kwa kusababisha madhala na vifo vitokanavyo na saratani kwa zaidi ya miaka kumi. Katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ambacho ni kituo pekee cha saratani Tanzania, inaonesha kuwa asilimia 38 ya wagonjwa wapya wa saratani waliopokwa katika kitengo hicho mwaka 2015 walikuwa ni wa saratani ya mlango ya kizazi. Takwimu hizi zimetokana na takwimu za usajili wa wagonjwa  Katika taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

Amesema, “wizara imeweka juhudi kubwa katika kupambana na saratani ya mlango wa kizazi nchini, mipango inayoendelea inalenga pia kuimarisha miradi ya saratani ya matiti na saratani ya tezi dume. Pia wamepiga hatua katika kuhakikisha wanaboresha upatikanaji wa huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na matibabu yake nchini. Kwa sasa kuna vituo 466 vinavyotoa huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na matibabu ambavyo ni hospitali zote za mkoa na wilaya nchini, na baadhi ya vituo vya afya na zahanati.
Mkurugenzi wa Afya ya Uzazi wa PSI Bi. Produnce Masako akitoa ufafanuzi wa jambo fulani katika mkutano wa "kufungwa kwa uchunguzi na matibabu ya saratani ya mlango wa shingo ya kizazi" uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.

Ameongeza, “Licha ya jitihada hizi zinazoendelea bado hatujaweza kukidhi mahitaji hata kufikia asilimia 10, wanawake wachache sana wamepata huduma ya uchunguzi hasa kwa wanawake walio maeneo yasiyofikika kirahisi. Kwa sababu hii, wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto inaahidi kuwezesha juhudi za kuboresha na kukuza huduma za saratani ya mlango wa kizazi ikijikita zaidi katika huduma za msingi za kinga na uchunguzi wa mabadiliko ya awali ya saratani hii.

Wizara ikiwezeshwa na GFF imenunua mashine 100 za kutoa tiba ya mgando ya mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi (cryotherapy) na mashine 9 za matibabu ya juu ya mabadiliko hayo ya awali (LEEP) ili kuboresha upatikanaji wa huduma ya uchunguzi na matibabu katika vituo 90 nchini.
Mkurugenzi wa Afya ya Mama na Mtoto wa Maria Stopes Dr. Jeremiah Makula akiichambua ripoti ya "mradi wa uchunguzi na matibabu wa saratani ya mlango wa shingo ya kizazi" mbale ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Marie Stopes Tanzania amesema, “mradi huu umetuacha na mafundisho mengi  ambayo yanaweza kutumiwa na wadau mbalimbali wanaotekeleza miradi ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi nchini Tanzania na amewataka wadau kutumia elimu hii iliyotokana na uzoefu wa kazi iliyofanywa na MST, PSI na UMATI badala ya kusumbuka kubuni vitu ambavyo tayari vimefanywa na mashirika haya.


Alifafanua kuwa majaribio ya utaratibu wa kutoa huduma ya uchunguzi wa saratani ya kizazi kwa kwa utaratibu wa huduma ya mkoba kwa kutumia kipimo cha HPV / DNA umekuwa ni wa ufanisi na kuwa ni utaratibu wa kwanza kufanikiwa duniani wa kuhakikisha mama anafanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu siku hiyo hiyo kwa kutumia care-HPV™ katika nchi zinazoendelea. 
Baadhi ya washiriki kutoka Hospitali, Taasisi mbalimbali pamoja na waandishi wa habari walioudhuria semina hiyo.