Wednesday, January 31, 2018

VIDEO-TBL WAELEZA KILICHOTOKEA MPAKA MTANDAO WAO UKADUKULIWA

Baada ya kudukuliwa kwa mtandao wa Castle Lite, Mkurugenzi wa masoko TBL Afrika mashariki, Bw. Thomas Kamphuis aelezea kilichotokea.

NAPE AENDELEA KUICHACHAFYA SERIKALI

Mbunge Nape Nnauye leo Bungeni ameipa changamoto Serikali juu ya gharama za kuunganisha umeme na kuishauri kuendelea kuchaji elfu 27,000 hata baada ya mradi wa REA kupita ambapo wataanza kuchaji 177,000 kuunganisha umeme.
              Tokeo la picha la NAPE NAUYE
Nape Nnauye ametoa ushauri huo alipopata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza Bungeni kwenda kwenye Wizara ya Nishati

"Kwanza niipongeze Serikali chini ya Wizara ya Nishati kwa kazi nzuri wanayofanya ya usambazaji mzuri wa umeme vijijini hasa REA awamu ya 3, kwa kuwa gharama za kuunganisha umeme wakati mradi unaendelea ni elfu 27,000 na mradi ukipita ni 177,000 na kwa kuwa idadi kubwa na nzuri ya watumiaji wa umeme ni biashara nzuri kwa TANESCO kwanini bei hii isiwe moja ya elfu 27" alisema Nape Nnauye

Hata hivyo Nape Nnauye aliendelea kusisitiza kuwa kama jambo hilo halitawezekana basi REA waendelee na uwekaji wa nguzo na miundombinu na TANESCO wafanye kazi moja ya kupeleka umeme na kukusanya kodi baada ya kupeleka umeme.

Naibu Waziri Wizara ya Nishati alijibu hoja hiyo na kudai kuwa amepokea ushauri huo wa Mbunge wa Mtama na kuwa atapeleka katika ngazi zingine na kuona Serikali nini itafanya

"Wazo alilosema Kaka yangu Nape Nnauye linapokelewa na litafanyiwa kazi kwani ni la msingi kwa sababu Wizara yetu na shirika letu la TANESCO na wadau wengine wa nishati tunauza bidhaa hii hivyo ni vema tunapouza tupate wateja wengi ili tupate mapato na kuendesha shughuli mbalimbali na uwekezaji mpya wa maeneoya nishati"

MBUNGE KABATI ATOA MSAADA WA MIFUKO 25 YA SARUJI KATIKA KANISA LA FREE PENTECOST CHURCH OF TANZANIA

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akimkabidhi mchungaji
wa kanisa hilo la Free Pentecost Church of Tanzania Francis Okero huku akiwa sambamba na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na viongozi mbalimbali  wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa pamoja na madiwani wa chama hicho.
 Hili ndio kanisa la la Free Pentecost Church of Tanzania ambalo mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ametoa msaada wa mifuko ishirini na tano (25) katika kanisa la Free Pentecost Church of Tanzania lililopo kata ya Isakalilo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa jipya ili kuendelea kutoa huduma bora ya neon la mungu.

Akizungumza wakati wa ibada iliyofanyika katika kanisani hilo Kabati alisema kuwa ni heri kujibembeleza kwa mwenye mungu kuliko kujipendekeza kwa binadamu mwenzako hivyo ni bora kuchangia shughuli za kihoro kuliko shughuli za kidunia.

“Mimi nimejitoa kuchangia shughuli zote zinazo muhusu mungu hivyo naomba mnishirikishe nami nitakuja bila kusita kwa kuwa ndio kazi yangu hata iliyonifanikisha mimi kuwa mbunge” alisema Kabati

Kabati alisema kuwa aliwaahidi kuwapa mifuko ishirini na tano ya saruji hivyo ametimiza ahadi hiyo kwa kuwapa mifuko ya saruji yote aliyoiadi hivyo amefanikiwa kutekeleza na kuwaomba wananchi wananchi wengine kuchangia maendeleo ya kanisani.

“Alikuja diwani hapa kwa niaba yangu na kuahidi mifuko hiyo ambayo ni sawa na tani moja hivyo nimeamua kutimiza kuwa lengo langu nikiahidi kitu lazima nitimize malengo yangu ya kuitoa ahadi hiyo” alisema Kabati

Aidha Kabati aliwata wananchi na viongozi mbalimbali kuendelea kuchangia shughuli za kimaendeleo kwa jamii na taasisi ambazo hazina uwezo wa kufikia mafanikio yanayotakiwa kwa ajili ya kutatua kero zinazorudisha nyuma maendeleo.

Kabati amesema kuwa wananchi na viongozi wanatakiwa kumtegemea mungu ili kuweza kufanikisha malengo wanayotarajia.

Katika hatua nyingine Kabati amewataka wazazi kuwapeleka shule watoto wao ili wakapate elimu ambayo ndiyo itakuwa dira ya maisha yao ya baadae.

Kwa uoande wake mchungaji wa kanisa hilo la Free Pentecost Church of Tanzania Francis Okero alisema kuwa walikuja viongozi wengi na kutoa ahadi nyingi lakini hakuna hata mmoja aliyetimiza ahadi yake zaidi ya mbunge Ritta Kabati.

"Nilialika wageni wengi wakala na kutoa ahadi nyingi kwa mbwembwe nyingi lakini kilichotokea hadi sana viongozi wote hakuna aliyetimiza malengo hayo hivyo nichukue furasa kushukuru" alisema Okero

Mchungaji Okero alimshukuru mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake ambayo itatusaidia katika ujenzi wa kanisa letu

SOMA HAPA SERA ZA MTULIA AKIWAOMBA WANA KINONDONI WAMPE RIDHAA YA KUONGOZA TENA JIMBO HILO.


Image may contain: one or more people, people on stage, crowd and outdoor

Mgombea Ubunge katika jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CCM Maulid Said Mtulia akinadi sera zake jukwaani na kuomba kura kwa wapiga kura wa Kata ya Ndugumbi.


**********

*YALIYOSEMWA NA MGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA KINONDONI, MAULID SAID MTULIA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI KATA YA NDUGUMBI JUMANNE JANUARI 30, 2018*

"Kama Mtulia angekuwa amenunuliwa asingepewa tena dhamana ya kugombea Ubunge " - Mtulia

"Ningekaaje kwenye chama ambacho Mwenyekiti na Katibu hawaelewani, nimejitoa ili niwe na uhuru wa kuwatumikia wana Kinondoni." - Mtulia


"Kile chama hamkusikia kimesimamisha wabunge 8, mlitaka nami nisimamishwe?" - Mtulia



"Mtulia nimejiuzulu ili kuwaokoa Wananchi wa jimbo la Kinondoni" - Mtulia


"Kuhama chama ili kujiunga na chama chenye maendeleo, huo ni usaliti?" - Mtulia

"Mtulia huyu ndio aliotoa hela yake mfukoni kujenga visima vya maji; Mtulia aliyefungua kesi mahakamani kuzuia bomoa bomoa; ndio Mtulia yule aliyeomba maghorofa ya Magomeni Watu waliojitokeza nyumba zao wakae bure" - Mtulia

"Mtulia mimi ni yule yule mkinichagua nitahakikisha naendelea kuwaletea maendeleo nikishirikiana na viongozi wenzangu na Rais wangu mpendwa Di. Magufuli " - Mtulia

"Ninaomba tena ridhaa ili nihakikishe nawaletea maendeleo wana Kinondoni kutokana na kugombea kwenye chama chenye ilani ya uchaguzi iliyoshikan dola" - Mtulia

"Naomba dhamana ya kugombea ili nikashirikiane na wenzangu kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2015 - 2020" - Mtulia

"Kazi yangu mkinichagua ni kwenda kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na si porojo wala usanii" - Mtulia

"Ukichagua Mtulia umechagua maendeleo; ukimchagua Mtulia umejenga daraja kati ya Wananchi na Serikali" - Mtulia

Monday, January 29, 2018

MPYA--MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2017 YAPO HAPA

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

CSEE 2017 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES

BONYEZA HERUFI YA KWANZA YA JINA LA SHULE YAKO UTAPATA MATOKEO YAKO


CLICK ANY LETTER BELOW TO FILTER CENTRES BY ALPHABET


A

B

C

D

E

F

G

H

I

J

K

L

M

N

O

P

Q

R

S

T

U

V

W

X

Y

Z

Form Four Secondary Education Examinations (CSEE) results released today by the National Examinations Council of Tanzania (Necta).
The National Examinations Council of Tanzania (Necta) executive secretary announces the results of Form Four  national examinations ,
 Cheki matokeo ya kidato cha nne bofya hapa >>> Form Four National Assessment (CSEE) results released

Kupata habari zetu kwa urahisi zaidi kwa sasa Tafadhali tembelea Platform zetu zifuatazo.

Bonyeza hapa --Facebook

Bonyeza hapa--Twitter

Bonyeza hapa--Youtube

KUSOMA HABARI ZOTE ZA MTANDAO HUU BONYEZA HAPA HAPA HAPA HAPA HAPA HAPA HAPA HAPA 
KWA HABARI ZA PAPO KWA PAPO TUCHEKI WHATUP 0752402602 

BASI LA TAHMEED LAWAKA MOTO SOMA HAPA KUJUA.

Basi kampuni ya Tahmeed  lililokuwa likitoka jijini Dar es Salaam kwenda Mombasa, Kenya limeteketea kwa moto leo Januari 29, mwaka 2018  katika kijiji cha Kitumbi wilayani Handeni mkoani Tanga.

Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Handeni, William Nyero amesema polisi wapo eneo la tukio na hakuna madhara yoyote kwa abiria waliokuwa kwenye basi hilo.

Amesema dereva wa basi hilo baada ya kubaini kasoro aliliegesha pembeni na abiria kuteremka, kushusha mizigo yao.

"Abiria wote waliokuwa wakisafiri na basi hilo wapo salama. Baada ya abiria kushuka na kushusha mizigo yao basi liliwaka moto,” amesema.

DK. SLAA AKUTANA NA RAIS MAGUFULI IKULU LEO, SOMA HAPA KUJUA WALICHOKIZUNGUMZA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Januari, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mteule Mhe. Dkt. Wilbrod Peter Slaa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya Mazungumzo hayo Balozi Mteule Mhe. Dkt. Slaa amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Balozi na ameahidi kuwa yupo tayari kutekeleza majukumu atakayopangiwa kwa kutanguliza maslahi ya Taifa.

Mhe. Dkt. Slaa amempongeza Mhe. Rais Magufuli na Serikali yake ya Awamu ya Tano kwa uongozi bora wenye maono na uthubutu wa kutekeleza mambo makubwa yenye maslahi kwa nchi ikiwemo miradi mikubwa kama vile ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), ujenzi wa daraja la juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela (Tazara), mradi wa uzalishaji umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stieglers’ Gorge) na mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

“Kwa kweli naona faraja, ninafurahi Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza hatua kwa hatua karibu yote tuliyokuwa tunayapigania kwa miaka takribani 20 ya huko nyuma, na mimi Dkt. Slaa nilikuwa napiga kelele kwa sababu nilikuwa naona kuna upungufu.

“Leo ninasema ninafurahi yale niliyokuwa napigia kelele yanatekelezwa kwa sababu nimeyaona, sasa kitu kikubwa ni macho, ushabiki katika maendeleo hauna tija, ushabiki katika siasa nao hauna tija, kama nilivyowahi kueleza huko nyuma siasa ni sayansi, wapo wanaofikiri siasa ni upotoshaji na siasa ni udanganyifu lakini siasa ni sayansi, na siasa kama ni sayansi ina misingi yake inayohitaji kusimamiwa, na misingi yake ni nini kilikuwa ni tatizo na tatizo hilo linatatuliwa kwa misingi ipi, sasa haya tunayoyasema ni hivi, tulikuwa na tatizo la umeme, Stieglers’ Gorge inaanza kujengwa, na miradi mingine mikubwa inatekelezwa, haya ndio mambo ya msingi” amesema Mhe. Dkt. Slaa.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Dkt. Slaa kwa moyo wake wa kizalendo na amesema aliamua kumteua kuwa Balozi kwa kuwa anatambua kuwa ataweza kupigania maslahi ya Tanzania popote atakapopangiwa kuiwakilisha.

“Dkt. Slaa alinijulisha kuwa anakuja na akaomba akija angependa kuja kuniona na nikampangia leo, tumezungumza mambo mengi na ameniahidi kuwa atakwenda kufanya kazi yake vizuri kwenye nchi atakayokwenda kuwa Balozi.

“Mhe. Dkt. Wilbrod Slaa ni mtu safi, anazungumza kutoka moyoni na anaipenda Tanzania na mimi kutokana na moyo wake wa kuchukia ufisadi na kuchukia wizi nikaamua kumteua kuwa Balozi” Amesema Mhe. Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameagana na maafisa wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao wanastaafu baada ya kutimiza umri.

Walioagana na Mhe. Rais Magufuli ni Luteni Jenerali James Mwakibolwa aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ na Meja Jenerali Michael Isamuhyo aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Wengine ni Brigedia Jenerali Aron Lukyaa, Brigedia Jenerali William Kivuyo, Brigedia Jenerali Elizaphani Marembo na Kanali Peter Samegi.

Akizungumza baada ya kuagana, Luteni Jenerali Mwakibolwa amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ na amesema anaondoka na kuliacha jeshi likiwa na nidhamu, utii, uzalendo na weledi.

Nae Meja Jenerali Isamuhyo pamoja na kumshukuru Mhe. Rais Magufuli  amesema anafurahi kuiacha JKT ikiwa imeimarika katika majukumu yake yakiwemo ujenzi wa viwanda, kilimo na kuimarisha mafunzo kwa vijana wazalendo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
29 Januari, 2018

UFAFANUZI WA KUKAMATWA KWA GARI YA MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM.

Ndugu waandishi wa habari. Napenda kutumia fursa hii kuwapa pole wananchi wa jiji la Dar es Salaam kutokana na taarifa ambazo zimeripotiwa leo kwenye baadhi ya magazeti.

Image result for gari la meya wa jiji

Jumamosi ya Tarehe 27 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita alishiriki kwenye kampeni za mgombea  Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Salum Mwalimu ambapo. Ambapo kabla ya kufika kwenye eneo mbalo kampeni hizo zinafanyika Dereva alimshusha  Meya ,na kuchukua gari nyingine kuelekea kwenye eneo ambalo kampeni hizo zilikuwa zikifanyika.

Kwakuwa Magari ya serikali hupaki kwenye Taasisi za Umma,  Dereva alikwenda kupaki gari kwenye ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM. Hata hivyo baada ya muda , walijitokeza vijana kadhaa na kutoa upepo gari hiyo bila kufahamu sababu  wakati huo ambapo dereva na wenzake  wawili walikuwa wameenda kula.

Ndugu  waandishi wa habari. Baada ya kufanyika kwa tukio hiko, licha ya dereva huyo kujieleza na kutoa vitambulisho kuwa ni mtumishi wa serikali nasio wa chama, bado waliendelea kumtuhumu kwamba alikuwa na lengo la kuvuruga uchaguzi na hivyo walimkamata, wakampiga na baade alipelekwa kituo cha polisi Magomeni kwa ajili ya kuhojiwa.


 Naomba ifahamike kuwa Meya wa jiji hawezi kujihusisha kwenye matukio ya kupanga njama zozote kwa ajili ya kufanya vurugu kwenye matukio yoyote ya kisiasa hususani kwenye uchaguzi.

Ndugu waandishi wa habari. Napenda kuwaeleza wananchi wa jiji la Dar es Salaam kuwa, Meya wa jiji hakuwahi kushiriki,wala kujihusisha na matukio yoyote ya kufanya vurugu wakati wakampeni za uchaguzi wala matukio ya kisiasa kama ambavyo taarifa hiyo imetolewa na Vijana wa UVCCM.

Mazungumzo ambayo yalikuwa yakifanyika kwa kutumia ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu ,ilikuwa ni baina ya Dereva na Katibu wa Meya ambapo alikuwa akipewa taarifa kuhusu kukamatwa kwa gari hiyo. Ambapo namba hizo ni 0784………16 dereva, katibu ni 0717 …….52.

Meya wa jiji amewahi kushiriki kampeni za uchaguzi mdogo wa marudio ya Udiwani kata ya Kijichi lakini haikuwahi kutokea vurugu yoyote. Hivyo taarifa ya kusema kwamba amekuwa akijihusisha kwenye matukio hayo hazina ukweli wowote na kwamba zinalenga kulichafua jina na heshima kubwa ya kisiasa aliyojiwekea tangu achaguliwe kuliongoza jiji hili.

Meya wa jiji amekuwa akifanya kazi zake za kuliongoza jiji bila kuwepo na mvutano na kiongozi yoyote serikalini, kisiasa, licha ya kwamba nafasi yake inatokana na chama cha upinzani. Lakini  ielewe kuwa kushiriki kwakwe kwenye kampeni hakukuwa na maana ya kupanga njama yoyote ya kihalifu bali alihudhuria kama viongozi wengine wanavyo hudhuria kwenye shuguli hizo.

Meya wa jiji amesikitishwa na kulaani vikali kitendo cha kukamatwa kwa gari lake na kutolewa upepo Dereva wake hali ya kuwa ni mtumishi wa serikali na kwamba jambo hilo linapoteza taswira bora ya katika uongozi.

Gari ya serikali kupaki kwenye ofisi yoyote sio jambo baya kwa kuwa haikuwa na bendera ya chama na kwamba hakukuwa na sababu za kulikamata na kuihuisha kwa mbinu mbaya ambayo inalenga kuchafua sifa ya jiji.

Hivyo niombe jeshi la polisi kwakuwa wote ni watumishi wa serikali, wanawatumikia wananchi, kama itawapendeza kufanya uchunguzi wao wa kina kuhusiana na jambo hili, ikiwa ni pamoja na kutenda haki bila kujali kwamba tukio hili linatokana na mtu wa chama gani.

Imetolewa leo Januari 29, 2018 na

Christina Mwagala, Ofisa habari na Msemaji Mkuu wa Mshiki Meya wa jiji la Dar es Salaam.

Sunday, January 28, 2018

DKT. SHENI "SIWEZI KUONGEZA MUDA WA UTAWALA, MUDA WANGU UKIISHA NTAONDOKA MAPEMA TU".

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein amesema hayupo tayari kuongeza muda wa uongozi kutoka miaka mitano hadi saba kwani kufanya hivyo ni kukiuka katiba ya Zanzibar.
Dkt Shein amesisitiza kwamba, aliapa kuilinda katiba ya Zanzibar hivyo hawezi kubadilisha muda wa uongozi na hakuna mtu atakayemfanya abadilishe au amvutie yeye kuendelea kukaa madarakani.

Rais Dkt Shein ameyasema hayo jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume visiwani Zanzibar alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baaada ya kurejea kutoka kwenye ziara ya wiki moja katika nchi za Falme za Kiarabu (UAE) alipokua ameambatana na mke wake, Mama Mwanamwema Shein.

“Mimi naheshimu katiba ya Zanzibar, na nina heshimu sheria za Zanzibar. Muda wangu ukifika nitaondoka haraka sana. Hakuna atakayenilazimisha mimi nikae, au atakayenivutia mimi nikae”alisema Rais Dkt Shein.

Aidha, Dkt Shein amesema kuwa, alisikia wawakilishi katika Baraza la Wawakilishi wakizungumza hilo, lakini hawazuiwi kujadili kwani wanafanya hivyo kwa mujibu wa sheria, lakini yeye hayuko tayari kuongeza muda.

“Hilo walizungumza wawakilishi barazani, wana haki ya kuzungumza, kwa mujibu wa taratibu zao na sheria zao na yeyote mwingine anaweza kuzungumza. Mimi nilisikia wakati wananzungumza, Mwakilishi mmoja akasema kwamba kuna baadhi ya nchi duniani zina miaka mitano nyingine saba, sasa kwanini na sisi tusiwe na miaka saba!”

Rais Dkt Shein amesema kuwa, suala la miaka saba labda linaweza kuwepo baada ya yeye kutoka lakini hadhani kama kuna jambo kama hilo.

“Mie sijalisema, sitolisema, na hakuna atayanilazimisha niliseme”alihitimisha Rais Dkt Shein, huku akitilia mkazo kwamba, muda wake ukiisha atamchukua mkewe na kumwambia waondoke