Tuesday, January 31, 2017

JUMIA TRAVEL YAJIKITA KATIKA UTALII




Na Jumia Travel Tanzania


Mwaka wa 2016 ulikuwa wenye mafanikio makubwa kwa sekta ya utalii duniani ambapo kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO), watu bilioni 1.2 walisafiri duniani huku waliotembelea Afrika wakiwa milioni 58.

CUF YA PROFESA LIPUMBA YAJIBU MAPIGO KUHUSU RUZUKU WALIYOPEWA NA HAZINA


Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi (Taifa) wa Chama cha Wananchi (CUF), Thomas D.C Malima (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam leo kuhusu ruzuku ya chama hicho iliyopokelewa kupitia akaunti namba 2072300456 ya Benki ya NMB Tawi la Temeke. Kulia ni Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Mneke Jafar na Katibu Jumuiya ya Wanawake (JUKE), Salama Masoud.
Meza Kuu. Kutoka kulia ni Kamanda Mkuu, Athumani Hamadi,Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Mneke Jafar, Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi (Taifa) wa Chama cha Wananchi (CUF), Thomas D.C Malima, Katibu Jumuiya ya Wanawake (JUKE), Salama Masoud na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Masha Amour.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Mkutano ukiendelea.

Injury News: Bocco, Kingue, Sure Boy


BAADA ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, kuanza rasmi mazoezi jana jioni kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Ndanda, daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa, amezungumzia hali za kiafya za baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi.

DKT. MWAKYEMBE AZINDUA RASMI OFISI ZA WIZARA YAKE MKOANI DODOMA

Katibu Mkuu Prof sifuni Mchome akitoa maelezo mafupi kwa Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe mara baada ya kukata utepe na kuzindua rasmi ofisi za wizara mjini Dodoma

Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kukata utepe na kuingia ndani ya jengo la Wizara ambako alizindua rasmi ofisi za wizara mjini Dodoma

Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe katika picha ya pamoja na watumishi na wageni wake mara baada ya kuzindua rasmi  ofisi za wizara mjini Dodoma
ambako wizara imehamia rasmi mkoani Dodoma


Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikata utepe kuzindua rasmi Makao Makuu ya Wizara yaliyopo katika jengo la Masomo ya Biashara na Sheria katika Chuo Kikuu cha Dodoma ambako Wizara imehamia rasmi makao maku ya Serikali mkoani Dodoma

Breaking Newzz--Tizama matokeo ya kidato cha nne 2016 Hapa

matokeo ya mtihani kidato cha nneBaraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.

Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.

Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60

Shule 10 bora kitaifa
 
Shule kumi (10) za mwisho kitaifa-Dar es salaam yaongoza ​
 

Benki ya KCB Tanzania yatoa mafunzo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali Mkoa wa Arusha.

Meneja wa kanda ya kaskazini wa Benki ya KCB Tanzania Judith Lubuva (aliyekaa wapili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali waliohudhuria na kumaliza mafunzo ya ujasiriamali yalitolewa na benki hiyo katika mkoa wa Arusha.

Meneja wa kanda ya kaskazini wa Benki ya KCB Tanzania Judith Lubuva, akiongea na wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hyo mkoani Arusha.

Mwalimu wa Ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Nina Nchimbi akitoa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania kwa wanawake wajasiriamali wa mkoa wa Arusha.

Afisa Mawasiliano ya Umma wa benki ya KCB Margaret Makere akiongea na wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hiyo mkoani Arusha.

Katika swala zima la kumkomboa mwanamke mjasajiriamali, Benki ya KCB Tanzania inaendelea na programu ya mafunzo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali yanayoitwa 2JIAJIRI. Programu hii inalenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika changamoto zinazosababisha biashara yake ishindwe kuendelea.
Benki ya KCB imepanga kufundisha wanawake wajasiriamali 315 kutoka mikoa ya Dar Es salaam, Mwanza, Morogoro, Arusha, Moshi na Zanzibar  ambapo matawi ya benki hiyo yapo.
Mafunzo haya ni bure kabisa, benki ya KCB inagharimia gharama zote. na yanahusisha Elimu ya Fedha (Financial Literacy), Kufikiwa huduma za kifedha (Financial Inclusion), Masuala ya Kisheria (Legal Framework), Ushindani wa Kibiashara (Business Competitiveness) na kuwa na sifa za kukopesheka (How to be bankable).
Zaidi ya mafunzo hayo, benki ya KCB itawapatia wanawake wajasiriamali hao maafisa watakao wafundisha kwa vitendo kwenye maeneo ya biashara zao. Maafisa hao watakua ni afisa fedha, afisa sharia na afisa masoko.
Kwako mwanamke mjasiliamali “JIULIZE KWANINI uhangaike wakati benki ya KCB tupo!”

ANNA ABDALAH AWATAKA VIONGOZI WANAWAKE WAWAFUNDE WASICHANA ILI WAWE VIONGOZI BORA WA BAADAYE

 Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guide Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimvisha beji Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,  Zakhia Meghji wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam juzi. 
 Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi, akimpongeza Anna Abdalah 

Monday, January 30, 2017

Rais wa Guinea achaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Afrika (AU)

Rais wa Guinea, Alpha Conde amechaguliwa leo kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika (AU), uchaguzi uliofanyika katika vikao vya viongozi wa nchi wanachama vinavyoendelea katika Makao Makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Mkutano Wa 6 Wa Bunge Kuanza Kesho.....Wabunge 4 Kula Kiapo, Maswali 125 Kuulizwa Na 16 Ya Papo Kwa Papo Kwa Waziri Mkuu

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Masiliano Ofisi ya Bunge, Owen Mwandumbya akizungumza na wanahabi mjini Dodoma leo akitoa taarifa ya yale yatakayojiri katika Mkutano wa sita wa Bunge la 11 unaotaraji kuanza kesho Januari 31 hadi Februari 10 mwaka huu mjini Dodoma.

RAIS MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA - UN


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres mara baada ya mazungumzo yao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Malawi Peter Mutharika kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Rais wa Malawi Peter Mutharika pamoja na viongozi wengine mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Kidemokrasia ya Sahrawi(SADR) Brahim Ghali katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia. 


PICHA NA IKULU

Zimetufikia Habari mbaya za Kupigwa Risasi kwa Mwenyekiti wa CCM Mbeya

Mwenyekiti was CCM wilaya ya Mbeya mjini ndugu Ephrahim Mwaitenda akifikishwa hospitali ya Rufaa mkoa wa Mbeya asubuhi ya leo Jumatatu Januari 30,2017
Kulia ni kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya ndugu Lobe Zongo akimpokea Mwaitenda katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya baada ya kudaiwa kupigwa risasi. Chanzo Kalulunga blog


Taarifa zaidi tutawaletea hivi punde

ZIARA YA KIKAZI YA NAIBU WAZIRI MASAUNI MKOANI KATAVI

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akiongozwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando wakati akiwasili ofisi ya mkoa huo kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kuona changamoto za  masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.Wengine ni viongozi wa  serikali mkoani hapo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) 
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando (kushoto), akitoa taarifa ya Mkoa  kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya  Naibu Waziri huyo mkoani hapo ikiwa na lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi. (Picha na Wizara ya Mambo ya  Ndani ya Nchi)

Katibu Tawala Mkoa wa Katavi, Paul Chagonja akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo  mkoani hapo yenye  lengo la kuona changamoto za  masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Sunday, January 29, 2017

WATANZANIA WAOMBWA KUMUUNGA MKONO RAIS DK.JOHN MAGUFULI

 Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, John Shibuda (katikati), akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kuuaga mwaka wa 2016 na kuukaribisha mwaka 2017 Dar es Salaam jana. Kulia ni Msajili Msaidizi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Sisty Nyahoza na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ADA na Waziri wa Nchi asiye na Wizara Maalum, Zanzibar.
 Mkutano ukiendelea.
 Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwanahabari Suleiman Msuya akiuliza swali katika mkutano huo.

Maalim Seif ajitangaza atakuwa Rais Zanzibar,Waliookolewa Mgodini Geita wasimulia makubwa,Mwinyi ataka mahakama kutoa Haki Bila kuingiliwa,Zanzibar yapata uhaba wa Mchanga,Yanga yaishusha simba Kileleni,Soma magazeti ya leo Jumatatu Jan 30,2017

ZIARA YA KIKAZI YA NAIBU WAZIRI MASAUNI WILAYANI NKASI KUTEMBELEA IDARA ZA WIZARA

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili wilayani Nkasi kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kupitia shughuli zinazofanywa na idara zilizopo ndani ya wizara yake na kubaini changamoto wanazokutana nazo na kuzitafutia ufumbuzi.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mtanda. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) 

CHUO CHA AFRICA GRADUATE UNIVERSITY CHAWATUNUKU PhD WANAOFANYA KAZI ZA JAMII NCHINI


Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University  cha jijini Dar es Salaam, Profesa Stiven Nzowa, akiongoza mahafali ya kuwatunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD) wanaharakati na watumishi wa mungu nane pamoja na wengine kadhaa waliotunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili HDD Dar es Salaam jana.
 Mwanaharakati wa Haki za Watoto ambaye ni Rais wa Tanzania Music Foundation Dk.Donald Kisanga aliyetunukiwa PhD ya masuala ya Usimamizi na Uongozi wa Biashara akiwa kwenye mahafali ya 30 ya Chuo cha Africa Graduate University yaliyofanyika Dar es Salaam jana.
 Askofu Dk. Godfrey Mallasy wa Kanisa la Tanzania Fellowship of Churches, akielezea kazi mbalimbali alizofanya kabla ya kutunukiwa tuzo hiyo.

Picha 22: JINSI WACHIMBAJI 15 WALIOFUNIKWA UDONGO MGODINI GEITA WALIVYOOKOLEWA WAKIWA HAI


Mungu Mkubwa!! Ndivyo unaweza kusema...Hatimaye wachimbaji wa madini 15 waliokuwa wamefunikwa na udongo katika mgodi wa dhahabu wa RZ Union mkoani Geita wameokolewa wakiwa hai na wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Geita.

KAMPENI KUCHEZA OLIMPIKI 2020 KUZINDULIWA KESHO


Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Omari; Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa kushirikiana na Makamu Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau kesho Jumatatu Januari 30, kwa pamoja watazindua kampeni maalumu za kuifanikisha Tanzania kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan.

Saturday, January 28, 2017

INTER SCHOOL DEBATE COMPETITION 2017 YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM



Wanafunzi mbalimbali wa shule za Seciondaruy jana walipata nafasi ya kushiriki katika mashiundano makubwa ya Interschool Debate Compitition yaliyofanyika Jijini Dar es salaam katika Viwanja vya sabasaba ambapo katika mashindano hayo wanafunzi hao walikuwa na nafasi ya kuchangamsha Bongo zao kwa Kuchangia Mada mbalimbali huku washindi wakijinyakulia Zawadi mbalimbali zikiwemo Vitabu kwa ajili ya masomo yao
Akizungumza na Mtandao Huu wa HABARI24 BLOG Mwanzilishi  na Mwaandaji wa mashindano hayo Bwana Shukuru Ngongoje ameeleza kuwa mashindano haya yanalenga kuwajenga wanafunzi wa Tanzania hususani wa shule za Secondary katika kujiamini na kuwa na uwezo wa Kutoa hoja na kukubali hoja jambo ambalo litawasaidia hata baada ya maisha ya uwanafunzi kwa kuwa dunia ya sasa imekuwa ikihitaji wanafunzi ambao wanauwezo wa kujieleza na kutoa hoja zenye nguvu.

Amezitaja shule ambazo zilishindanishwa jana katika INTERSCHOOL DEBATE COMPITATION kuwa ni Tuisiime Secondary school,Jitegemee Secndary,St Maria Salome,Mwandege Boys,Gome secondary,Kibasila Secondary ambapo washindi watatu wa Juu ambao ni Best Speaker wakiondoka na Zawadi kedekede yakiwemo madaftari kwa ajili ya masomo yao mashuleni.

Mashindano hayo yamepewa Nguvu na Masumini Printways and stationary, pamoja na Channel Ten na magic Fm.
PICHA ZAIDI BONYEZA CHINI

MADIWANI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI WATOA ZAWADI KWA WAGONJWA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA KILIMANJARO,MAWENZI.




Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakiwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro,Maawenzi wakiwa  wamebeba zawadi mbalimbali kwa ajili ya kutoa kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo