HISPANIA imeitoa Italia katika Kombe la Mabara kwa ushindi wa matuta wa 7-6 mjini Fortaleza, kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 katika mchezo wa Nusu Fainali usiku huu.
Wataliano walifungwa na Waspanyola katika Fainali ya Euro mwaka jana wameshindwa kulipa kisasi na sasa Fainali ya michuano hiyo mwaka huu Jumapili Uwanja wa Maracana, itawakutanisha wenyeji La Roja na Brazil wenyeji.
Leonardo Bonucci wa Italia alikosa moja ya penalti 14 na Jesus Navas akaweka nyavuni mkwaju wa mwisho na kuipeleka Hispania Fainali.

Ni tishio: Hispania wametinga Fainali ya Kombe la Mabara kwa kuifunga Italia kwa penalti mjini Fortaleza

Ushindi wa mbinde: Hispania wakishangilia 7-6 na sasa watamenyana na Brazil

Maumivu: Italia wameng'oka
Si zaidi ya mwaka uliopita, Italia walipigwa 4-0 mjini Kiev, lakini The Azzurri waliwasili Fortaleza wakiamini kisasi kinawezekana, ingawa haikuwa hivyo.
Mikwaju ya penalti; Jesus Navas alifunga a ushindi na kufanya 7-6 , baada ya Leonardo Bonucci mkwaju wake kuota mbawa.
Wengine wote waliotangulia walifunga; upande wa Hispania ni Sergio Busquets, Juan Manuel Mata, Sergio Ramos, Gerard Pique, Andries Iniesta na Hernandez Xavi.
Italia ni Riccardo Montolivo, Andrea Pirlo, Sebastian Giovinco, Daniele De Rossi, Alberto Aquilani na Antonio Candreva.
Kikosi cha Hispania kilikuwa: Casillas, Arbeloa, Sergio Ramos, Pique, Jordi Alba, Xavi, Busquets, Iniesta, Pedro/Mata dk79, Torres/Javi Martinez dk94 na Silva/Jesus Navas dk52.
Italia: Buffon, Maggio, Bonucci, Barzagli/Montolivo dk45,Chiellini, Candreva, De Rossi, Pirlo, Marchisio/Aquilani dk79, Giaccherini na Gilardino/Giovinco dk91.
Anakosaaa: Leonardo Bonucci mkwaju wake uliota mbawa

Ya ushindi: Jesus Navas alifunga ya mwisho, chini anashangilia

Shakira alikuwapo jukwaani Fortaleza

Hii ni kwa ajili yako: Pique akishangilia ushindi wa Hispania
Shakira jukwaani

Shakira alikutana na Rais wa FIFA, Sepp Blatter katika eneo la VIP uwanjani

Shakira akimuangalia mpenzi wake Pique akiichezea Hispania

Dakika 120 ziliisha 0-0

Giorgio Chiellini wa Italia akijaribu kupiga kichwa katikati ya Sergio Ramos na Gerard Pique

Jitihada: Fernando Torres alifumua shuti lililopanguliwa Gianluigi Buffon

Anateleza: Christian Maggio alikaribia kumtungua kipa wa Hispania, Iker Casillas

David Silva akipasua

Andres Iniesta alimtungua Buffon kwa penalti