Sunday, April 30, 2017

MH. MWAKYEMBE KUZINDUA KITABU CHA COLOR OF LIFE DAR ES SALAAM

Waziri wa sanaa utamaduni na michezo MH Harrison Mwakyembe amezindua kitabu kilichobeba jina la THE COLOR OF LIFE kilichoandikwa na muandishi wa kitanzania Ritha M. Tarimo. 

Uzinduzi huo umefanyika kwenye hotel ya HYATT REGENCY jijini dar es salaam tarehe 30 ya mwezi march 2017. MH. Mwakyembe aliweza kupongeza jitihada za dhati zilizofanywa na dada huyo na kusema kuwa yeye ni shujaa na ni mfano wa kuigwa na jamii.  

Alisema  ni ngumu sana kwa nchi kama yetu ya Tanzania ambayo vijana wake wengi wameweka akili zao kwenye mitandao kuweza kujitokeza mtu kuandika kitabu. sisi kama viongozi  inabidi tumpe moyo na kuweza kurudisha utamaduni wa zamani wa kusoma vitabu “Kwani leo hii ukienda maktaba ukiona vijana wapo wengi jua kuna mtihani karibu” alisema . 

Aliongezea kuwa amekisoma kitabu hicho japo sio mpaka mwisho lakini akuona makosa  na kimeandikwa vizuri. Muandishi amejaribu  kuwatia moyo vijana kuwa wanapotafuta kitu wasichoke mpaka wakipate. Na hii itafanya nchi yetu kusifika kuwa hata sisi tunawez kuandika vitabu vyetu kwa kiingereza.

WAZIRI WA SANAA UTAMADUNI NA MICHEZO DKT HARRISON MWAKYEMBE AKIONGEA NA  WAGENI WAALIKWA HYATT REGENCY DAR ES SALAAM

Ritha Tarimo ambaye ni mtunzi wa kitabu hicho alisema yeye kwa nafasi yake alihitaji kutengeneza historia kupitia uandishi wa vitabu kama ilivyo kwa wengine walivyoweza kuweka nguvu kwenye muziki, mpira, siasa nk. Na sababu kubwa iliyomfanya kuandika kitabu hicho ni kuweza kuwasaidia wanafunzi ngazi ya sekondari, vyuoni ili waweze kugundua mapungufu yake ili na wao waje kuwa waandishi wazuri zaidi yake . Lakini pia aliweza kuona ni vyema kutumia lugha ya kiingereza kwa kuwa shule zote kuna somo la hilo. Na vitabu vingi vinavyofundishiwa ni vya kutoka nje ambao waandishi wake ni watu wa mataifa mengine. Ivyo basi yeye aliamua kujikita huko kuweza kuwapa moyo waandishi wengine wa kitanzania waweze kufanya kama yeye alivofanya ili taifa liweze kupata vitabu vitakavyotumika kwenye mitaala ya shule zetu.

RITHA M. TARIMO AKITOA UFAFANUZI JUU YA KITABU CHAKE KINACHOZINDULIWA NA WAZIRI MWAKYEMBE

Lakini pia aliweza kumshukuru MH. Halisoni mwakyembe kwa kuweza kukubali wito wake wa kuhudhulia kwenye tafrija hiyo na kuweza kupongeza kile alichokifanya. Na kumuahidi kununua nakala kadhaa  za  kazi yake.  kwenda kuwaonyesha na viongozi wenzake wa ngazi ya juu kama waziri wa elimu na wengine ili kuweza kuwapa motisha vijana wengine wenye vipaji kama vyake. pia aliweza kuishukuru familia yake pamoja na marafiki kwa mchango wao wa dhati wa kimawazo hata kiuchumi kwa kuweza kufanikisha kwa uzinduzi huo.

MH. HARRISON MWAKYEMBE AKIKATA UTEPE KUZINDUA RASMI KITABU CHA THE COLOR OF LIFE

BAADA YA KUKATA UTEPE MH. MWAKYEMBE NA RITHA TARIMO WAKIONYESHA WAGENI WAALIKWA KITABU KILICHOZINDULIWA

PICHA YA PAMOJA BAADA YA TAFRIJA KUISHA

PICHA/STORY NA MUANDISHI WETU VICENT MACHA.

HII ORODHA NZIMA YA WATUMISHI WENYE VETI FEKI HII HAPA

Kama kawaida yetu Msumbanews.com ni kukupa taarifa pindi zinapojiri tumekuweke hapo chini orodha yenye majina ya watumishi wenye vyeti feki TANZANIA.
WAFANYAKAZI WA HALMASHAURI WENYE VYETI FEKI   
<<BONYEZA HAPA>>
 
KWA WAFANYAKAZI WA TAASISI ZA SERIKALI MFANO,UDSM 
 >>BONYEZA HAPA<<

Burudani za Castle Lite Unlocks zahamia La Chaz Bar Sinza Mori




Sakata la Wafanyakazi Hewa.ACT WAZALENDO watoa neno lao

Juzi tarehe 27 Aprili 2017, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mh. Angela Kairuki alikabidhi rasmi Ripoti ya zoezi la Uhakiki wa Vyeti ambapo iliripotiwa kuwa jumla ya watumishi 9932 wanatumia vyeti feki.

Chama cha ACT Wazalendo kinaunga mkono uamuzi wa serikali kuwachukulia hatua watumishi wote wa umma waliobainika kutumia vyeti feki ikiwemo kuwafukuza kazi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

 Bila shaka hatua hii itapanda mbegu ya uwajibikaji, kuchochea uadilifu na kuhakikisha uweledi kwenye utumishi wa umma.

Mbali na kupongeza, yapo masuala kadhaa yaliyoibuka kwenye zoezi hilo ambayo tunadhani hayakwenda sawasawa na hivyo basi sisi kwa nafasi yetu tunao wajibu wa kuyakemea ili kuufanya mchakato huu uende kwa haki:

Mosi, kauli ya Mh. Rais kuwasamehe wale wataojiondosha kazini wenyewe na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na wale wataoendelea kubaki kwenye nafasi zao ni kinyume cha sheria na katiba ya nchi.

 Kisheria Rais hana mamlaka ya kumsamehe mtu anayetuhumiwa kufanya kosa la jinai iwapo mtu huyo hajafikishwa kwenye vyombo vya sheria na kuhukumiwa.

Madaraka pekee aliyonayo . Rais ni kutoa Msamaha kwa wafungwa wanaotumikia kifungo (President's Prerogative of Mercy) kama alivyofanya hivi karibuni kwenye Sherehe za Muungano.

 Iwapo tutaacha hulka ya viongozi kuchukua hatua wapendavyo hata kama kwa kusigina sheria za nchi basi tujue wazi tunalipeleka taifa kwenye "Utawala wa Mtu Binafsi" badala ya "Utawala wa Sheria".

Pili, madai ya Waziri Kairuki kuwa mchakato wa uhakiki wa vyeti haujawagusa wanasiasa na wateule wa Mh. Rais kwa sababu cheti si sifa ya kupatikana kwao unapotosha mantiki ya zoezi zima na kuweka upendeleo wa dhahiri.

Ikumbukwe kuwa msingi wa zoezi hili ni kuhakikisha kuwa taifa linabaki na watumishi wenye sifa. Waziri Kairuki anasema kuwa sifa pekee ya Kikatiba ya Viongozi wa kisiasa ni kuwa wajue kusoma na kuandika. Jambo ambalo Waziri Kairuki hakutaka kujiuliza ni kuwa iwapo viongozi wa kisiasa watathibitika kughushi vyeti ambalo ni kosa la jinai haitawaondolea sifa yao ya uongozi.

 Kama Waziri mwenye dhamana ya utawala bora hakuona kuwa uhakiki wa vyeti kwa viongozi wa kisiasa na wateule wa . Rais kama vile Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kungehakikisha kuwa viongozi hao wanakwenda sambamba na viapo na matakwa ya kimaadili?

Uamuzi huu wa kutowagusa viongozi wa kisiasa katika zoezi hili la uhakiki wa vyeti ni ushahidi wa dhahiri kabisa wa jinsi serikali inavyohaha kuwalinda baadhi ya wateule wa Mh. Rais na wanasiasa ambao wametuhumiwa na umma kwa makosa ya kughushi vyeti.
ACT Wazalendo tunatoa rai kwa serikali kutanua mawanda ya zoezi hili liguse  viongozi wa kisiasa wa CCM na vyama vya upinzani.

Ado Shaibu,

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano.
30 Aprili 2017

ACT WAZALENDO KUADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA KWA CHAMA HICHO

Maadhimisho ya Siku ya Kuzaliwa Chama cha ACT Wazalendo:

Tarehe 05 Mei 2017, Chama cha ACT Wazalendo kitatimiza miaka mitatu tangu kilipopata usajili wa kudumu tarehe 05 Mei 2014 wakati huo kikiitwa ACT Tanzania.

Maadhimisho ya miaka mitatu ya kuzaliwa kwa ACT Wazalendo yatafanyika Kahama Mjini Mkoani Shinyanga tarehe 05 Mei 2017.

DC Mjema: Daladala, bajaji zisizokuwa na 'dustbin' kutozwa faini

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewaagiza madereva wa daladala na bajaji kuhakikisha vyombo vyao vya usafiri vinakuwa na kikapu cha kuwekea taka, vinginevyo watatozwa faini ya uchafuzi wa mazingira.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika kufanya kwa vitendo kampeni ya usafi ya kila jumamosi ya mwisho wa mwezi DC Mjema alitembelea kituo cha daladala cha stesheni na kukuta magari mengi ya abiria hayana vikapo vya taka, ambapo wameyatoza takribani magari saba  kiasi cha shilingi 50000 kwa kila moja katika eneo hilo.
Huku kwa upande wa madereva wa bajaji wanaopaki eneo la Soko la Samaki Feri wamepewa onyo na kuombwa kufanya hivyo mara moja kabla hawajachuliwa hatua na mamlaka husika ya Halmashauri hiyo ya Ilala.
Katika hatua nyingine DC Mjema amewataka wafanyabishara wadogo wanaopanga bidhaa zao kandokando ya barabara iliyopo jirani na soko la samaki Feri kujiandikisha kwa afisa mtendaji na kuondoka eneo hilo mara moja, huku Halmashauri hiyo itawapangia maeneo ya biashara ndani ya soko hilo la samaki la Feri.

Saturday, April 29, 2017

Rais Magufuli ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Kilimanjaro


 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Kmnda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Hamisi Issa alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongiozana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Rais wa TUCTA Bw. Tumaini Nyamhokwa alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu Mhe. Kassim majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aiiongiozana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wanahabari alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wana UVCCM alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo leo Jumamosi Aprili 29, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi wa Bomang'ombe Wilaya ya Hai waliomsimamisha kwa muda wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi wa Bomang'ombe Wilaya ya Hai waliomsimamisha kwa muda wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza changamioto za wananchi wa Kwa Sadala Wilaya ya Hai waliomsimamisha kwa muda wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017
 Kijana akiwa kabebwa mgongoni akirekodi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi wa Karanga Wilaya ya Moshi mjini waliomsimamisha kwa muda wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi wa Karanga Wilaya ya Moshi mjini waliomsimamisha kwa muda wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017
 
 
 
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi wa Karanga Wilaya ya Moshi mjini waliomsimamisha kwa muda wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiagana na wananchi wa Karanga Wilaya ya Moshi mjini waliomsimamisha kwa muda wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi wa Karanga Wilaya ya Moshi mjini waliomsimamisha kwa muda wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017
 
 
 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maagizo wa kutotoza ushuru wachuuzi kwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Hai Bw. Yohana Sintoo wakati akiongea na wananchi wa Kwa Sadala waliomsimamisha kwa muda wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maagizo wa kutotoza ushuru wachuuzi kwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Hai Bw. Yohana Sintoo wakati akiongea na wananchi wa Kwa Sadala waliomsimamisha kwa muda wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017
 
 
  Mbunge Mstaafu na aliyekuwa Mkuu wa Sekondari ya Weruweru, Dk Maria Kamm akimshangilia Rais Magufuli alipoongea na wananchi wa Karanga
 Mbunge Mstaafu na aliyekuwa Mkuu wa Sekondari ya Weruweru, Dk Maria Kamm akisalimiana na Rais Magufuli aliposimamishwa kuongea na wananchi wa Karanga
 Rais magufuli akiwa na Mbunge Mstaafu na aliyekuwa Mkuu wa Sekondari ya Weruweru, Dk Maria Kamm eneo la Karanga
 Rais magufuli akiwa na Mbunge Mstaafu na aliyekuwa Mkuu wa Sekondari ya Weruweru, Dk Maria Kamm akisalimiana na wanafunzi
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi wa Karanga Wilaya ya Moshi mjini 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi wa Karanga Wilaya ya Moshi mjini  
 Wananchi wa Kibololoni wakimshangilia Rais Magufuli
  Wananchi wa Kibololoni wakimshangilia Rais Magufuli
 Rais Dkt. Magufuli akiongea na Wananchi wa Kibololoni.