Tuesday, November 13, 2012
MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amependekeza kuvunjwa kwa Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwani badala yake kupambananayo inaipalilia.
Akifungua tawi ya Chadema Kata za Katesh linalopakana na ofisi za Takukuru Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara juzi, Mbowe alisema taasisi hiyo imeshindwa kazi.
Mbowe alisema Takukuru imeshindwa kudhibiti hata rushwa ya wazi ndani ya CCM kwenye chaguzi ambazo zilifanyika hivi karibuni.
“Hakuna ambaye hakujua rushwa ndani na CCM na jinsi ambavyo imeathiri chama hicho, lakini Takukuru wameshindwa kupambana na rushwa hiyo badala yake wanailea,” alisema Mbowe.
Alisema Rais Jakaya Kikwete ambaye anasimamia Takukuru iliyopo kwenye wizara yake, ameshindwa kuibana ndiyo sababu hata yeye amekuwa akilalamika.
Pia, Mbowe alifungua matawi kata za Endasaki na Ganana, alisema kutokana na Takukuru kushindwa kupambana na rushwa, isipovunjwa chama hicho kikiingia madarakani kitawatimua watendaji wote wa taasisi hiyo ili wafanye kazi nyingine.
Alisema Takukuru imeshindwa hata kusaidia kurejesha mabilioni ya fedha za Watanzania ambayo yamefishwa nchini Uswis.
“Hawa Takukuru walipaswa kuanza kufanya uchunguzi juu ya fedha hizo baada ya kupata taarifa na kusaidia taifa kuzipata, lakini wamekaa kimya,” alisema Mbowe.
Alisema kutokana na ukimya huo, ndiyo sababu Chadema kupitia Naibu Katibu Mkuu wake, Kabwe Zitto waliomba serikali kufanya uchunguzi na kutoa taarifa bungeni juu ya walioficha fedha na utaratibu wa kuzirejesha.
“Bunge lijalo, kama wasipoleta taarifa ya maana juu ya fedha za Uswis tunajua la kufanya, nadhani mmeona jinsi hoja hii ilivyoungwa mkono na watu wengi,”alisema Mbowe.
Awali, Mbowe alizitaka ofisi hizo za Chadema, alizofungua kuwa kimbilio la wanyonge kutoa kero zao na kusaidiwa badala ya kuwa maeneo ya kukaa viongozi pekee
RIPOTI KAMILI YA UCHSGUZI WA CCM DODOMA HII HAPA
Mwenyekiti
Kura zilizopigwa 2397
Kura zilizoharibika 0
Kura za HALli 2397
Makamu wa Tanzania Bara
Kura zilizopigwa 2397
Kura zilizoharibika 0
Kura za HALli 2397
Malamu wa Zanzibar
Kura zilizopigwa 2397
Kura zilizoharibika 0
Kura za HALli 2397
WAKATI matokeo ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), yakiwa yamevuja baadhi ya wapambe wa wagombea walioshinda wameanza kusherehekea, huku wengine wakitambiana.
Hata hivyo, matokeo hayo yamekuwa machungu kwa baadhi ya vigogo walioanguka wakiwamo mawaziri, wabunge na watu maarufu.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuunda sekretarieti mpya baada ya uchaguzi wa mwenyekiti na makamu mwenyekiti Bara na Zanzibar utakaofanyika leo.
Kwa upande wa Zanzibar,
Kura zilizopigwa 2268
Kura zilizoharibika 55
Kura za HALli 2213
matokeo hayo yanaonyesha kuwa walioshinda ni pamoja na Mbunge wa Uzini, Mohamed Seif Khatib; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Ali Mwinyi 1576, Waziri wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee, Abdulhakim Chasama na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha 1603.
Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan 1525, Khadija Hassan Aboud 1625, Bhaguanji Mansuria, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa 1850 na Khamis Mbeto.
Watu maarufu walioangukia pua katika uchaguzi huo ni Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Abdallah Juma Sadallah, mtoto wa Rais Mstaafu, Abdallah Mwinyi ambaye pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Mbunge wa Viti Maalumu, Kidawa Salehe na Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Abdisalaam Issa Khatib.
Walioshinda Bara
Kura Zilizopigwa 2389
Kura Zilizoharibika 52
Kura halali 2337
Majina ya wajumbe wa Nec walioshinda bara na kura walizopata katika mabano ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira aliyeongoza kundi hilo kwa kupata kura 2,135, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (2,093), Mwekahazina wa CCM, Mwigulu Nchemba (2,012), na Katibu wa UVCCM, Martine Shigela (1,824).
Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi (1,805), Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe (1,455), Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo (1,414), Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome (1,207), Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (1,174) pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Fenela Mukangara (984).
Wakati walioshinda Bara na wapambe wao wakitambiana, majina makubwa yaliyoanguka katika uchaguzi huo ni pamoja ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, Mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama, Richard Hiza Tambwe na Mbunge wa zamani wa Muleba Kaskazini, Ruth Msafiri.
Wednesday, November 7, 2012
RATIBA YA MICHEZO YA JUMAMOSI lig kuu england
RATIBA YA MICHEZO YA JUMAMOSI NOV 10 YA LIGI YA ENGLAND
Everton v Sunderland Goodison Park 17:00
Southampton v Swansea St. Mary's Stadium 17:00
Stoke v QPR Britannia Stadium 17:00
Reading v Norwich Madejski Stadium 17:00
Wigan v West Brom The DW Stadium 17:00
Arsenal v Fulham Emirates Stadium 17:00
Aston Villa v Man Utd Villa Park 19:30
Arsenal v Fulham Emirates Stadium 17:00
Aston Villa v Man Utd Villa Park 19:30
Subscribe to:
Posts (Atom)