Tuesday, November 13, 2012
RIPOTI KAMILI YA UCHSGUZI WA CCM DODOMA HII HAPA
Mwenyekiti
Kura zilizopigwa 2397
Kura zilizoharibika 0
Kura za HALli 2397
Makamu wa Tanzania Bara
Kura zilizopigwa 2397
Kura zilizoharibika 0
Kura za HALli 2397
Malamu wa Zanzibar
Kura zilizopigwa 2397
Kura zilizoharibika 0
Kura za HALli 2397
WAKATI matokeo ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), yakiwa yamevuja baadhi ya wapambe wa wagombea walioshinda wameanza kusherehekea, huku wengine wakitambiana.
Hata hivyo, matokeo hayo yamekuwa machungu kwa baadhi ya vigogo walioanguka wakiwamo mawaziri, wabunge na watu maarufu.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuunda sekretarieti mpya baada ya uchaguzi wa mwenyekiti na makamu mwenyekiti Bara na Zanzibar utakaofanyika leo.
Kwa upande wa Zanzibar,
Kura zilizopigwa 2268
Kura zilizoharibika 55
Kura za HALli 2213
matokeo hayo yanaonyesha kuwa walioshinda ni pamoja na Mbunge wa Uzini, Mohamed Seif Khatib; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Ali Mwinyi 1576, Waziri wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee, Abdulhakim Chasama na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha 1603.
Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan 1525, Khadija Hassan Aboud 1625, Bhaguanji Mansuria, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa 1850 na Khamis Mbeto.
Watu maarufu walioangukia pua katika uchaguzi huo ni Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Abdallah Juma Sadallah, mtoto wa Rais Mstaafu, Abdallah Mwinyi ambaye pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Mbunge wa Viti Maalumu, Kidawa Salehe na Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Abdisalaam Issa Khatib.
Walioshinda Bara
Kura Zilizopigwa 2389
Kura Zilizoharibika 52
Kura halali 2337
Majina ya wajumbe wa Nec walioshinda bara na kura walizopata katika mabano ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira aliyeongoza kundi hilo kwa kupata kura 2,135, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (2,093), Mwekahazina wa CCM, Mwigulu Nchemba (2,012), na Katibu wa UVCCM, Martine Shigela (1,824).
Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi (1,805), Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe (1,455), Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo (1,414), Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome (1,207), Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (1,174) pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Fenela Mukangara (984).
Wakati walioshinda Bara na wapambe wao wakitambiana, majina makubwa yaliyoanguka katika uchaguzi huo ni pamoja ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, Mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama, Richard Hiza Tambwe na Mbunge wa zamani wa Muleba Kaskazini, Ruth Msafiri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment