Kushuka kwa nidhamu,maadili mema na hofu ya mungu kwa wanafunzi nchini umetajwa kama moja kati ya vyanzo vikuu vya matokeo mabaya ya kidato cha nne yaliyotangazwa mwezi huu nchini ambayo zaidi ya asilimia 60 ya wanafunzi wamefeli
Hayo yamesemwa na mdau wa elimu ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa shule ya secondary ya CORNELIUS docta EMILI WOISO wakati akitoa maoni yake kwa waandishi wa habari juu ya kushuka huko kwa kiwango cha kufaulu
Docta WOISO amesema wadau wamekuwa wakitupa lawama kwa serikali na waalimu juu ya matokeo hayo na kuwasahau wanafunzi ambao ndio walengwa wa kwanza.amesema wanafunzi wengi wamekuwa hawana nidhamu ya masomo na hata kushindwa kuwaheshimu walimu wao
Ameongeza kuwa nidhamu ndio msingi mkubwa wa shule yoyote kufanya vizuri huku akitolea mfano shule mbalimbali zilizosimamia nidhamu na kufanya vizuri kama shule yake iliyofanikiwa kushika nafasi ya 11 mkoani dar es salaam
Aidha dacta WOISO amewashauri waazazi na walimu washirikiane kwa pamoja kuwasiimamia watoto wao juu ya suala la nidhamu jambo litakalowafanya waweze kufanya vizuri katika masomo yao
EM REPORTING
No comments:
Post a Comment