Mkuu wa Chuo Kikuu huria nchini Tanzania Prof, Tolly Mbwette akibadilishana Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano wa Kitaaluma baina ya chuo kikuu huria na Chuo kikuu cha Trimphant Collage-Widhoek Namibia. Anayepokea Mkataba ni Elizabeth Kiyangi Mkurugenzi Mtendaji wa Triumphant Collage. |
Vyuo vikuu nchini Tanzania vimeshauriwa kuhakikisha vinajitanua kimataifa katika kutoa elimu yake jambo ambalo limetajwa kuwa litasaidia wanafunzi wa Tanzania kujifunza mambo mapya katika nchi nyingine.
Hayo yamesemwa leo na mkuu wa chuo kikuu huria cha Tanzania Prf TOLLY MBWETTE wakati akisaini mkataba wa makubalioano ya ushirikiano na serikali ya Namibia kupitia chuo chake cha TRIUMPHANT COLLEGE mkataba wenye malengo ya kushirikiana kitaaluma baina ya vyuo hivyo viwili.
Prof, MBWTTE amesema kujitanua kimataifa ni jambo muhimu ambalo amesema moja kati ya faida zake kubwa ni kusaidia wanafunzi kupata elimu bora na yenye viwango vya kimataifa zaidi.
Aidha amesema chuo kikuu huria kimekuwa ni chuo kikuu cha kwanza kusaini mkataba wa kimataifa wa kusaidia katika elimu jambo ambalo amesema liafaa kuigwa kwa vyuo vingine ili visaidie katika kukuza elimu ya Tanzania.
Mkuu wa Chuo Kikuu huria nchini Tanzania Prof, Tolly Mbwette (kulia) pamoja na Elizabeth Kiyangi Mkurugenzi Mtendaji wa Triumphant Collage wakiweka sahihi kwenye Mkataba wa Kushirikiana kitaaluma Baina ya Vyuo hivyo viwili. |
No comments:
Post a Comment