Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Mtondoo akitoa hutuba wakati wa Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Kanda ya Mashariki iliyofanyika katika Wilaya yake ya Mafia,semina hiyo ilikuwa na lengo la kutoa elimu kwa wannchi wa Wilaya hiyo juu ya Haki na wajibu wa watumiaji wa huduma za Mawasiliano, katikati ni Mkurugenzi wa Watumiaji na watoa huduma za Mawasiliano Dk. Raymond Mfungahema,(Kulia ) Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mohamed Kimbule.
MAMLAKA ya Mawasiliano nchini, kanda ya mashariki imetoa rai kwa watumiaji wa mitandao ya simu za mkononi kuwa macho na wizi unaofanywa na watu wenye nia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, ambapo idadi kubwa ya wateja wa simu wamejikuta wakilalamikia wizi huo.
Mojawapo mwa udanganyifu ni pamoja na mmiliki wa simu kutumiwa ujumbe unahitaji kutuma fedha kwa ajili ya kulipia gharama za huduma kwa njia mtandao ili hali anayetumiwa fedha hizo hafahamiki.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Watumiaji na watoa huduma za Mawasiliano Dk. Raymond Mfungahema wakati alipokuwa akitoa mada ya kazi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mfia waliohudhuria katika Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Masharaiki
Afisa Utumishi Mkuu,Esuvatie Masinga katika Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Mashariki, iliyofanyika kisiwani Mafia.
Semina hiyo iliyofanyika Machi 7a mwaka huu iliwashirikisha wadau mbalimbalimbali wa mawasiliano wilayani Mafia, wakiwemo watendaji wa serikali wa ngazi ya kitongoji, kata na tarafa na wilaya.
Katika semina hiyo iliyohudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya Mafia, Sauda Mtondoo ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi,Masinga alisema, wizi wa mitandao ya simu ni changamoto iliyo mbele ya wateja ambayo inaweza ikakabiliwa kama kila mmoja atakuwa na ufahamu wa kubaini ujanja na mbinu zinazofanywa na wajanja wachache.
Alisema ili kukabiliana na mbinu na ujanja wa wachache hao, wamiliki wa simu za mkononi wanatakiwa kuwa macho ujumbe wowote unaozungumzia utumaji wa fedha iwe kwa njia ya ujumbe mfupi ama mawasiliano ya moja kwa ya simu wa watu wasiowajua.
Amesema,wateja wengi wamekuwa wakitumiwa ujumbe unaowataka watume fedha kwa watu wasiowajuwa wakiamini kuwa wanatuma fedha hizo kwa makampuni ya simu, jambo ambalo si kweli, kwani makampuni yote ya simu yana namba zao za utambulisho pindi wanapoendesha zoezi lolote la kihalali.
"Utakuta mmiliki wa simu ya mkononi anatumiwa ujumbe unaomtaka atume kiasi cha fedha kwa mtu asiyemjua, huku asitambue anatuma fedha hizo kwa ajili ya kulipia huduma gani. Hili ni tatizo lililo katika changamoto inayohitaji wateja kubaini aina hii ya wizi kwa njia ya mitandao ya simu" alisema Masinga.
Alisema, wateja wa simu wana wajibu wa kubaini ujanja wa watu wachache kwa kutilia mashaka ujumbe ama simu yoyote inayoelekezwa kwao na inayohitaji fedha kwa kuchukua hatua ya kuwasiliana na makampuni ya simu husika kubaini kama kuna kuna mahitaji ya namna hiyo.
Katika hotuba yake, Mkuu wa Wilaya Mafia, Sauda Mtondoo aliiomba TCRA kutilia mkazo suala la uelimishaji umma pindi kunapotokea changamoto za matumizi ya huduma mbalimbali zilizo chini ya mamlaka ili kuwaongezea uelewa watumiaji.
Alisema, elimu kwa umma juu ya huduma ngeni inawasaidia kuwaondolea usumbufu wateja hivyo kwenda na kasi ya utandawazi na kuwaondolea usumbufu ambao unaweza ukawapa mwanya wajanja wachache kunufaika.
Aidha alipongeza hatua ya TCRA kutoa elimu ya matumizi ya ving'amuzi kwa muda mwafaka, jambo lililosaidia kuwaondolea wateja usumbufu pindi mamlaka hiyo ilipotangaza hatua ya Tanzania kuacha kuanza kutumia mfumo wa kidijitali kwa baadhi ya mikoa nchini.
"Ni jambo la kufurahisha kwamba TCRA imetoa elimu kwa umma kuhusu namna ya kuweka antena hizo ili picha ziweze kuonekana katika maana halisi ya dijitali.Vilevile faraja kusikia kuwa mamlaka inawasiliana na watoa huduma za kurusha matangazo ya dijitali ili waweke vizuri mitambo yao na kuongeza mitambo kule ambako haipo ili matangazo yawafikie watazamaji wengi" ilisema Mkuu huyo wa wilaya.
Pia aliitaka mamlaka kuyabana makampuni ya mawasiliano ya simu inayobuni utaratibu wa kujipatia fedha kwa njia za kuwataka watumiaji wa simu za mkononi kuingia katika utumaji wa fedha kwa njia ya ujumbe mfupi ili hali huduma hiyo siyo lazika kwa wateja.
Alisema hatua ya watumiaji kukatwa fedha kwa huduma isiyo ya lazima humuongezea mzigo mteja na kuwayafaidisha makampuni ya simu jambo linazua manung’uniko yasiyo ya lazima.
Aliitaja mfano wa huduma hizo za kuchangia fedha ni pamoja na nyimbo za miito ya simu ambayo haina ulazima kwa mteja hivyo kuwaagiza wachangie bila ridhaa ya mteja wa simu ya mkononi ni hatua inayowaongezea mzigo wamiliki wa simu za mkononi.
Kwa upande mwingine washiriki wa semina hiyo walipata mafunzo ya mfumo wa anuani za makazi na Posta Kodi iliyotolewa na Patrice Lumumba ambaye aliwataka wananchi wa wialya hiyo kuwa makini na kujua anuni za makazi yao.
HABARI KWA HISANI YA MJENGWA BLOG
No comments:
Post a Comment