Wednesday, April 10, 2013
KAMPUNI YA STARTIMES KUBORESHA HUDUMA ZAKE
Wakati ikiwa ni mwaka wa kwanza baada ya Tanzania kuingia rasmi katika mfumo wa matangazo wa digital mfumo huo umeanza kuimarika hatua kwa hatua baada ya kampuni inayotoa huduma hiyo ya STAR TIMES kutangaza mikakati yake mipya ya kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora kutoka kwao
Akitangaza mikakati hiyo meneja wa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo bw SULEMAN DISOMILE amesema kampuni hiyo ina mitambo miwili ya kurushia matangazo huku akiitaja kuwa mmoja unapatikana kisarawe na mwingine makongo na kuwaomba wateja wake ambao wengi wamekuwa wakilalamika kutopata matangazo hayo kwa ufasaha kuwa waelekezee antenna zao katika maeneo hayo ambayo mitambo hiyo inapatikana. Katika hatua nyingine bw SULEMAN ametambulisha bidhaa mpya za kamuni hiyo ambazo ni simu na television za kwenye magari ambazo zina huduma ya kujionea tv zinazopatikana katika kingamuzi chao,na kusema kuwa hiyo ni kampuni ya kwanza kufanya hivyo.Ameongeza kuwa siku zote kampuni hiyo nia yao ni kutoa bidhaa zenye ubora wa kiwango kwa bei nafuu zenye kudumu kwa muda mrefu na zenye kuridhisha na kukidhi mahitaji ya watanzania walio wengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment