Hakuna tatizo kwa redio kutopiga nyimbo ya msanii yoyote kwan redio hujiendesha yenyewe. Magic Fm imekaa mdaa mrefu bila kupiga nyimbo za diamond na hata east Africa redio ilikaa mdaa mrefu bila kupiga nyimbo ya ray c, amesema ruge mutahaba
Akizungumza leo asubuhi katka kipindi cha power breakfast Mkurugenzi wa Clouds Entertainment RugeMutahaba amezungumzia suala ambalo limekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii na midomoni mwa watu kuhusiana na LADY JAY DEE kutoa kashfa nzito.
|
RugeMutahaba |
Ruge amesema nchi kama nchi tunatakiwakujadili mambo ya msingi na siyo binafsi na kuwa kimya muda mrefu kutoongelea tatizo hili kwasababu halina maslaiya taifa inatakiwa tukae tumalize binafsi na hajui tatizo ni nini .
Clouds fm ni chombo binafsi iliyosajiliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania kwa kufuata Masharti tofauti na kuchagua vitu vyao kuwa ni Redio ya burudani na inapanga wao nyimbo za kupiga na sio mtu mwingine na KUSEMA WANAWEZA KUAMUA WASIPIGE NYIMBO YEYOTE YA BONGO FLEVA.
Pia Ruge amesema kila mtu mzuri akifanya kitu kizuri lazima kiwe na lawama na tatizo hili limeanza vipi yeye afahamu chochote .
Amesema wana record ya kupiga wimbo mpya wa jay dee mara 46 kwa hiyo haelewi kwanin anasema hwapigi nyimbo zake.
Ameongeza kuwa LADY JAY DEE anahofia band ya sky right ambayo inamilikiwa na SEBASTIAN NDEGE ambaeni mfanyakazi wa mwandamizi wa CLOUDS MEDIA GROUP.
“Sky rights imeanza kwa kuchukua wanamuziki toka bendi mbalimbali ikiwemo ya lady jay dee lakin sio chanzo cha kuigopa. So jay dee anatakiwa apelike makombora yake kwa sky rights sio kwangu” amesema Ruge
Aidha Ruge amesema kuwa muziki ni mchezo wa kupokezana vijiti na mtu uwezi tawala sku zote kwani sasa kuna watu wanakuja juu sana kama kina ommy dimpoz.
Kuhusu Lina na barnaba kutopiga show amesema kuwa tatizo ni hawakupatana vizuri kwenye suala la malipo.
Amesema kuwa clouds media group inafanya tamashamoja kwa mwaka kwa hiyo wanaosema kuwa wanawanyonya wasanii kwenye show wanatoa wapi ayo.
Ameongeza kuwa clouds media group huwazamini wasanii kila week kupiga show kwenye kumbi za bilcanas na maisha club.
LAD JAY DEE NAYE KUPITIA PAGE YAKE YA FACEBOOK KASEMA HAYAA.
|
LADY JAYDEE |
Kama mtakumbuka niliahidi kutoa awamu ya pili tar 15 au 17 May na ahadi ni deni..Japo naona mbali ila Nitafanya hivyo, bado nina mengi sana ya kuzungumza kuhusu Ruge na wenzake...Ile ilikuwa ni trailer tu, Movie ndio linaanza sasa #TeamAnaconda no surrender.
1 comment:
kaisha kimuziki huyu dada yetu
Post a Comment