Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeamua kumuachia huru Ramadhani Selemani Mussa ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya kukutwa na kichwa cha mtu.
Rama, ambaye muda wote huo alikuwa rumande gereza la Segerea akisota kusubiri hukumu yake, alikamatwa hospitali ya Muhimbili mwaka 2008 ambapo pia alikiri kuwa alikuwa na tabia ya kula nyama za watu ambayo amefundishwa kichawi toka alipokuwa mdogo.
Mahakama imemuachia huru kwasababu mtuhumiwa alitenda kosa hilo pasipo kuwa na akili timamu. Hata hivyo mahakama hiyo imetoa agizo la kuendelea kumuweka kijana huyo katika hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya akili, hospitali ya Isanga iliyopo Dodoma mpaka pale atakapona ndipo aruhusiwe kurudi mtaaani.habari kutoka karibu ndani
No comments:
Post a Comment