KOCHA Sir Alex Ferguson anajiandaa kuhitimisha miaka yake 27 ya kuifundisha Manchester United.
BIN ZUBEIRY inafahamu kupitia Sportsmail kwamba,
mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 71 anajiandaa kuuga umati wa
mashabiki Uwanja wa Old Trafford Jumapili baada ya mechi ya United dhidi
ya Swansea, wakati watakapokabidhiwa taji la ubingwa wa Ligi Kuu
England, hilo likiwa la 13 chini ya Ferguson.
Mazungumzo yanaendelea kumsaka mrithi wake na kocha wa Everton, David Moyes ni miongoni mwa wanaopewa nafasi.
Mtaalamu: Sir Alex Ferguson akishangilia taji la 13 la ubingwa wa Ligi Kuu England akiwa na Manchester United
MATAJI 49 YA FERGIE...
Sir Alex Ferguson ameshinda mataji 49 akiwa kocha mwenye mafanikio zaidi Uingereza...
ST MIRREN
Daraja la Kwanza Scotland (1): 1976-77.
ABERDEEN
Ligi Kuu Scotland (3): 1979-80, 1983-84, 1984-85.
Ligi Kuu Scotland (3): 1979-80, 1983-84, 1984-85.
Kombe la Scotland (4): 1981-82, 1982-83, 1983-84, 1985-86.
Kombe la Ligi Scotland (1): 1985-86.
Kombe la Washindi Ulaya(1): 1982-83.
Super Cup ya Ulaya (1): 1983.
MANCHESTER UNITED
Ligi Kuu England (13): 1992-93, 1993-94, 1995-96, 1996-97, 1998-99, 1999-2000, 2000-01, 2002-03, 2006-07, 2007-08, 2008-09, 2010-11, 2012-13.
Ligi Kuu England (13): 1992-93, 1993-94, 1995-96, 1996-97, 1998-99, 1999-2000, 2000-01, 2002-03, 2006-07, 2007-08, 2008-09, 2010-11, 2012-13.
Kombe la FA (5): 1989-90, 1993-94, 1995-96, 1998-99, 2003-04.
Kombe la Ligi Cup (4): 1991-92, 2005-06, 2008-09, 2009-10.
Ngao ya Jamii/Hisani (10): 1990 (shared), 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011.
Ligi ya Mabingwa Ulaya (2): 1998-99, 2007-08.
Kombe la Washindi Ulaya (1): 1990-91.
Super Cup ya Ulaya(1): 1991.
Kombe la Mabara(1): 1999.
Klabu Bingwa ya Dunia (1): 2008.
Mrithi wake? David Moyes ni miongoni mwa wanaotajwa kurithi mikoba ya Ferguson
Mkono wa mikoba? Kocha wa Everton, Moyes anaongoza katika mbio za kuwania siti inayaochwa wazi na Ferguson Old Trafford
Mafanikio hadi Ulaya: Fergie akiinua taji la Ligi ya Mabingwa mjini Moscow mwaka 2008
Tuzo mbili: Fergie, akiwa ameshika tuzo ya mafanikio ya muda mrefu ya BBC na David Beckham mwaka 2001
No comments:
Post a Comment