KLABU ya Manchester United inajiandaa kumtangaza David Moyes Alhamisi jioni kuwa kocha wake mpya.
Ferguson
asubuhi ya Jumatano alitangaza kuhitimisha miaka yake 27 ya kufanya
kazi Old Trafford na ataaga katika mchezo dhidi ya West Brom Mei 19.
BIN ZUBEIRY kupitia Sportsmail inafahamu
kwamba United itamtangaza rasmi mrithi wa Sir Alex Ferguson baada ya
kufikia naye makubaliano Na hiyo inamaanisha kwamba, mtu huyo hatakuwa
Jose Mourinho, licha ya mazungumzo yake na Chelsea kubuma wiki hii.
Mjumbe
wa bodi ya United, Sir Bobby Charlton - inaaminika anavutiwa zaidi na
Moyes kutokana na kazi yake nzuri Everton na namna anavyojitolea katika
kutengeneza timu. Mscotland huyo alikutana na Mwenyekiti wa Everton,
Bill Kenwright ofisini kwake mjini London jioni ya jana.
Nichukue kama wewe unaweza: David Moyes akiwa mwenye furaha wakati anatoka ofisini kwa Bill Kenwright' jana
Mlango mmoja umefungwa: David Moyes akiwasili na kuondoka ofisini kwa Bill Kenwright
Enlarge
Anakwenda
United? David Moyes (kulia) akiondoka Uwanja wa mazoezi wa Everton,
Finch Farm jana akiendeshwa na mdogo wa wakala wake, Kenny
Mabosi
wa Old Trafford wanaamini kwamba kocha huyo wa Everton anaweza kurithi
nafasi itakayoachwa wazi na Fergie Mwisho wa msimu.
Moyes anamaliza mkataba wake na Everton mwisho wa msimu huu na bado hakuna makubaliano ya mkataba mpya ndani ya Goodison Park.
Moyes,
(50), aliwahi kusema kwamba anataka kusubiri mpaka mwisho wa msimu
kabla ya kuamua kama anaongeza mkataba Goodison Park alipokaa kwa miaka
12 ama la.
Atakuwa na furaha kufanya kazi na Ferguson, ambaye amepata shavu kwenye Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo.
Moyes
anapewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya Ferguson kutokana na
kutokutetereka akiwa na Everton na mapenzi yake kwa klabu hiyo.
Tabia yake ya kukuza vipaji ni kitu kingine ambacho kinampa pointi za juu kwenye mchakato huu wa kumpata mbadala wa Ferguson.
Mkuu
wa Manchester United, David Gill alikiambia kituo cha MUTV: “Tulijua
siku hii itakuaja na tumekuwa tukijiandaa kwa hilo. Bodi itasikiliza
maoni ya Sir Alex na Sir Bobby (Charlton) kwa maoni yao.”
Charlton aliongelea kuhusu kukerwa na uvumi kwamba Mourinho atamrithi Ferguson.
Alisema:
“Mourinho ni kocha mzuro, lakini hili ndilo naweza kulisema, anaongea
sana kitu ambacho sikipendi. Japokuwa ni kocha mzuri.”
Hatahivyo,
Gill alisema kwamba mtu atakaye mrithi Ferguson lazima awe na uzoefu wa
kutosha wa soka la England na Ulaya, hili linaweza kumnyima nafasi
Moyes. Moyes anauzoefu mdogo sana kwenye soka la Ulaya.
Mourinho, ambaye anatarajiwa kuondoka Real Madrid wakati wa kiangazi amekuwa akihusishwa sana na kurudi Chelsea.
Ujio
wake Stamford Bridge unaonekana kugonga mwamba baada ta Roman
Abramovich kukataa kumlipia ada yake ya kuvunja mkataba na Real Madrid
na malipo ya wafuasi wa Mourinho.
Abramovich
alimlipa Mourinho na wafuasi wake kiasi cha pauni milioni 17 baada ya
kuwatimua mwaka 2006, na sasa hivi inasemekana ilikumchukua Mourinho
kutoka Madrid ni lazima kumlipia kiasi cha pauni milioni 20, lakini dau
hilo linakaribisha mazungumzo.
Mourinho
bado anapewa nafasi kubwa ya kumrithi, Rafa Benitez, Stamford Bridge,
lakini Chelsea wanataka kusimamia zaidi usajili wa wachezaji, kuliko
ilivyokuwa mara ya kwanza alipotua kutoka Porto mwaka 2004.
Moyes,
Mscotland mwenzake Ferguson amekuwa akiiongoza Everton kwa zaidi ya
miaka 10 na ni kocha wa tatu kwa kukaa muda mrefu zaidi kwenye Ligi Kuu
England.
Akiwa Everton hajatetereka na amekuwa na mapenzi ya kweli na timu hiyo.
Hata
hivyo kuna maswali juu ya ubora wake kuongoza timu kubwa – kikosi chake
cha Everton hakijawahi kuzifunga Manchester United, Chelsea, Arsenal au
Liverpool ugenini licha ya kujaribu mara 44.
Lakini akiwa na bajeti kubwa kwenye timu kama Man United, ni wazi Moyes anauwezo wa kufanya makubwa Old Trafford.
Yuko
tayari kufanya kazi huku akiangaliwa kwa karibu na Ferguson ambaye
atakuwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi. Moyes pia anauwezo wa kukuza vijana ,
kitu ambacho Man United wanakiamini sana.
No comments:
Post a Comment