KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Kim Poulsen amesema kwamba Rais Jakaya Kikwete amewataka wachezaji wa timu hiyo kupigana kufa na kupona katika mechi za kufuzi kushiriki fainali ya Kombe la dunia nchini Brazil mwaka 20014.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Poulsen alisema kwamba kauli ya Rais imepokelewa vyema na vijana wake na anamini kwamba wataifanyia kazi na kuibuka na ushindi katika mechi zote zinazowakabili.
"Tumetoka Ikulu mimi na vijana wangu tumefarijika sana kukutana na Rais Kikwete, Rais ametueleza maneno yakishujaa na kuwafanya vijana kuwa na morari kubwa na wamemwakikishia Rais kwamba watapigana kufa na kupona na kuibuka na ushindi"alisema Poulsen.
Mbali na mwaliko huo Stars jana ilipokea kitita cha Tsh 30milioni kutoka kwa kamati ya Saidia Stars ishinde inayo ongozwa na Mohamed Dewji. Leo vijana hao wa Kocha Kim Poulsen wamepata mwaliko wa kukutana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kikwete Ikulu jijini Dar es Saalam.
Stars inajiandaa kucheza mechi ya marudiano nchini Morocco juni 8 mwaka huu kabla ya kukipiga na Ivory Coast jijini Dar es Salaam, Stars inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi moja nyuma ya Ivory Cost yenye pointi 7 inatarajia kushinda mechi hiyo kabla ya mechi ya Ivory Coast itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa. Wachezaji hawa wa Taifa Stars wataondoka nchini hapa Mei 26 kwenda Addis Ababa Ethiopia ambako watacheza mechi ya kirafiki na baadaye kuondoka kwenda Casablanca ambako watacheza mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia Juni 8.
No comments:
Post a Comment