Monday, May 27, 2013

LWAKATARE ARUDI RUMANDE TENA .JAY DEE ASOGEZWA MBELE

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usala wa Chadema,Wilfred Lwakatale akionyesha alama ya vidole, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,jijini Dar es Salaam
WAKATI kesi inayomkabili Msanii wa muziki wa kizazi kipya Judith Wabura, (Lady Jay Dee) akiahirishwa hadi Juni 13 mwaka huu,Mkurugezi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakare amenyimwa dhamana kwa mara nyingine.
Lwakatare alipanda kizimbani kwa mara nyingine huku akitarajia kupata dhamana ya kesi yake, baada ya Mahakama Kuu kumfutia mashtaka ya Ugaidi yaliyokuwa yakimkabili na kumnyima dhamana.
Baada ya shitaka hilo kufutwa alibakiza kesi ya njama ya kumdhuru Denis Msacky ambayo inadhaminika.
Hata hivyo matumaini ya Lwakatare kupata dhamana ilitoweka na kurudishwa rumande hadi Juni 10 mwaka huu, Lwakatare amekosa dhamana hiyo baada ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo kuwa likizo.
Katika hatua nyingine kesi ya inayomkabili Lady Jay Dee iliahirishwa hadi Juni 13 mwaka huu, Mwanadada huyo alifunguliwa mashtaka katika Mahamaka ya Hakimu Mkazi Kinondoni na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media
Group, Joseph Kusaga pamoja na Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio Ruge Mutahaba.


Read 29 times

No comments: