Mwanaume Mwenye umri kati miaka 30- 40 aliyejulikana kwa jina moja la BANZA anayejishughulisha na biashara katika eneo la Ubungo Darajani jijini Dar es salaam, amejikuta akilazimishwa kuoga baada ya kilichoelezwa kuwa ni kukithiri kwa uchafu wa mwili wake kunakotokana na tabia ya kutooga.
|
BAB NOAH ADAMU AKIMNYOA NYELE BWANA BANZA . |
|
KICHWA CHA BWANA BANZA KIKIWA KIMEJAWA NA MAPUNYE, KUTOKANA NA KUTOOGA KWA TAKRIBANI MWAKA NA NUSU. |
Hatua hiyo ilichukuliwa na baadhi ya watu wanaoshirikiana na Banza katika biashara ambapo wamedai kuwa tabia hiyo imekuwa ikimsababishia mwezao huyo kukimbiwa na wateja na pia ikiwa kero kwao kutokana na harufu kali.
|
BAB NOAH ADAMU - ALIYE TEKELEZA ZOEZI LA KUMUOGESHA BWANA HUYO AKISIMULIA. |
|
MAMA RASHIDI - MKAZI WA DAR ES SALAAM AKIELEZEA UKWELI WA KIJANA HUYO KUWA KERO SEHEMU HIYO |
Mwanaume huyo inaelezwa kuwa Inafikia mwaka mmoja na nusu sasa akiwa hajawahi kuoga na mwili kuto kujua maji jambo ambalo liliwakera wateja na hata vijana wenzie nakuchukua uamuzi wa kumnyoa nywele, kumsafisha masikio na kumuogesha.
|
BWANA BANZA AKIWA AMESHIKILIA NGUO ZAKE CHAFU BAADA YA KUOGESHWA MCHANA KWEUPEE. |
|
BANZA KUSHOTO NA KULIA NI BAB NOAH ADAM AKIMVISHA NGUO BAADA YA KUMUOGESHA.
Shughuli hiyo ya kumuogesha lilifuatiwa na harambee ya kushtukiza kwa lengo la kumnunulia Banza nguo safi ambazo hata hivyo alizikataa kuzivaa lakini baadae alivalishwa kinguvu .
HABARI NA MR SEMVUA MSANGI BLOG
|
No comments:
Post a Comment