MWENYEKITI WA JUKWAA LA KATIBA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM KUHUSU MAAMUZI HAYO AMBAYO WAMEYAFIKIA YA KWENDA MAHAKAMANI KUZUIA MCHAKATO WA KATIBA MPYA |
MAELEZO KIDOGO
Jukwaa la katiba Tanzania limetangaza rasmi kwenda mahakamani kusimamisha mchakato mzima wa kutapatikana kwa katiba mpya kwa kile walichokisema kuwa ni mchakato huo kwenda kinyume na makubaliano yaliyotangawa na serikali wakati mchakato huo unaanza
Tamko ilo limetolewa na mwenyekiti wa jukwaa hilo bw DEUS KI KIBAMBA leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam
Bw KIBAMBA amesema wamefikia uamuzi huo baada ya juhudi zao nyingi walizozifanya ikiwemo kuonyesha mapungufu mengi yaliyojitokeza katika mchakato huo kutokufanyiwa kazi jambo ammbalo amesema ni kuwaburuza watanzania ambao wengi wanategemea kupata katiba imara
Aidha bw KIBAMBA amesema kuwa ni lazima tume ya katiba ikubali kuwasikiliza wadau wakiwemo wanasiasa,taasisi binafsi pindi zinapoikosoa mchakato huo ili waweze kutengeneza katiba imara nay a watanzania wote
Katika hatua nyingine ukwaa la katiba Tanzania limemwandika barua raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ya maombi ya kukutana naye kwa lengo la kumweleza hali halisi ya mchakato huo wa katiba na mapungufu ambayo wao wameyaona
No comments:
Post a Comment