Ni sehemu ya Nyumba kubwa iliyokuwepo katika Maeneo ya Kitongoji cha Mkombozi kijiji cha Kivule jijini Dar es Salaam, iliyobomolewa na Polisi kwa Madai kuwa wananchi hao hawaruhusiwi kukaa katika Maeneo hayo, ambapo Nyumba zaidi ya 300 zilibomolewa na wahanga hao wamepanga kwenda kwa Waziri Mkuu kupata haki yao baada ya kuomba msaada katika ngazi zote za Chini na kutopata Msaada wowote.
Takriban Wakazi zaidi ya 500 katika kijiji cha Mkombozi kata
ya Kivule Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam wasiokuwa na makazi ya kuishi
baada ya Kubomolewa nyumba zao na Polisi
kwa madai ya kuwa hawastahili kuishi maeneo hayo wanajiandaa kufanya Maandamano
ya kwenda katika Ofisi ya waziri Mkuu kupeleka malalamiko yao kwa ajili ya
kupata haki yao.
Akizungumza katika kikao cha wakazi hao Katibu wa wahanga hao, Mwanaharakati Julius
Zephania, alisema kuwa, wanaamini
kuwa haki yao ipo ila ni swala la wao kuipigania.
Zefania alisema kuwa, siku ya kwenda kwa Waziri mkuu
imekaribia ambayo wanaamini kuwa, ndio mkombozi wao ambapo alimwomba waziri
mkuu watakapofika wawaikiliza na kuwahurumia kwani nao ni wananchi kama walivyo
watu wengine.
Naye Mwenyikiti wa wahanga hao, Bw, Habibu Iddi amesema
kuwa, sababu zilizofanywa wao kubomolewa nyumba zao ni kwamba hawaruhusiwi
kukaa katika Eneo hilo na kwamba
anayewanyanyasa ni mtu mmoja walio mtaja kwa Majina ya Jordan Rugimbana
ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kinondoni ambaye anadai kuwa Eneo hilo ni lake.
“Tunamshangaa sana huyu mtu kutubomolea nyumba zetu , sasa
sisi umefika wakati wetu wa kupata haki yetu na ni lazima tufike kwa Waziri Mkuu kwani tunaamini ndiye pekee
anayeweza kutusikiliza. MAASINDA ilimtafuta Mwenyekiti wa Kijiji hicho,
Bw, Joseph Gasaya ambapo amesema kuwa,
swala hilo ameshalifikisha katika ngazi za juu lakini bado
anazungushwazungushwa ambapo alisema kuwa ni haki ya wananchi wake kwenda
Mahakamani.
No comments:
Post a Comment