Monday, May 6, 2013

TUKIO LA KULIPUKA KWA BOMU JANA ARUSHA HILI HAPA.































Kanisa katoliki parokia ya Olasiti ambalo leo hii lilikuwa linapandishwa hadhi ya kuwa Parokia lililolipuliwa na kitu kinachosemekana kuwa ni bomu mapema leo hii wakati ibada ikiendelea ambapo katika Ibada hiyo Balozi wa Papa alikuwa amehudhuria na ndiye aliyekuwa azindue Parokia hiyo.










Katika Sehemu iliyowekwa alama ya Pembe tatu ndipo kifaa hicho kinachosadikiwa kuwa ni bomu kilipo angukia na kulipuka na kujerui zaidi ya watu Ishirini ambapo inasidikika kuwa mtu mmoja amefariki Dunia.










Waumini walikuwa wamekaa eneo hili, ambapo baada ya Mlipuko huo eneo hilo lilizungushiwa uzio na Usalama  kwa ajili ya uchunguzi zaidi.










Hawa ni Baadhi tu ya Majeruhi










Huyu Bwana naye ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa urahisi, alijeruhiwa na Kitu hicho










Watu walikimbia Ovyo ovyo bila kujali kuwa wamesahau viatu vyao.

MAASINDA BLOG INATOA POLE KWA WALIOFIKWA NA MATATIZO HAYO NA KUWATAKA WAKRISTO WOTE KWA UJUMLA, KULIWEKA SWALA HILI KATIKA MAOMBI PAMOJA NA KUOMBA AMANI KWA AJILI YA TAIFA LETU.
 




















No comments: