VIJANA WAKIWA MAKINI KUJADILI MUSKABALI WA KATIBA YAO LEO JIJINI DAR ES SALAAM |
MGENI RASMI WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRICA MASHARIKI MH SAMWELI SITA AKIWA MAKINI KUZUNGUMZA NA WATANZANIA HAO VIJANA |
Waziri wa ushiurikiano wa Africa mashariki mh SAMWELI SITA amesema kuwa kundi kubwa litakalo athiriki au kufaidika na katiba ijayo ni kundi la vijana hivyo kuwataka vijana kuwa makini katika kuichambua rasimu ya katiba hiyo ili kupata katiba itakayotetea kundi hilo
Hayo ameyasema leo jijini dare s salaam katika uzinduzi wa mkutano wa siku tatu ulioandaliwa na baraza la katiba la vijana Tanzania wenye lengo la kujadili na kutoa mapendekezo yake katika rasimu ya katiba mpya ,mkutano ambao umewakutanisha vijana kutoka kila mkoa wa Tanzania
Mh SITA amesema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa kundi la vijana ndio kundi lenye watanzania wengi ambao ni zaidi ya asilimia 70 na watakaoishi Tanzania kwa muda mrefu hivyo katiba ijayo lazima iwalinde vijana na kuhakikisha mambo ya msingi yanaingia katika katiba mpya
Mh SITA amewataka vijana kuhakikisha katika katiba ijayo inaweka wazi mambo ikiwa ni pamoja na kuondoa utawala wa mabavu,utawala wa kujilimbikizia mali,na katiba ifanye Tanzania iwe na uongozi wa kidemocrasia jambo ambalo amesema limeanzaa kutoweka kwa sasa nchini
Katika mkutano huo vijana watajadili rasimu ya katiba iliyotolewa na tume ya mabadiliko ya katiba Tanzania,na mwisho kuwasilisha mapendekezo ya vijana katika tume hiyo
PICHA YA PAMOJA KATIO YA VIJANA HAO NA MH SITA |
No comments:
Post a Comment