Saturday, August 3, 2013

MWIGULU NCHEMBA AKIRI TATIZO LA AJIRA TANZANIA,ASEMA WATANZANIA WENGI WANA STRESS ZA MAISHA

           NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM BARA MH MBUNGE MIGULU NCHEMBA AMESEMA KUWA ASILIMIA KUBWA YA WATANZANIA HUSUSANI VIJANA WANA STRESS ZA MAISHA KUTOKANA NA HALI YA MAISHA KUENDELEA KUWA NGUMU SIKU HADI SIKU

          AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA JIMBO LAKE WANAOISHI JIJINI DAR ES SALAAM AMESEMA KUWA WATANZANIA HASA VIJANA WAMEKUWA WAVIVU WA KUWA WABUNIFU PINDI WANAPOMALIZA MASOMO NA BADALA YAKE KUAMUA KUKAA MAJUMBANI WAKISUBIRIA AJIRA JAMBO AMBALO AMESEMA SIO SAWA KWA SASA



AMESEMA KUWA TATIZO LA AJIRA NCHINI KWA SASA BADO NI DOGO UKILINGANISHA NA HUKO TUNAKOENDA KWANI HALI ITAKUWA MBAYA SANA KUFWATIA WATU WENGI SANA KUENDELEA KUHITIMU KATIKA VYUO VYETU  NA UFINYU WA AJIRA KUENDELEA KUWA MKUBWA

AMESEMA KUWA YUPO MBIONI KUPEKLEKA HOJA BINAFSI BUNGENI KUHUSU SWALA LA AJIRA KWANI JAMBO HILO LIMEANZA KUWA SUGU SANA KWA WATANZANIA WALIO WENGI.

MH NCHEMBA AMEKUTANA NA WANANCHI WANAOISHI DAR ES SALAAM AMBAO NI MPANGO WAKE WA KUWAWEKA PAMOJA WANANCHI HAO AMBAO NI WAPIGA KURA WAKE ILI KUILETEA MAENDELEEO JIMBO LAKE.

KATIKA MKUTANO HUO PIA UMEHUDHURIWA NA MKUU WA WILAYA YA IRAMBA

No comments: