Saturday, August 17, 2013

WANAOTAFSRI FILAMU ZA ULAYA NA KUZIUZA WAPIGWA MARUFUKU,

          KATIBU mtendaji wa bodi ya firamu Tanzania  Joiyce Fissoo ametoa miezi sita kwa watu ambao wanatafsiri Filamu za nje hapa nchini Tanzania kuacha mara moja kwani ni kinyume na sheria

       Akiongea na mwandishi wetu alisema “tumetoa miezi sita kwa watu wanaofanya kazi ya kutafsiri filamu za nje hapa nchini  kuacha mara moja na ni kinyume cha makosa ya hati miliki”alisema Fisoo

Aliongeza “atakaye kaidi amri hii atachukuliwa hatua kali na ikiwemo kufunguliwa mashtaka”alimarizia Fisoo

        Uchunguzi uliofanywa na HABARI24 umebaini kuwepo kwa watanzania wanaofanya kazi hiyo ya kutafsiri.Watanzania hao ambao uzichukua firamu hizo kwenye mitandao na kuziingiza Maneno ya Kiswahili na kuziuza

       Huku filamu hizo zikiwa hazina nembo ya Mamlaka ya Mapata Tanzania (TRA) kuashilia kama serikali inamapata mapato kupitia Biashara hiyo

          Habari24  ilifanikiwa kufika Maeneo ya Mtoni mtongani Wilaya ya temeke jijini Dar es salaam ambapo ndipo kuna mitambo ambayo inazidurufu Filamu hizo na kukuta biashara hiyo ikiendelea huku watu wakizigombania Filamu hizo ambazo teyari wameshaziingiza maneno ya Kiswahili.

          Mwandishi  alipowauliza wafanyabiashara waliokuwepo maeneo hayo ambao huzichukua filamu hizo  na kuzipeleka sokoni kuwa hawaoni kuwa ni makosa kufanya biashara isiyo halali “tunajua kuwa biashara hii sio halali lakini mbona serikali wanawaachia,ukiona hivyo hii biashara ni iko pouwa”alisema mfanyabiashara wa filamu hizo ambaye akutaja jina lake

       “Huu ni uzembe wa (TRA) hawafahamu hii inauzika sana wangekuja kuongea na hawa wanao fanya kazi hizi maana filamu hizi zinauzika nchi nzima na hapa kuna watu toka mikoa mbalimbali wamekuja kuzichukua firamu hizi” alisema mfanyabiashara wa firamu hizo ambaye akutaja jina lake

            Mwandishi alibaatika kupata majina ya watu wanaozitafsiri firamu hizo ambao ni Juma Shine au maharufu  Dj maki na mwengine anayejulikana kwa Jina moja Rufufu pamoja na Juma kani walipotafutwa wote kwa pamoja hawakuwa teyari  kulielezea hili na hawakupatikana mala moja

            HABARI24  iligonga hodi kwenye ofisi za Mamlaka ya mapato  Tanzania (TRA) kutaka kujua  wao kwanini wanawafumbia macho watu hawa. Nao hawakupatikana mtu wakuweza kuyajibu haya na zaidi mwandishi wa gazeti hili alazimika kuwacha taarifa kwa maandishi ofisini hapo na zitajibiwa

            Mwandishi akabaini kama serikali ikiendelea kuwafumbia macho watu hawa taifa liko hatarini kuwalipia madeni wananchi wake kutokana na watafsili kujipati mamilioni huku wasanii wa hizo firamu za nje hawapati kitu na wakija kufahamu serikali ijiandae kulipia wananchi wake

No comments: