Wednesday, August 14, 2013

WATUMISHI WA SERIKALINI NA WA SECTA ZA UMMA SASA KUNUFAIKA NA NYUMBA ZA BEI NAFUU,ZINAJENGWA MAENEO YA BUNJU NA MBEZI,NAIBU WAZIRI WA UJENZI AZITEMBELEA ,AUKUBALI MRADI HUO




            NAIBU WAZIRI WA UJENZI NCHINI TANZANIA MH GERISON LWENGE AMEFANYA ZIARA LEO KATIKA MAENEO YA BUNJU B NA MBEZI BEACH WA KUJIONEA MRADI WA NYUMBA ZAIDI YA 1400 AMBAZO ZINAJENGWA NA WAKALA WA MAJENGO TANZANIA KWA AJILI YA KUWAUZIA WAFANYAKAZI WA SERIKALINI NA WALE WA SECTA ZA UMMA

             KATIKA ZIARA HIYO MH NAIBU WAZIRI ALIKUTA ZAIDI YA NYUMBA 130 ZIKIWA KATIKA HALI NZURI YA KUKAMILIKA NA KUANZA KUTUMIKA AMBAPO AMERIDHIKA NA KASI YA UJENZI HUO HUKU AKUWASIHI WAONGEZE KASI ILI WAWEZE KUZITUMIA KWA MUDA MUAFAKA


NAIBU WAZIRI WA UJENZI MH GERISON LWENGE AKIPOKEA MAELEKEZO KUHUSU MAJENGO HAYO KUTOKA KWA VIONGOZI MBALIMBALI WA WAKALA WA MAJENGO TANZANIA WAKATI WA ZIARA HIYO ILIYOFANYIKA LEO 

MUONEKANO WA NYUMBA HIZO AMBAZO ZINAJENGWA MAENEO YA BUNJU B NA MBEZI BEACH JIJINI DAR ES SALAAM
         NAO WAKALA WA MAJENGO TANZANIA WAMEMUHAKIKISHIA NAIBU WAZIRI KUWA NYUMBA ZAIDI YA 130 ZITAKUWA TAYARI KWA KUTUMIKA IFIKAPO MWEZI WA KUMI MWAKA HUU KAMA HAKUTAKUWA NA MATATIZO MENGINE MADOGO AMBAYO YATAJITOKEZA HAPO KATIKATI,

ZIARA INAENDELEA
            KWA MUJIBU WA NAIBU WAZIRI NA WAKALA HAO NI KUWA WANAMPANGO WA KUJENGA NYUMBA ZAIDI YA 1400 JIJINI DAR ES SALAAM AMBAZO ZITAKUWA ZINAUZWA KWA WATUMISHI WA SERIKALINI NA WALE WA SECTA BINAFSI HUKU AKISEMA KUWA NYUMBA HIZO ZITAUZWA KWA BEI NAFUU AMBAYO KILA MYUMISHI ANAWEZA KUZINUNUA.



MSANIFU MAJENGO KUTOKA WAKALA WA MAJENGO TANZANIA TBA BI JULIET NDANDA MWAKYUSA  AKITOA MAELEZO KWA NAIBU WAZIRI JUU YA MRADI HUO MARA BAADA YA KUFIKA MAENEO HAO


HAPA AKIMWONYESHA RAMANI YA MAJENGO YALIYOPO MBEZI BEACH AMBAYO NAYO YANAJENGWA NA TBA


MAJENGO AMBAYO YANAJENGWA NA TBA KATIKA MAENEO YA MBEZI BEACH 


No comments: