Wednesday, September 25, 2013

SERIKALI YASEMA RUKSA KUFANYIA HARUSI UWANJA MPYA WA TAIFA

bw GODLEASE MALISA AMBAYE NI MSEMAJI WA WIZARA HIYO
       Serikali kupitia wizara ya michezo  tanzania imesema ni ruksa kwa mtu yoyote kuutumia uwanja mpya wataifa katika shughuli nyingine kama harusi,mikutano na matamasha mbalimbali kwa lengo la kupata mapato zaidi tofauti na ilivyoripotiawa na vyombo kadhaa kuwa ni kosa kufanya hivyo

    Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam msemaji wa wizara ya habari,vijana utamaduni na michezo bw GODLEASE MALISA amesema katika mkakati wao ni kupata mapato zaidi kwa kutumia uwanja huo jambo ambalo haliwezi kufanikiwa kwa kutegemea michezo husika tu hivyo lazima shughuli mbalimbali zifanyike katika uwanja huo ikiwemo harusi na mikutano mingine

No comments: