Tuesday, September 24, 2013

WAWILI WAKUTWA NA MAITI YENYE MADAWA YA KULEVYA TUMBONI HUKO TABATA


MADAWA AMBAYO MAREHEMU ALIUKUTWA NAYO TUMBONI
    Jeshi la plisi kanda maalum ya dar es salaam linawashikilia watu wawili kwa kosa la kkutwa na maiti ambayo ilikuwa na madawa ya kulevya tumboni aina ya heroine pipi 33,

    Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam kamishna  wa polisi  kanda maalum ya dar es salaam  SULEMAN KOVA  amewataja watuhumiwa hao kuwa ni NASRI OMARI na MWANAISHA SALIMU  wakazi wa kigogo luhanga.

              Madawa hayo yalikamatwa maeneo ya tabata ambapo KOVA amesema kua polisi walpata taaifa kuwa kuna mtu mmoja amefariki hghafla muda mfupi baada ya kutoka bafuni kuoga ndipo walipofika nyumbani kwa NASRI OMARI na kuhoji hatimae kugundua uwepo wa maiti sebuleni iliyouwa imelazwa chali.
Kwa mujibu wa mmliki wa nyumba hiyo NASRI alisema kuwa marehemu anajulikana kwa jina la RAJABU KIDUNDA .

           Polisi wamesema kuwa marehemu alifika toka mtwara na alipokelewa na watuhumiwa hao wawili ,ambapo wate wanashikilia kwa uchunguzi zaidi
KAMISHNA KOVA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MAPEMA LEO
BAADHI YA WANAHABRI WAKISIKILIZA KWA MAKINI

No comments: