TAARIFA MBAYA ZILIZOJIRI DAR LEO.SOMA HAPA
Kiwanda cha kutengeneza ndala cha Ok Plastic kilichopo maeneo ya Vingunguti Jijini
Dar es salaam kimeteketea kwa moto leo.Moto huo unasemekana
kusababishwa na kijana mmoja aliyekuwa akichoma mabaki ya takataka ya
kwenye dampo lililopo jirani na Kiwanda hicho ambapo inasemekana kwamba
moto huo ulishika kasi na kusambaa katika maeneo mengine yaliyo jirani
na sehemu ambako moto ulianzia na baadaye kuufikia Kiwanda hicho.Mpaka
muda huu habari hizi zinaripotiwa magari ya kuzima moto yameshafika eneo
la tukio wakiendelea kuuzima moto huo.
SOURCE ITV
No comments:
Post a Comment