Wednesday, October 9, 2013

WAMILIKI WA MALORI WAMJIA JUU WAZIRI MAGUFULI,SOMA WALICHOKISEMA

FEISAL LAZA
     Wamiliki wa malori chini leo wamesema kuwa hawajagoma kama inavyoelezwa bali walichokifanya ni kupai magari yao kuepuka kuharibu barabara kama ilivyoelezwa na waziri wa ujenzi maguguli.akizungumza na aandish wa abari jijini dar es salaam mmoja wa wamiliki hao DAVIS MOSHA amesema kuwa wamiliki wa malori ni watanzania wazalendoivyo hawawezi kugoma kwa lolote na hakuna manya biashara anayegoma bali wamepaki malori yao hadi hapo waziri magufuli atakapo wasikiliza

   Aidha wamesema kuwa wamechoka kuburuzwa na waziri magufuli kwani sio mara ya kwanza kwa kuburuzwa kwani wamekuwa wakitungiwa sheria bila kushirikishwa na kuanza kuzitumia jambo ambalo wamesema sasa hawalikubali tena litokee.Wamesema kuwa hawatawasha magari yao hadi hapo watakaposikizwa madai yao na waziri husika kwani wao hawana tatizo na serikali bali wanatatizo na waziri wa ujenzi mh JOHN POMBE MAGUFULI.

    Aidha wamesema kuiwa wanashangazwa na kauli ya MAGUFULI kuwa wakizidisha hata tani moja wataharibu barabara na kuwa inawezeana ubora wa barabara hizo sio mzuri,kitu ambacho kinamfanya waziri kua na wasiwasi

DAVIS MOSHA AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO


No comments: