SERIKALI imeahidi
kuendelea kutoa ushirikiano na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA ili kuiwezesha mamlaka hiyo iweze
kufikia malengo yaliyokusudiwa .
Rai hiyo
imetolewa na Makamu wa raisi wa jumhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Mohammed Gharib Bilali katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya mamlaka ya
mawasiliano Tanzania TCRA.
Katika
kipindi cha miaka kumi mamlaka ya mawasiliano TCRA imelifanya Taifa kupiga
hatua katika maendeleo kiuchumi.
Pamoja na
hayo Bilali amezitaka kampuni za mawasiliano zisambaze huduma zake zote katika
maeneo yote hapa nchini kwani serikali kupitia mfuko wa kusambaza huduma za
mawasiliano watahakikisha wanatoa huduma wanao nufaika na mfuko huo kwa manufaa
ya wananchi.
Hata hivyo
ametoa wito kwa makampuni kutoa fursa ya mafunzo na elimu ya kisasa ya mifumo
mipya ya mawasiliano kwa wafanyakazi wake ili waendane na kasi ya mabadiliko ya
kiteknolojia.
mwishooo
|
No comments:
Post a Comment