MKURUGENZI WA MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA TSNP ALPHONCE LUSAKU AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM |
MTANDAO wa Wanafunzi nchini “TSNP’
umemtaka Waziri mkuu nchini , Mh Mizengo Pinda kuitoa hadharani mara moja
Ripoti ya tume iliyoundwa kwa ajiri ya kuchunguza matokea ya kidato cha nne,
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam
na Mkurugenzi wa mtandao huo wa wanafunzi
nchini, ALPHONCE LUSAKU amesema wao Umoja wanafunzi wanamuomba waziri
mkuu atoe ripoti ya tume hadharani ili wananchi wafahamu,
“Tunamtaka wazir mkuu Mh Mizengo Pinda.
Ndani ya wiki moja, atoe Ripoti ya tume hadharani.Juu ya madhaifu
yaliyopatikana,wakina nani wamehusika na madhaifu husika,mapendekezo ya
tume husika ili yasijurudie tena kwa wadogo zetu’”alisema LUSAKU
Vilevile mtandao huo wa wanafunzi
nchini wamemtaka pia mwenyekiti wa tume hiyo pia ambaye ni katibu wa
Wizara ya elimu kwa sasa Profesa Sifuni Mchome ajitokeze hatokeze Hadharani na
aitoe ripoti husika kwa watanzaia.
Ripoti hii iliundwa baada ya matokeo
mabaya ya kidato cha nne mwaka jana,yalionyesha kuwa watainiwa walikuwa 397,136
kati ya wanafunzi hao nusu yake walipata daraja la sifuri,na kupelekea
kuwepo kwa manunguniko mengi kutoka kwa wadau wa elimu pamoja na wananchi,
Kwa upande mwingine mwenyekiti mtandao huo
wa wanafunzi nchini Julias Maila alimtaka waziri wa elimu nchini, Shukuru
kawambwa kusitisha mala moja mabadiriko ya madaraja ya kwawanafunzi wa kidato
cha nne
“Tumesikitishwa sana na mkanganyiko
uliojitokeza hivi karibuni,juu ya uwepo wa division “o” na division ‘5” kati ya
katibu wa wizara mkuu wa wizara ya elimu profesa Sifuni Mchome na Naibu
waziri wa elimu Mhm Philipo Mlugo .Hasa katika wakati huu anbapo wadogo zetu wa
kidato cha nne wanafanya mitihani yao ya mwisho”alisema Maila
No comments:
Post a Comment