MAMA NYERERE KUHUDHURIA MAZISHI YA MANDELA
Maria
Nyerere ambaye ni mke wa aliyekuwa rais wa kwanza nchini Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere, amesema Nelson Mandela ataendelea kukumbukwa kwa
moyo wake wa kusamehe na kumtaja kwamba alikuwa ni zawadi ya dunia
katika kuleta upendo na maridhiano.
Uhusiano
kati ya familia ya Mwalimu Nyerere na ile ya Mzee Nelson Mandela
umekuwa ni wa karibu kiasi kwamba familia yake inajiandaa kwenda
kuhudhuria katika mazishi yatakayofanyika tarehe 15 mwezi huu.
Source:BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment