Na Karoli Vinsent
MWENYEKITI wa
chama cha democrasia na Maendeleo’ CHADEMA Freeman Mbowe ,amehofia chama chake huwenda
kikapata mpasuko,kama uliowakuta Chama cha NCCR Mageuzi kipindi cha nyuma.
Hofu hiyo
ilibainika Leo wakati wa Mkutano mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi uliofanyika jijin
Dar es Salaam,ambapo Freeman Mbowe alipokuwa anazungumza kwa niaba ya Vyama vya
upinzani,alisema watu wengi hawajui historia ya vyama vya kisiasa vilivyoanzia
,
“Leo watu wengi hawajui vyama hivi vya kisiasa vimeanzia
wapi kwa mfano chama cha NCCR kimepitia sehemu nyingi hebu tukumbuke wote
chama hiki kipindi kile walipoibuka “UDETA” Umoja wa Demokrasia Tanzania
walibuka watu wakawa wakaipasua chama hichi, wako wanaojiita NCCR asilia,leo
wako wapi na kila chama cha upinzani Tanzania kitapia Sehemu hii hata
mimi napitia huku”alisema Mbowe
Freemani Mbowe
ambaye ni Mbunge wa Jimbo Hai kupitia Chama Cha Chadema na pia ni
Kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni alizidi kusema kuwa inahitajika nguvu
kubwa sana kuvilinda vyama vya kisiasa
“Kukiua Chama cha
Kisiasa ni kazi ndogo sana ila Kukijenga chama cha Kisiasa ni kazi kubwa ambayo
inaitaji hata kipindi cha muongo mmoja mpaka kukirudisha chama
hicho,tunaitaji nguvu kubwa sana kuvilinda vyama ,leo tunaitaji Nccr au
Cuf,Chadema yenye nguvu tuweze kuijenga nchi na tuweze kuondoa CCM
mdarakani”alizidi kusema Mbowe
KUHUSU KATIBA MPYA-ENDELEA HAPO------
Mwenyekiti
huyo wa Chadema aliwataka vyama vya kisiasa visiingilie katika mchakato
huu wa katiba Mpya kwani wanaweza kuharibu mwenendo huu wakatiba mpya
“Leo nashangaa
sana sisi wanasiasa tunavyoingila mchakato huu wa katiba mpya nashangaa sana
leo CCM wanavyosema wao wanaunga mkono serikali mbili kwakuwa sio ilani
ya chama chao, swali la kujiuliza je katiba hii ni ya chama au ya
wananchi, nawaomba wanasiasa wenzangu tusiingilie mchakato huu kwani tutakuwa
tunahalibu kwani katiba hii si ya wanasiasa bali ya wananchi hata wengine
wasiokuwa na chama”alimalizia Mbowe
Kwa upande wake
Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM Mustafa
Jaffer Sabodo alivitaka vyama vya kisiasa nchini hususani chama cha Wanchi CUF
pamoja na Chadema na Chama cha NCCR mageuzi kuungana ili waweze kuingoa CCM
madarakani,
“Naviomba vyama CUF na NCCR pamoja
na CUF unganeni ili muweze kuingoa CCM madarakani,nataka niwambia kuwa kuiondoa
CCM mdarakani inahitajika nguvu kubwa sana kutoka kwenye vyama hivi”alisema
Sabodo
Katika hatua nyingine Kada huyo wa
Chama cha Mapinduzi akatoa hundi yenye Thamani ya Sh milioni 20 kwenda kwa
Chama hicho cha NCCR pamoja na kukihaidi chama hicho kukipia msaaada kwenye
Majimbo ya Wabunge wachama hicho Maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwajengea visima
vya maji kila Jimbo
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi CCM “bara” Philipo Mangula alikipongeza chama cha
NCCR kwa kazi kubwa walioifanya sana mpaka kufika Chama hicho kufanya Mkutano
huo mkuu
Mpaka Mwandishi wa mtandao huu anaondoka ukumbini hapo Chama hicho cha
siasa kulikuwa bado akijanza kufanya uchaguzi mkuu wa chama hicho
No comments:
Post a Comment