KATIKA
kukabiliana na uhaba wa walimu nchini serikali imetangaza kuajiri walimu wapya
36,071 ambapo watapangiwa vituo vya kazi mwezi ujao.
Hatua
hiyo ni mikakati ya serikali katika kukabiliana na uhaba wa walimu ambapo sasa
watakuwa na upungufu wa walimu 21684 kutoka 57755 iliyokuwepo kabla ya kutanga
ajira hizo mpya.
Naibu
waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Kassim
Majaliwa, alisema jana kuwa walimu hao watasambazwa katika shule za msingi na
sekondari nchini.
Alisema
taratibu zote za ajira kwa walimu hao wapya zimekamilika na kwamba mwezi ujao
wote walioajiriwa watakuwa wamepangiwa vituo vyao vya kazi.
Majaliwa
alisema majina ya walimu wote walioajiriwa na vituo vyao vya kazi tayari kwa
kuanza majukumu na serikali itaendelea kuhakikisha uhaba wa walimu nchini
unakuwa historia.
Hata
hivyo alisema kati ya walimu hao wapya 36021 watakuwa chini ya TAMISEMI na
waliobaki watapelekwa kuwa chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Aliongeza
kuwa kati ya walimu hao wa ngazi ya cheti ni 17,928 stashahada 5416 na wale wa
ngazi ya shahada ni 12,677.
Alisema
mgawanyo wa walimu hao uatazingatia na kutoa kipaumbele kwa maeneo na shule
zenye uhaba mkubwa ili kuhakikisha changamoto hiyo inaendelea kutatuliwa.
"Tumepanga
walimu kulingana na mahitaji ya shule husika ili kuifanya ikama itoshe. Tumetoa
maelekezo kwa maofisa elimu na wakurugenzi nchini kuacha tabia ya kuwajaza
walimu wengi katika kituo kimoja. Tutasimamia kikamilifu kuwasambaza walimu hao
ili kuhakikisha shule zenye uhaba mkubwa zinapewa kipaumbele," alisema.
Alisema
baada ya kukamika kwa taratibu walimu wapya wanatakiwa kuanza kuripoti katika
vituo vyao vya kazi kuanzia aprili mosi mwaka huu.
Alisema
idadi hiyo inajumuisha walimu wa masomo ya sayansi wa shule za msingi,
sekondari, vyuo vya ualimu na walimu wa elimu maalumu.
Kwa
mujibu wa vyanzo mbalimbali kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kila
mwaka zaidi ya walimu 40,000 huitimu nchini kutoka kwenye vyuo mbalimbali.
Mwaka
jana serikali ilitoa ajira mpya kwa walimu 26,537 wa shule za msingi, sekondari
na vyuo vya ualimu ambapo mwaka juzi wali
No comments:
Post a Comment