BW FADHIL SULEMAN AKISHANGILIA KWA FURAHA BAADA YA KUKABIDHIWA MFANO WA HUNDI YA SHILINGIM MILLION KUMI KAMA MSHINDI WA TIGO |
Kampuni ya simu za mikononi yaTIGO TANZANIA leo imehitimisha promotion
yake ya CHEZA KWA FURAHA UNAPOSHINDA KITITA kwa kuwakabidhi washindi wake wa
mwisho ambapo kivutio kikubwa ni dereva bajaji aliyejishindia shilingi million
kumi
Akizungumza na wanahabari leo jijini
dar es salaam mratibu wa promotion hiyo MERY RUTTA amewataja washindi wa zawadi
za mwisho leo kuwa ni MWANTUM JUMA aliyeshinda million mbili ambaye ni mama
ntilie,na mshindi wa million kumi ambaye ni dereva bajaji maeneo ya kijitonyama
bw FADHIL SULEMAN.
Akizungumza baada ya kupata zawadi hiyo
bw FADHIL amesema kuwa hakuamini hata kidogo baada ya kupigiwa simu kuwa
ameshinda lakini sasa anaanza kuamini kuwa ameshinda kweli na kusema kuwa
itamsaidia kwenye mambo yake ya kila siku.
Leo ndio imefikia mwisho wa promotion
hiyo ambayo meneja mwasiliano wa tigo bw JOHN WANYANCHA amesema kuwa lengo la
shindani hilo ilitokana na kampuni hiyo kuwapa kipaumbele wateja wake kwa
kuwapa puia sababu ya kutabasamu na fursa ya kuweza kubadilisha maisha yao.katika
kipindi cha miezi miwili jumla ya billion 1.2 zimenyakuliwa na wateja wa tigo
katika promotion hiyo
MRATIBU WA PROMOTION HIYO MARY RUTTA AKIMKABIDHI HUNDI |
No comments:
Post a Comment