Chemba iliyobomoka ikiwa wazi maeneo ya Mwenge
Hapa ni chemba Hiyo ambayo ipo wazi na pembeni ya barabara ya mwenge kukunja kuelekea mama ngoma
Mawe yakiwa yamewekwa kuzuia magari yasipite hapo baada ya chemba hiyo kubomoka
Hapa ni njia ya kukunja ya magari yanayotoka Njia ya mama ngoma eneo la mwenge
Chemba
iliyobomoka maeneo ya mwenge jiji dar imekuwa kero kwa watumiaji wa
barabara ya kutoka mwenge kuelekea afrika sana.Chemba hiyo ambayo
ilibomoka baada ya gari la mizigo kutumbukia hapo na kusababisha
kuharibika kwake.Mtandao wetu wa Dj sek blog ulifanya mahojiano na
waendesha bajaj na wafanyabiashara wa eneo hilo ambao walisema shimo
hiilo limekuwa ni hatari kwa watumiaji wa barabara hiyo kwani kuna
magari mengi yametumbukia hapo baada ya kupasuka kwa shimo hilo.
Waliongeza kuwa baada ya chemba hiyo kupasuka Dawasco walikuja
wasafisha tu uchafu uliokuwemo humo na kuweka alama za tahadhari kisha
wakaondoka.
Sasa imepita takribani wiki moja sasa toka dawasco wameliona tatizo hilo lakini hakuna matengenezo yoyote ya chemba hiyo.
Pia
wameongeza kwa kusema ifikapo jioni huwa shida sana kwa magari
kupishana eneo hilo kwani magari yanayotoka afrika sana inabidi kukunja
kwa kutumia upande wa magari yanayotoka barabara inayotoka kwa mama
ngoma,hivyo kusababisha foleni kubwa na usumbufu.
Watumiaji
wa eneo hilo wameiomba manispaa ya Kinondoni kutatua tatizo hilo kwani
mvua zinazoendelea kunyesha zitaleta madhara kwa kuwa chemba hiyo
itakuwa inamwaga maji machafu nje ambayo itapelekea magonjwa.
No comments:
Post a Comment