Monday, March 31, 2014

HABARI AMBAYO IMELISONONESHA TAIFA LEO--------AJALI MBAYA 14 WAFARIKI DUNIA, WAOKOAJI NAO WAZOLEWA WAFARIKI NA KUFIKIA WATU 21



         Watu 21 wamefariki dunia katika ajali mbaya imetokea Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani ikihusisha magari 3 na wengine 11 kujeruhiwa.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei, alisema ajali hiyo imetokea katika Barabara Kuu ya Dar es Salaam-Lindi, eneo la Ikwiriri, wilayani humo.
         
        Awali ajali hiyo ilihusisha magari mawili, Toyota Hiace (T 948 CUX), iliyokuwa ikitokea Ikwiriri kuelekea Rufiji ambalo lilikwenda kukwaruzana na Lori(T 132 AFJ) kwa nyumba, ambalo lilikuwa limeharibika na kusimama barbarani.

         Alisema baada ya kulikwaruza roli hilo, mlango wa Hiace uling'oka na kubaki kwenye roli ambapo gari hiyo lilipoteza mwelekeo na kwenda kugongana uso kwa uso na gari nyingine aina ya Canter(T 774 CJW) na kupinduka.
 
       "Katika ajali hii, watu 14 walifariki dunia papo hapo, wakati polisi na baadhi ya wananchi wakiendelea kuwaokoa majeruhi ili wakimbizwe hospitali, likatokea basi la kampuni ya Mining (President)( T 242 BXA), kuwakanyaga watu waliokuwa wakitoa msaada na kuwaua ndio maana idadi ya waliokufa imefikia 21.

No comments: