Na karol vicent
BAADA ya kuwa kimya kwa muda
mrefu,mfanyabiashara maarufu Nchini,Rostam Azizi ameanza kujipanga upya
kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,kwa kuamua kuimarisha kampuni yake ya Magazeti
ya New Habari(2006LTD),Huku akingoa kikosi cha wahariri wa Kampuni ya Mwananchi
,mtandao huu umebaini.
Rostam tangu ajiuzulu nyadhifa zake zote
hapa nchini amekuwa kimya huku akitajwa kutumia mda mwingi nje ya nchi
kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya biashara zake.
Taarifa za kuaminika ambazo mwandishi wa
mtandao huu amezipata na pia zimethibitishwa na vyanzo mbalimbali ndani na nje
ya kampuni ya Mwananchi ,zinaeleza kuwa Rostam sasa ameanza mikakati mzito wa
kuimarisha kampuni yake ya magazeti ya NewHabari na kuivuruga Kampuni ya
Mwananchi.
Taarifa,hizo zinasema mpaka wiki
iliyopita watu walikuwa wamethibitisha kuacha kazi na kuchukuliwa na
Kampuni ya Rostam ni pamoja na Dennis Msacky ambaye alikuwa Mhariri Mtendaji wa
Gazeti la Mwananchi.
Msacky amekuwa akitajwa kama kiungo
muhimu cha mafanikio ya Gazeti Mwananchi kabla ya malalamiko ya hivi karibuni
kutoka kwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samweli Sitta kumshutumu
Mhariri huyo kujiingiza katika Masuala ya Kisiasa.
Wengine ambao wamekwisha kutoa Barua za
kuacha Kazi ni Edwini Mjwahuzi ambaye alikuwa ni Mpiga picha Mkuu wa Kampuni ya
Mwananchi na pia huyu naye amekuwa akitajwa kuwa ni kiungo muhimu wa mafanikio
ya Gazeti hilo.
Kwa Mujibu wa vyanzo vyetu
vinasema .katika mkakati huo Rostam ameweza kumchukua mhariri wa Habari
wa Mwananchi,Samsoni Mfalila ambaye naye ametajwa kuwa na uwezo mkubwa.
Taarifa hiyo inazidi kusema kwamba
yuko pia mpiga picha mwingine Fidelis Felix naye anakwenda kwenye
kampuni hiyo na kujiunga na kikosi cha Rostam kutoka Mwananchi.
Chanzo hicho kinasema Mbali na
wahariri hao,pia katika kikosi hicho yumo Meneja usambazaji msaidizi Erasto
Matasia ambaye naye amekabidhi barua ya kuacha kazi kwenye Gazeti la
Mwananchi.
Vyanzo hivyo vinasema mpaka
sasa wahariri hao walikuwa bado hawajaripoti moja kwa moja kwenye kampuni
ya New Habari,lakini mwisho wa safari yao ni kwenye kampuni hiyo yenye mako
makuu sinza kijiweni.
Rostam,ambaye alikuwa mbunge wa
Igunga alijuzuru ubunge huo na kutokana na kile alichokisema siasa za Tanzania
zimejaa siasa Uchwara,Taarifa hizo zinasema sasa wahariri watatu pamoja na
Mpiga picha mmoja wanasuburi muda wao waliotoa kampuni ya Mwananchi uweze
kukamilika ndipo waondoke.
Chanzo hicho kinasema kikosi hicho
cha wahariri kilichoondoka ni kidogo kwani kunaorodha nyingine ya watu muhimu
ya takribani 16 kwenda kwa Rostam,watu hao watatoka kwenye kitengo cha
picha,uzalishaji gazeti mitamboni,fedha,chumba cha habari na utengenezaji
gazeti(Graphics).
Rostam ambaye pia anatajwa kwa sasa
kununua hisa kwenye kampuni ya Airtel Kenya na ujenzi wa bomba la mafuta kutoka
Lamu hadi juba,sudani kusini,anapanga kuifanyia New Habari kuwa kubwa zaidi
nchini kuliko Mwananchi.
TIDO APAMBANA KUNUSURU JAHAZI
Lakini,katika mkutano wake na wafanyakazi
uliofanyika mwanzoni wa wiki iliyokwisha jana,Mkurugenzi Mtendaji wa
MCL.Tido Mhando aliwaasa wafanyakazi waliobaki wasiwe na wasiwasi na wasiwe
kama na kutangatanga njia kama wafugaji wanaotafuta malisho.
Tido ambaye pia aliwananga wanaohama
kuwa akiwaita kama Makanjanja wanaotafuta Fedha za Mafisadi,alitangaza haraka
kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wahariri hao waliondoka.
Kwa upande wa Mhariri mtendaji wa
Mwananchi ilichukuliwa na mhariri kutoka gazeti la michezo la Mwananspoti Frank
Sanga iliyoachwa wazi na Msacky huku Reginald Miruko akijaza nafasi ya mhariri
wa Habari iliyoachwa wazi na Mfalila.
Chanzo hicho kilisema kiliongeza na
kusema kwamba Tido na Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi,Bakari Machumu
wamekuwa wakijipanga kuhakikisha Kampuni hiyo haiyumbi katika kipindi hiki
kigumu.
Taarifa za Kuaminika ambazo
Mwandishi wa Mtandao huu amezipata kuwa mkurugenzi huyo wa Mwananchi Tido naye
kwa upande wake mkataba wake unakaribia kumalizika na Duru hizo zinasema atarajiwa
kwenda Kampuni ya Azam.
MSACKY ATAJWA KUENDESHA UASI
Hata hivyo,hii si mara ya kwanza kwa
Mwananchi kukimbiwa na kundi la waandishi wakiongozwa na Msacky,mara ya kwanza
ilikuwa mwaka 2007 walipokimbilia kampuni ya Kampuni ya Gurdian.
Katika kipindi hicho Msacky
aliondoka na mahariri mwengine aliyekuwa nguzo ya kampuni hiyo Sakina Datoo
lakini, Baadaye msacky alirejea tena Mwananchi na kuacha wafuasi wake (kasoro
Mjwahuzi)Gurdian.
Katika hatua Nyingine
Mwandishi wa Mtandao huu amezipata kutoka kwa Kampuni ya New Habari ambao ni
wachapishaji wa Magazeti ya Mtanzania,Rai nguvu ya hoja.The African,gazeti la
michezo la Dimba pamoja na Bigwa,zinasema Uongozi wa Kampuni hiyo teyari
umeanza kuwaambiwa waandishi wake ambao wanatoa mchango mdogo katika ufanyaji
kazi na wale wenye elimu ndogo wajiaandae kufukuzwa.
Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania
ambaye akutaka jina lake litajwe kwenye Mtandao huu kwa kile alichokisema yeye
sio msemaji wa Kampuni hiyo alisema kwa sasa kampuni yake imekuwa inaanza
kufuatilia ufanyaji kazi wa kila mwandishi na kusema kwa sasa kampuni hiyo
itawafukuza kazi na kupunguza waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment