Nkamia
amebainisha kuwa magazeti yanayowachafua watu, serikali na kuhatarisha usalama
wa nchi yatakumbana na kifungo.
Itakumbukwa
mwaka jana serikali ililifungia gazeti la Mtanzania kwa miezi mitatu na
Mwananchi kwa wiki mbili, kwa madai ya kuandika habari za kichochezi.
Nkamia, alitoa vitisho
hivyo jana kwenye tamasha la vijana lililoandaliwa na Taasisi ya
Voice of Youth (VOYC) lililokuwa likijadili masuala mbalimbali yahusuyo vijana.
Miongoni mwa
mambo yaliyokuwa yakijadiliwa ni ujira, uzalendo, ujasiriamali na ajira,
Nkamia alisema hatakubali siku moja asutwe kwa kutotimiza wajibu wake katika wizara anayoisimamia, kwa kuwaachia waandishi wasiofuata maadili ya taaluma yao.
Nkamia alisema hatakubali siku moja asutwe kwa kutotimiza wajibu wake katika wizara anayoisimamia, kwa kuwaachia waandishi wasiofuata maadili ya taaluma yao.
“Mimi sitaki kufanya kazi na waaandishi wa habari
makanjanja, ambao si makini na wanaofanya kazi kwa masilahi ya kundi fulani la
watu.
“Tutakifuta, kukifungia chombo chochote cha habari pamoja na
waandishi wake wanaokwenda kinyume cha maadili ya uandishi wa habari,
sitaruhusu wanaoendekeza kuwachafua wengine, umbea,” alisema.
Alisema
amefanya kazi hiyo kwa kuzingatia maadili ya taaluma hiyo kabla ya kuingia
kwenye siasa ambako sasa anasimamia wizara inayoshughulika na waandishi wa
habari.
Nkamia pia
alitumia fursa hiyo kuwasihi vijana waache kushiriki kwenye maandamano
yanayoitishwa na vyama vya siasa alivyoviita havina malengo mema kwa taifa.
Alibainisha
kuwa vijana hawawezi kupatiwa fedha kama hawafanyi kazi yoyote, kwani hata
mataifa yaliyoendelea ambayo ni Marekani na Uingereza hawafanyi hivyo.
Hata hivyo
katika mkutano huo, viongozi wa halmashauri na mkoa walikacha kuhudhuria na
hawakutuma wawakilishi katika tamasha hilo licha ya kualikwa.
Kukacha kwao huko kulisababisha
gumzo kubwa na Afisa Tarafa ya Nyamagana, Maximilian Kailanga, alibeba jukumu
la kumkaribisha Nkamia
No comments:
Post a Comment