Wednesday, April 30, 2014
UKAWA ZANZIBAR INATISHA WAITEKA ZANZIBAR KIWANJA CHA KUBANDA MAITI LEO
BREAKING NEWS; AZAM FC YAIMALIZA YANGA--FRANK DOMAYO ASAINI MIAKA MIWILI AZAM LEO
KIUNGO mkabaji wa Yanga SC, Frank
Domayo amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na mabingwa wapya wa Tanzania
Bara, Azam FC jioni ya leo mjini Mbeya.
Domayo amesaini Azam FC baada ya
kumaliza Mkataba wake wa miaka miwili na Yanga SC, ambayo alijiunga nayo
akitokea JKT Ruvu miaka miwi iliyopita.
Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa
Mohamed ‘Father’ amesema katika kuendelea kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya
msimu ujao wamepiga hatua nyingine kwa kumsaini Domayo.
“Kama unavyojua, baada ya kumaliza
msimu vizuri tukiwa mabingwa wa Bara, tuligundua mapungufu kwenye kikosi chetu
na kwa ushauri wa mwalimu wetu (Joseph Marius Omog) ndiyo tunayafanyia
kazi,”alisema Father.
Domayo anakuwa mchezaji wa wa pili
ndani ya siku mbili kusajiliwa na Azam FC kutoka mabingwa wa zamani na mabingwa
wa kihistoria Tanzania Bara, Yanga SC baada ya jana klabu hiyo kumsaini
mshambuliaji Mrundi Didier Kavumbangu.
MAJAMBAZI WAVAMIA OFISI ZA GAZETI LA MAJIRA,WAKOMBA KOMPYUTA ZOTE
Na Karoli Vinsent
Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa Majambazi wamevamia makau makuu ya ofisi za Gazeti la majira,zilizopo
Jijini Dar Es Salaam na Kuiba Kompyuta zilizopo kwenye Chumba cha Habari.
Kwa Mujibu wa Waandishi wa Gazeti hilo
waliozungumza na Mwandishi wa Mtandao huu ambao hawakutaka kutajwa Majina yao
kwenye Mtandao huu wakisema wao sio wasemaji wa Gazeti hilo,walithibitisha wezi
kulivamia Gazeti hilo na kuiba vitu vyenye Thamani isiojulikana.
SERIKALI YAENDELEA KUTOA ONYO KALI KWA GAZETI LA MAWIO,SASA WAWATAKA KUFWATA MAAGIZO YALIYOTOLEWA,LA SIVYO----
Na Karoli Vinsent
MKURUGENZI wa Idara ya Habari MAELEZO
amelitaka Gazeti la Mawio kufuata maagizo aliyatoa ,Lasivyo wakiendelea kukaidi
Basi wasubili hatua kali zaidi.
Kauli hiyo ya mkurugenzi wa
idara hiyo Asah Mwambene,imekuja siku chache kupita baada ya Gazeti la mawio
kwa kupitia mkurugenzi wake kusema kwamba hawajapata barua kutoka kwenye Idara
hiyo ya Habari maelezo iliyowataka waombe Radhi na kusema hawana barua hiyo ili
wao waweze kuchukua hatua hiyo
wanayoitaka.
KATIBU MKUU WA FIFA KUWASILI NCHINI KESHO
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Jerome Valcke
anawasili nchini kesho (Mei 1 mwaka huu) ambapo atafungua semina ya mawasiliano
kwa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na
Kati (CECAFA).
Valcke
ambaye atafuatana na maofisa wengine saba wa FIFA baadaye kesho hiyo hiyo (Mei
1 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika
saa 4 kamili asubuhi kwenye hoteli ya Double Tree by Hilton iliyopo Oysterbay,
Dar es Salaam.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
KUWA WA KWANZA KUFAHAMU HUDUMA MPYA ILIYOZINDULIWA LEO NA BENKI YAKO YA NMB
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NMB,Mark Wiessing |
Na Karoli Vinsent
BENKI ya NMB katika kuonyesha inawajali wateja wake
sasa Imezindua huduma itakayowafanya Wateja wake kufurahia Ubora wa Benki
hiyo,Baada ya Kuzindua Huduma mpya ijulikanayo “JIHUDUMIE”
Akizindua
Huduma hiyo,leo hii Jijini Dar Es Salaam, mbele ya Waandishi wa Habari na
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NMB,Mark Wiessing alisema Kampeni inayojulikana
“Jihudumie ni huduma mpya ambayo itakayowafanya Wateja Wa Benki hiyo kufurahia
ubora na Ufanisi.
Tuesday, April 29, 2014
REAL YAIKUNGUTA ‘ BAYERN MUNICH, YAITANDIKA 4-0 NA KUIVUA UBINGWA WA ULAYA
Tumewaangamiza; Ronaldo kushoto akishangilia baada ya kufunga bao la tatu lililoikata maini kabisa Bayern Munich |
Maana
yake- Bayern wamevuliwa ubingwa wa Ulaya kwa kipigo cha jumla cha mabao
5-0, baada ya awali kuchapwa 1-0 Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini
Madrid katika Nusu Fainali ya kwanza na Real inaingia Fainali kwa mara
ya kwanza baada ya miaka 12, ambako itakutana na ama Chelsea au majirani
zao Atletico Madrid ya Hispania pia.
Shujaa
wa Real alikuwa ni Sergio Ramos aliyefunga mabao mawili, la kwanza
dakika ya 16 pasi ya Luka Modric na la pili dakika ya 20 pasi ya Pepe
kabla ya Mwanasoka wa Bora Dunia, Cristiano Ronaldo kumaliza kazi kwa
kufunga mabao mawili dakika ya 34 pasi ya Gareth Bale na dakika ya 90.
Kipindi
cha pili, Bayern inayofundishwa na kocha Mspanyola, Pep Guardiola
ilijikaza na kukataa kuruhusu mabao zaidi, hivyo kukubali kutema taji
kwa kichapo cha 5-0.
Real
inayofundishwa na Mtaliano Carlo Ancelotti sasa inasubiri mshindi wa
jumla wa Nusu Fainali ya pili kesho Uwanja wa Stamford Bridge kati ya
wenyeji Chelsea na Atletico Madrid, baada ya sare ya O-O katika mchezo
wa kwanza Hispania ili kukutana nayo katika fainali Jumamosi ya Mei 24,
mwaka huu Uwanja wa Sport Lisboa mjini Benfica Ureno.
Kikosi
cha Bayern Munich kilikuwa: Neuer, Lahm, Dante, Boateng, Alaba,
Schweinsteiger, Kroos, Ribery/Gotze dk73, Muller/Pizarro dk73 na Robben,
Mandzukic/Martinez dk46.
Real
Madrid: Casillas, Carvajal, Pepe, Ramos/Varane dk75, Coentrao, Alonso,
Modric, Di Maria/Casemiro dk84, Ronaldo, Bale na Benzema/Isco dk80.
MTANGAZAJI MAARUFU TSAKA SSALI AMTEBELEA MH LOWASA OFISINI KWAKE LEO
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akifurahi jambo wakati akiwa katika mazungumzo na mtangazaji maarufu wa Kituo Cha runinga Cha Serikali ya Marekani (VOA),Tshaka Ssali. |
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akizungumza na mtangazaji maarufu wa Kituo Cha runinga Cha Serikali ya Marekani (VOA),Tshaka Ssali aliemtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.Ssali ambaye amejijengea umaarufu duniani kwa kuwahoji viongozi maarufu hususan wa Afrika, alimtembelea Mh Lowassa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje. |
MALAWI KUWASILI MEI 1 KUIVAA STARS
Timu
ya Taifa ya Malawi (Flames) inatarajiwa kuwasili nchini Mei 1 mwaka huu
kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Mei 4
mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Flames yenye msafara wa 31
utakaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa
Miguu cha Malawi (FAM) utaingia Mbeya kwa usafiri wa barabara. Wachezaji
katika msafara huo ni 20.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha
mpya, Mart Nooij tayari ipo jijini Mbeya kujiwinda kwa mechi hiyo ikiwa
ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Zimbabwe
itakayochezwa jijini Dar es Salaam kati ya Mei 16 na 18 mwaka huu.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
DILI LIMEKAMILIKA! DIDIER KAVUMBAGU AMWAGA WINO AZAM FC
Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
DIDIER
Kavumbagu kwaheri Yanga. Hii ni baada ya mchana wa leo kusaini mkataba
wa mwaka mmoja na mabingwa wapya wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu
ya Azam fc.
Taarifa hii imethibitishwa na meneja wa Azam fc, wana Lambalamba, Jemedari Said.
“Kavumbagu tumemalizana nae na amesaini rasmi mkataba wa mwaka mmoja, so tutakuwa nae msimu ujao kwenye kampeni ya kutetea ubingwa wetu pamoja na michuano ya klabu bingwa ya Afrika,” alifunguka Jemedari
Mshambuliaji
huyo hatari na nahodha wa timu ya Taifa ya Burundi ameamua kumwaga wino
Azam baada ya Uongozi wa Yanga kusuasua kumpa mkataba mwingine baada ya
ule wa miaka miwili kumalizika.
UJANJA UJANJA WA TAASISI ZA MIKOPO NCHINI WAWAKERA LHRC,SASA WAIGEUKIA SERIKALI,WATOA OMBI NZITO,SOMA HAPA
Kaimu mkutugenz wa uradi huo kutoka LHRC wakili FLAVIANA CHARLES akizungumza na wanahabari mapema leo jijini dar es salaam juu ya mradi huo |
Kituocha sheria na haki za binadamu Tanzania LHRC
kimeitaka serikali kuunda mamlaka rasmi ya kusimamia taasisi zinazijuhusisha
katika kutoa mikopo kwa wajasiriamali nchini ili zitoe mikopo yenye riba nafuu
na tija kwa watanzania tofauti na sasa ambapo taasisi nyingi za utoaji wa
mikopo zimekuwa zikutoa mikopo kwa riba kubwa ambayo imekuwa ikiwafanya
watanzania kukata tamaa katika kupata mikopo hiyo.
Hayo yamesemwa leo jijini dar es salaam na kaimu mkurugenzi wa mradi maalum wa kazi za staha unaoendeshwa na kituo hicho wakili FLAVIANA CHARLES wakati akizungumza na wanahabari kuhusu mradi unaoendeshwa na kituo hicho kwa kushirikiana na shirika la ujerumani linalohusika na idadi ya watu la DSW mradi wenye lengo la kuendeleza miradi ya kazi za staha kwa wananchi walioajiriwa katika sekta zisizo rasmi.
Mmoja wa watanzania anayenufaika na mradi huo BAKARI ALLY MOHAMED akizungumza na wanahabari |
Wakili
FLAVIANA amesema kuwa baadhi ya taasisi zimekuwa sio rafiki kwa wajasiriamali
ambapo wamekuwa wanalenga zaidi kuwafilisi wajasiriamali hao kwa kutoa mikopo
yenye riba kubwa na hatimaye kuuza vitu ambavyo watu wanakuwa wameweka kama
dhamana jambo ambalo limekuwa likiwafanya watu kushindwa kwenda kukopa katika
taasisi hizo ambapo ameitaka serikali kuhakikisha inaunda mamlaka maalum ya
kushughulikia tatizo hilo
Aidha
amesema kuwa tasisi nyingi za utoaji wa mkopo zimekuwa hazijasajiliwa kisheria
jambo ambalo limekuwa likileta matatizo
pale ambapo linapowakopesha watu na mwisho wa siku kubaini kuwa wametapeliwa na
taasisi hizo,ambapo amesema kuwa kesi zaidi ya 26 zimeripotiwa katika kituo
hicho kwa mwaka huu juu ya utapeli na ukiukwaji wa sheria unaofanywa na taasisi
hizo za mikopo,ambapo wengi wanalenga tu kutaifisha tu mali kwa kuweka masharti
ya ujanja ujanja ujanja.
Wanahabari mbalimbali wakisikiliza kwa makini mapema leo |
Mradi
huo unaoendeshwa na kituo hicho cha sheria umekuwa ukifadhiliwa na umoja wa
ulaya EU ambapo mradi huo umekuwa ukiendeshwa katika halmashauri tatu zilizopo
kanda ya kaskazini ambazo ni MERU,ARUSHA NA BABATI,
Subscribe to:
Posts (Atom)