Tuesday, April 29, 2014

UJANJA UJANJA WA TAASISI ZA MIKOPO NCHINI WAWAKERA LHRC,SASA WAIGEUKIA SERIKALI,WATOA OMBI NZITO,SOMA HAPA

Kaimu mkutugenz wa uradi huo kutoka LHRC wakili FLAVIANA CHARLES akizungumza na wanahabari mapema leo jijini dar es salaam juu ya mradi huo
Kituocha sheria  na haki za binadamu Tanzania LHRC kimeitaka serikali kuunda mamlaka rasmi ya kusimamia taasisi zinazijuhusisha katika kutoa mikopo kwa wajasiriamali nchini ili zitoe mikopo yenye riba nafuu na tija kwa watanzania tofauti na sasa ambapo taasisi nyingi za utoaji wa mikopo zimekuwa zikutoa mikopo kwa riba kubwa ambayo imekuwa ikiwafanya watanzania kukata tamaa katika kupata mikopo hiyo.
        
           Hayo yamesemwa leo jijini dar es salaam na kaimu mkurugenzi wa mradi maalum wa kazi za staha unaoendeshwa na kituo hicho wakili  FLAVIANA CHARLES  wakati akizungumza na wanahabari kuhusu mradi unaoendeshwa na kituo  hicho  kwa kushirikiana na shirika la ujerumani linalohusika na idadi ya watu la DSW mradi wenye lengo la kuendeleza miradi ya kazi za staha kwa wananchi walioajiriwa katika sekta zisizo rasmi.

Mmoja wa watanzania anayenufaika na mradi huo BAKARI ALLY MOHAMED akizungumza na wanahabari

   Wakili FLAVIANA amesema kuwa baadhi ya taasisi zimekuwa sio rafiki kwa wajasiriamali ambapo wamekuwa wanalenga zaidi kuwafilisi wajasiriamali hao kwa kutoa mikopo yenye riba kubwa na hatimaye kuuza vitu ambavyo watu wanakuwa wameweka kama dhamana jambo ambalo limekuwa likiwafanya watu kushindwa kwenda kukopa katika taasisi hizo ambapo ameitaka serikali kuhakikisha inaunda mamlaka maalum ya kushughulikia tatizo hilo

         Aidha amesema kuwa tasisi nyingi za utoaji wa mkopo zimekuwa hazijasajiliwa kisheria jambo ambalo limekuwa likileta  matatizo pale ambapo linapowakopesha watu na mwisho wa siku kubaini kuwa wametapeliwa na taasisi hizo,ambapo amesema kuwa kesi zaidi ya 26 zimeripotiwa katika kituo hicho kwa mwaka huu juu ya utapeli na ukiukwaji wa sheria unaofanywa na taasisi hizo za mikopo,ambapo wengi wanalenga tu kutaifisha tu mali kwa kuweka masharti ya ujanja ujanja ujanja.

Wanahabari mbalimbali wakisikiliza kwa makini mapema leo

Mradi huo unaoendeshwa na kituo hicho cha sheria umekuwa ukifadhiliwa na umoja wa ulaya EU ambapo mradi huo umekuwa ukiendeshwa katika halmashauri tatu zilizopo kanda ya kaskazini ambazo ni MERU,ARUSHA NA BABATI,


No comments: