Na Karoli Vinsent
MCHAKATO wa Katiba mpya wazidi kumpasua Kichwa Samweli
Sitta,sasa amuangukia Rais Jakaya Kikwete na kumuomba aongeze mda wa Vikao vya
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
Hayo,yamesemwa leo na
Mwenyekeiti wa Bunge maalum la Katiba,Samweli Sitta wakati alipokuwa
akiwatembelea Viongozi Dini Jijini Dar es Salaam,ambapo amesema kutokana na
mchakato ulipofikia unahitaji mda zaidi.
“Jana Nilionana na Rais Kikwete na tumemwomba akubali
kuongeza mda kwa Siku 20 ili Bunge liwapishe Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
na Wabunge wa Muungano ili waweze kwenda kujadili Bajeti ya Serikali kwa mda wa
Miezi miwili”
“Tunamanisha kwamba Vikao vya Bunge hili la katiba ifikapo
Tarehe 28 mwezi huu itakuwa imetimia siku 70 ambazo ndizo tulizopewa
kikanuni,na ukisoma Sheria namba 83 inasema siku ni hizo tu zitumike kufanya
kazi,na ikifika tarehe hiyo tutasitisha shuhuri za bunge la Katiba na Kupisha
bajeti ya Serikali”
Sitta ambaye pia Waziri wa Uhusiano wa Afrika Mashariki amezidi kusema bajeti ya Serikali itachukua
miezi miwili yaani mwezi wa Tano na wa sita na na mwezi wa saba wabunge
watapewa mda wa kwenda kuwa kuwatembelea wananchi wao,na kuhusu vikao vya
bunge la katiba vitaendelea mwezi wa nane ambapo Rais atatangaza Tarehe
ya kuanza vikao vya bunge la katiba kwenye Gazetia la Serikali .
Vilevile Sitta amesema wamefika maamuzi hayo kutokana na
suala muhimu la Bajeti ya Serikali,na ipo kanuni ambayo itampa mamlaka ya
kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment