Wednesday, April 16, 2014

HATARI TUPU---BAADA YA KUTOKA BUNGENI,HII NDIO POST YA JULIUS MTATIRO.SOMA ALIYOANDIKA

TUMEJIONDOA RASMI KATIKA MCHAKATO WA KATIBA;

  Tumeamua kuwaachia CCM waendelee na mchakato wa katiba wanayoitaka.

        Kwa sababu wameyakataa maoni ya wananchi, na Sasa wameanza vitisho kwenye makanisa, ati wananchi wakipitisha serikali Tatu Wao CCM wataikabidhi nchi iongozwe kijeshi ni vema Sasa tuwaache.

       Kwa nia njema kabisa, hatutaki kuwa sehemu ya matusi, kauli nzito kabisa za ubaguzi na kila aina ya upuuzi.
Kama CCM walikuwa na katiba yao wacha waendelee kutengeneza. Sisi tunarudi kwa wananchi.

     Katiba mpya itapatikana tu pale kutakapokuwa na nia njema hasa kutoka kwa vyama kinachoongoza dola.
Mungu ibariki Tanzania!

No comments: