TUME Ya Vyuo Vikuu nchini
(TCU) imepata muarubaini wa kudhibiti ongezeko la ada nchini kutokana na vyuo vikuu nchini kuongeza ada kiholela bila
mipangilio.
Hayo,yalisemwa mda huu na
Kaimu katibu mtendaji wa Tume hiyo,profesa Mwagishi Mgasa wakati wa Mkutano na
waandishi wa Habari makao makuu ya Tume hiyo Jijini Dar es Salaam,ambapo
alieleza wamefikia maamuzi hayo kutoka na kuwepo malalamiko kutoka kwa wananchi
juu ya ongezeko la karo linalotozwa na baadhi vyuo.
“Tumezindua mfumo wa
kutathimini ada za vyuo ambao ulizinduliwa na Waziri wa elimu Dr Shukuru
Kawambwa kwa lengo la kupambana onezeko kubwa la ada linalotozwa na baadhi ya
vyuo vikuu hapa nchini na kwa sasa wananchi wanaangaika sana hususani wanafunzi kutokana na ada kubwa
zinazotozwa”alisema Profesa Mgasa
Vilevile Profesa Mgasa alisema mfumo huu
utasaidia kupunguza ongezeko la ada nchini,na alizidi kusema kuongeza walianza
kufanyia utafidi na kubaini vyou vinaweza vikajiendesha pasipo kutegemea karo
kutoka kwa wananfunzi.
“Mfumu huu ni mzuri utasaidia
wananchi sana,kwanza hawezekani leo vyuo vitegemee ada kwa wanafunzi
kujiendesha kwani lazima chuo kitegemee asilimia75 kutoka kwa wananfunzi na
asilimi 25 kutoka vyanzo vengine ili kuaacha utegemezi wa kujiendesha kutoka kwa wanafunzi kwani itasadia kupunguza
mzigo kwa wanafunzi”alizidi kuongeza profesa Mgasa
Aidha Profesa mgasa aliwataka wanafunzi nchini kutoka vyuo
vikuu mbalimbali nchini kutolipa ada kwa
kutumia Fedha za kigeni yaani Dola na kama kipo
chuo kinafanya hivyo basi watoe taharifa kwenye Tume hiyo ili hatua zichukuliwe
kwenye vyuo hivo.
Kuhusu wanafunzi kununua
Andiko yaani( Desertation)
Profesa Mgasa alisema kwa
sasa Tume hiyo imeanzisha utaratibu wa kupambana ununuaji wa Desertation na
wanafunzi wa Vyuo vikuu nchini wakati wa kumaliza elimu yao.
“Kwasasa tume hii imejipanga
kupambana na tabia hizi na kutoka kwa wanafunzi wanaofanya Tabia ya kununua,kwa
sasa tumevitaka vyuo vikuu na vyuo vya
kati walete nakala zote za Andiko yaani (Desertation) ya kila mwananfunzi hapa TCU ili kubaini kama
yuko mwanafunzi ambae atafanya hivyo na
kama yuko atafutiwa shahada yake”alisema Mgasa
Vilevile tume hiyo iko mbioni
kuanzisha mtambo ambao utaweza kubaini watu watakanakili Dersatation za
wengine.
“Kwa sasa nakipongeza Chuo
kikuu Huria nchini kuanzisha mtambo
ambao unaweza kubaini wanafunzi wanaonakili Andiko yaani(Dersatation)na sisi tuko mbioni kuweka mtambo kama
huo iliuweze kupambana na watu wenye tabia hii”alisema Mgasa
No comments:
Post a Comment