Friday, May 30, 2014

HALFA YA KUKABIDHI MTAMBO WA MFUMO WA MAWASILIANO WA MASAFA MAREFU KWA JESHI LA MAJI YAFANYIKA

Balozi wa Marekani Nchini Lt.Kevin Balisky akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Silima wakati wa halfa ya kukabidhi  mtambo wa mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa jeshi la maji, masaada huo umetolewa na Serikali ya Marekani kupitia mradi wa AFRICO,leo jijini Dar es salaam.
pix 3 (1)Naibu Waziri wa Mambo ya ndani, Pereira Silima (kulia) akizindua mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa kikosi cha askari wa maji katika halfa iliyofanyika  leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni  Balozi wa Marekani nchini, Lt. Kevin Balisky,mtambo huo umetolewa na Serikali ya  Marekani kupitia mradi wa AFRICO kwa ajili ya kusaidia kudhibiti uhalifu wa majini na kuweza kutambua vyombo na shughuli zote zitakazofanyika katika maji.

pix 4Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Pereira(kulia) Silima akisiliza maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa mawasiliano Norman(katikati) kuhusu utendaji kazi wa mtambo wa mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa ajili ya kudhibiti usalama wa majini kwa kikosi cha askari maji leo jijini Dar es Salaam, anayeangalia kushoto ni  Balozi wa Marekani nchini, Lt. Kevin Balisky.
pix 5Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Pereira Silima, (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja ya viongozi wa jeshi la Polisi na Balozi wa Marekani nchini Lt. Kevin Balisky (wa tatu kulia waliokaa) katika halfa ya kupokea msaada wa mtambo wa mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa kikosi cha askari wa maji katika halfa iliyofanyika  leo jijini Dar es Salaam.
pix 6Kikundi cha Burudani kikitumbuiza katika halfa ya kukabidhi mtambo wa mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa ajili ya kudhibiti usalama wa majini kwa kikosi cha askari maji leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Lorietha Laurence-Maelezo

No comments: