Meya Wa Manispaa ya Ilala Mh Jery Silaa Wa Kwanza kulia akifika eneo la Tabata St Marrys kukagua kipande cha barabara huyo ambacho kimezua mgogoro baina na Manispaa na Shirika la maji safi na salama DAWASA.
Akaamua kupanda kwa kasi baaada ya vizuizi kutolewa na yeye mwenyewe. |
Pembenini maji yaliyotuama baada ya Bomba la Dawasa kupasuka Hivyo kuleta usumbufu kwa mkandarasi kukamilisha ujenzi wa eneo hilo. Meya wa Manispaaa ya Ilala Mh Jerry Silaa ametembelea eneo la Tabata-St Marys kujionea maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na pia kuweza kuona mabomba ambayo yanaleta mgogoro baina ya mkandarasi na Manispaaa na Dawasa,Akiwa eneo hilo la St Marys Mh Jerry Silaa ameweza kujionea namna mabomba ya Dawasa ambavyo yamepita katikati ya barabara na pembezoni yakiwa katika kima kifupi hivyo kumzuia mkandarasi kuendelea na ujenzi wake. Akiongea na vyombo vya habari Mh Meya Amesema kuwa barabara hiyo imetumia gharama za takribani bilioni 1 lakini imeshindwa kumalizika kwa wakati kwa sababu ndogo ya Dawasa kutokushirikiana nao ili kuweza kumpa mkandarasi ramani kamili ya bara bara hiyo,Meya Silaa akaongeza kuwa wameshawasiliana na wenzao wa Dawasa kuhusu tatizo hilo lakina wamekuwa hawapewi majibu kwa wakati na ya kuridhisha. Naye mkandarasi wa eneo hilo Bwana George Lupia amesema kuwa alipewa ramani na manispaa ambayo haikuonysha kama kuna mabomba ambayo yamepita hapo,lakini wakati ameanza kuchimba barabara hiyo ndio akakutana na mabomba hayo,Mkandarasi huyo akaongezea kwamba alishawasiliana na Dawasa kitambo sana lakini hapewi majibu ya kuridhisha kuhusu kushirikiana nao kuhamisha bomba hizo. Naye Diwani wa kata Hiyo Bibi Mtumwa Mohhamed amesema wanainchi wa eneo hilo wanapata tabu sana kwa kuwa magari yao hayawezi kutoka ndani wala kuingia kwa kuwa barabara imechimbwa kwa kina kirefu sana,hivyo amewaahidi wanainchi wa eneo Hilo kwamba wanaendelea kulitatua tatizo hilo na wenzao wa dawasco ili kuweza kuhamisha mabomba ya eneo hilo. |
No comments:
Post a Comment