Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
HATIMAYE kamati ya rufani ya shirikisho la soka Tanzania, TFF imemaliza kujadili rufani ya mgombea wa urais katika uchaguzi wa klabu ya Simba sc unaotarajia kufanyika juni 29 mwaka huu, Michael Richard Wambura.
Kamati ya Rufani chini ya mwenyekiti wake,wakili, Julius Luhaziya imekaa kuanzia jana juni 9 mpaka jioni ya leo (juni 10) katika Hoteli ya Courtyard iliyopo Upanga , jijini Dar es salaam.
Kikao hicho kilichojaa usiri mkubwa kimemalizika jioni ya leo na kufikia maamuzi juu ya rufani ya Wambura, lakini mwenyekiti wa kamati , Lugaziya ataongea na waandishi wa habari kesho mchana majira ya saa 6:00 katika ukumbi wa mikutano wa TFF.
No comments:
Post a Comment