Na Karoli Vinsent
KATIKA kile kinachotafsiriwa huwenda chama
cha Mapinduzi CCM kikapasuka Vipande vipande kwenye uchaguzi Mkuu Mwakani
zimeanza kuonekana,Baada ya Makundi yanoyosaka Urais kuzidi kuongekeza, mtandao
huu umebaini.
Makundi hayo,ambayo yameapa kutumia kila njia
kuhakikisha yanamtoa mtu wao mmoja kuja kumrithi Rais anayemaliza mda wake Jakaya
Kikwete,hivi sasa limeibuka kundi jengine ambalo limepanga kuhakikisha
mmoja wao anakamata nafasi hiyo ya Juu ya nchi.
Kundi hilo jipya liloibuka ambalo linajiita kwa kingereza “three
man”yaani wanaume watatu, ambao ni aliyekuwaWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba
pamoja na aliyekuwa waziri wa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja.
Kundi hilo ni jipya limeibuka ikiwa
miezi michache baada chama cha Mapinduzi CCM,ikiwa tayali
imewafungia Makada ambao walianza kuonyesha dalili za kutaka Urais ndani ya chama hicho kwenye
uchaguzi Mkuu mwakani,
Makada hao ni pamoja Waziri
Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond,
ambaye pia ni Mbunge wa Monduli,Edward Lowassa, wengine ni
Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye pamoja na aliyepata
kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja,January Makamba,Samweli
Sitta,ambao wote kwa pamoja wanatumikia kifungo cha miezi 12 kutofanya kampeni
za kusaka urais.
Kundi hilo jipya limejipanga kuhakikisha
linatumia ushawishi walikuwa nao ndani ya Halmashauri kuu Chama cha Mapinduzi
NEC ,na kwa wananchi vilevile kuhakikisha wanaipunguza kasi ya waziri
mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa,ambaye anaonekana kuwa mwiba mkali ndani ya
chama hicho kikongwe barani Afrika.
Naye mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama
cha Mapinduzi NEC kutoka mikoa ya Nyanda za juu kusini aliyezungumza na
Mwandishi wa Mtandao huu ambaye hakutaka Jina lake liandikwe kwenye mtandao huu
alisema Chama chake kinaelekea kubaya kutakana na kila mtu kutaka urais.
“Yaani hizo taarfa mimi mwenyenyewe
nimezisikia kwamba limeundwa kundi jipya linalojiita “three man” eti nalo
linataka kumtoa mtu miongoni mwao ili achukue Urais kwenye uchanguzi mkuu
mwakani hivi jamani akuna vitu vyengine vya kufikilia mpaka urais”
“Nchi leo inamatatizo lukuki serikali
haina pesa na bajeti inasuasua huko bungeni,leo viongozi wanafikiria urais,na
mimi naona kuna ishara mbaya sana chama hichi kupagalanyika mwakani na sababu
itakayosabisha ni hawa wasaka urais”alisema Mjumbe huyo
Duru za kisiasa zinasema kuongezeka
makundi ya chama hicho zinaashiria Mpasuko mkubwa ambao utakitikisa chama hicho
ambacho ni Kikongwe ambacho kipo madarakani,na mpasuko huo ambao haujawahi
kutokea tangu chama hicho kianzishwe.
Kwa upande wake Kigogo kutoka ndani wa
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM, UVCCM,aliyezungumza na mwandishi wa
mtandao huu kwa sharti la kutoandikwa jina lake mtandaoni, alisema makundi hayo
yanayozidi kuibuka kwenye chama hicho ni njama zinazofanywa ili kumpoteza
kabisa Waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa.
“Hizo njama tu ndugu yangu ambazo
zinafanywa na watu wasiomtaka Edward Lowassa kushika nafasi ya Urais ndio maana
wanajifanya kuanzisha makundi mapya ili kumzima kabisa mzee Lowassa”
“Na sisi vijana tunajua kwamba makundi
hayo yanaanzishwa ili kumzima lowassa,nakuhakishia kaka sisi hatutakubali na
tuko tayari kukihama hata chama chenyewe kama endapo jina la Lowassa kama
litakatwa pale NEC”alisema Kigogo huyo kutoka UVCCM
Naye mchambuzi na Msomi wa Masuala ya
Siasa kutoka Chuo kikuu cha Dodoma Seiph Yahaya ,alisema chama cha mapinduzi
kingojee kupasuka,kutokana na Chama hicho kutumia njia mbaya kumzima Lowassa
katika harakati zake za kutaka Urais.
“Hivi nani asiyejua kwamba ule mpango wa
kuwakataza bodaboda kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam ni miongoni mwa
mikakati ya kumpotezea sifa mzee wetu Lowassa,kwani hata hiyo sheria
wanayoisema kwamba hao bodaboda kuingia katikati ya jiji,imetungwa lini si
zaidi ya miaka miaka saba nyuma”
“Kwanini waianze kuitekeleza leo baada
ya Edward Lowassa kuzindua “Saccos” ya hao bodaboda ambayo iliyompa umaarufu
sana jiji humo,sasa wamezikataza pikipiki hizo,na sasa siwezi
kushangaa hata makundi mapya yaibuke tunajua tu wanataka kumzima kiongozi
huyo”alisema Seiph Yahaya.
No comments:
Post a Comment